Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Mdogo wangu ShesRise_1 hii mada sikuiona kabisa, halafu ipo toka juzi kwanini hukuni tag ?

Kimsingi πŸ€”

Mimi sijawahi kutamani hilo jambo, kwa sababu viumbe hai tuna sifa saba za msingi, ikiwemo Movement, Respiration, Growth, Reproduction, Excretion, Nutrition na Sensitivity

Sasa, kama nitqtamani nisizeeke kabisa, wakati Growth ni mojawapo ya sifa za viumbe hai, nitakuwa kiumbe hai kweli au nitakuwa nimeanza kuishi nje ya mfumo wa biolojia? πŸ˜‚πŸ˜‚

Halafu, ukitamani kubaki palepale maisha yako yote, si utakuwa OLD FASHIONED wakati dunia yenyewe inabadilika kila siku? 🀣

Kuna mambo mengine kuyatamani ni zaidi ya tamaa, ni kama unataka kuomba ruhusa ya kubishana na Mungu kuhusu kanuni za uumbaji!

TUKUBALI TU TUZEEKE LAKINI UZEE WETU UWE NA MWISHO MZURI KAMA MZEE WARIOBA, BABA WA TAIFA JK NYERERE etc
 
Mdogo wangu ShesRise_1 hii mada sikuiona kabisa, halafu ipo toka juzi kwanini hukuni tag ?
Kaka huja ni follow kwani?
Kwani unadhani hii mifumo ingekua kinyume na ilivyo sasa dunia ingekuwa mbaya ?

Ni kwa vile tumezoea mifuno iliyopo
Lakini kama kungekuwa na mfumo mwingine basi tungezoea huo mfumo kama tulivyozoea huu wa sasa
Halafu, ukitamani kubaki palepale maisha yako yote, si utakuwa OLD FASHIONED wakati dunia yenyewe inabadilika kila siku? 🀣
Old fashioned? kwamba kadri unavyozeeka ndio unaenda na fashione labda kama sielewi mie
Kuna mambo mengine kuyatamani ni zaidi ya tamaa, ni kama unataka kuomba ruhusa ya kubishana na Mungu kuhusu kanuni za uumbaji!
Kuingiza swala la Mungu hapa ni kutaka kuhamisha mjadala
TUKUBALI TU TUZEEKE LAKINI UZEE WETU UWE NA MWISHO MZURI KAMA MZEE WARIOBA, BABA WA TAIFA JK NYERERE etc
Shukran sana bro
 
Kaka huja ni follow kwani?

Kwani unadhani hii mifumo ingekua kinyume na ilivyo sasa dunia ingekuwa mbaya ?

Ni kwa vile tumezoea mifuno iliyopo
Lakini kama kungekuwa na mfumo mwingine basi tungezoea huo mfumo kama tulivyozoea huu wa sasa
Daaah πŸ˜‚, Sasa hapo umehamisha mjadala kutoka kwenye biolojia kwenda kwenye falsafa ya mazoea ya binadamu
Nakubaliana nawewe kwamba binadamu huzoea mazingira na mifumo wanayoishi ndani yake lakini kuzoea mfumo fulani hakumaanishi kwamba kanuni za asili zinazotawala mfumo huo zinabadilika kwa sababu tu tumeuzoea. Kumbuka mifumo inaweza ikabadilika lakin kanuni za asili haziwezi kubadilika.

Kwa mfano unaweza ukala mikate daily lakini chooni utaenda tu ?
 
Daaah πŸ˜‚, Sasa hapo umehamisha mjadala kutoka kwenye biolojia kwenda kwenye falsafa ya mazoea ya binadamu
Tokea hapo mada ilikua ya falsafa
Nilimaanisha kama asili ingeumbwa vingine tofauti na ilivyo ingezoeleka tu
Kwa mfano unaweza ukala mikate daily lakini chooni utaenda tu ?
Hii mifano hata sielewi bro
 
Old fashioned? kwamba kadri unavyozeeka ndio unaenda na fashione labda kama sielewi mie
πŸ˜‚πŸ˜‚ Sijamaanisha kwamba kadri unavyozeeka ndivyo unavyoendana na fashion! Nimetumia Old fashioned kumaanisha kitu kilichobaki katika hali ileile wakati mazingira yanabadilika

Angalia fashion yenyewe leo unavaa size M, miaka inaenda baadaye unavaa XL! 🀣 Mwili nao unapitia mabadiliko, kutoka utoto hadi ujana na uzee.

Sasa fikiria dunia inabadilika kila siku, lakini wewe unabaki vilevile milele (FOREVER YOUNG)Si utakuwa bidhaa ya zamani kwenye soko la viumbe hai? πŸ˜‚πŸ˜‚

Au ulikuwa unataka ubaki kama Mende πŸͺ³ tu ? Kubali biology ichukue nafasi yake japo ni ngumu kumeza
 
Duh noma aisee naona lugha gongana mimi sidhani kama kutokuzeeka kuna tatizo aisee

Kwahiyo ukizeeka ndio unaendana na dunia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…