Umewahi kupigwa hadharani? Mimi yalinikuta!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Hello,

Kuna muda hasa utotoni na tukiwa vijana wadogo huwa ni kawaida mtu ajitetee kwa kupigana, Hata wanyama hupigana ili kutafuta haki ama kuonyesha dominance.

Sasa katika mapambano haya kuna muda unakuta huna tofauti na mtu alievamia mtumbwi wa vibwengo, unaishia kuchapika mbele ya hadhara, Loh aibu hiyo isikieni tu.

Binafsi nakumbuka katika siku niliyopoteza pambano ilikuwa nikiwa kidato cha tano (form 5), Pambano lilikuwa ni mimi mtoto wa town mwenye rekodi yangu nzuri tu tangu shule ya msingi na mtaani nishakalisha wengi, niliyakanyaga kwa jamaa flani katoka kijijini huko mikoani namuona mshamba mshamba.

Nilikuwa napenda kumtania tania ila kuna siku alimaindi sana tukiwa darasani, nikamwambia atulize mshono jogoo wa shamba hawiki mjini, darasani pale nusu tudundane lakini tukakubaliana tuyamalize baada ya vipindi, mida ya saa saba hivi baada ya kutoka kwenye vipindi tukaenda nyuma ya ukuta wa shule ndio ilikuwaga sehemu ya kuyamaliza matatizo kiume.

Nikawa naruka ruka ile kujiona kama tyson kumtambia huyo jamaa wa bush jinsi watoto wa mjini tunavyopasha kabla ya mfumuo, mtoto wa town nikatumia mbinu yangu ya surprise attack, ile hata hajajiandaa vizuri nikamrushia ngumi kama mbili hivi, hii mbinu nishaitumia kumaliza pambano mapema ila kwa huyu jamaa hali ikawa tofauti, kwake ni kama ngumi zangu zilimpapasa yani kama hazijamuingia hata, alinirushia ngumi nikakwepa nikaongeza ujazo kwenye ngumi yangu kudhania za kwanza sikuzijazia lakini jamaa ilikuwa ni kama napiga gunia la mchele daaah!

Yeye ngumi nyingi akirusha nakwepa ila chache zinazonikuta ni zinauma jamani, ni kama napigwa na mawe, maumivu haya yalinipa hasira nikawa namtupia upper cut lakini wapi, narusha za chembe lakini wapi, narusha teke lakini ni kama napiga gunia tu, aisee!

yeye ngumi yake akiirusha inauma jamani acheni tu.
Ilibidi nikimbie pambano lakini watu walikuwa wametuzunguka wananisukuma nirudi ulingoni, najaribu kuzikinga ngumi za jamaa lakini jamaa ngumi zake zinaumiza mpaka mikono nayotumia kujikinga, na nikimrushia jama ngumi ni kama napiga gunia la mchele, kiukweli nilikata tamaa, tena kuna muda alinisoma ile navyomrushia ngumi nae anarusha yake na ikinikuta ilikuwa inanipasua kweli kweli.

Bahati yangu viranja walikuja kutuachisha lakini nilikuwa nimetandikwa si mchezo.
Nakumbuka tu baada ya wiki tulikuwa marafiki sana na huyo jamaa lakini aibu niliyoipata ile siku siwezi kuja sahau.
 
We unacheza na njemba kutoka bush.
Zinakuwa na nguvu simchezo zinakula vyakula mlima. ..

Mini kuna jomba moja limetoka bush
Nikalichukulia ndezi ndezi nikazipanga kwani nilitoboa kila nikipiga jomba nikama nalitekenya

lilikaniotea nilipigwa ngumi ya uso mpaka macho yakacheza cheza.nkasema mungu wa yosefu ni mungu wadaudi...
Nkaona usntanie nikala chocho..
 
mbona wako sio mtumbwi wa vibwengo,wangu ni mtumbwi wa majini.
sipendi ugomvi mpaka umri huu kisa nilipigwa na mwanamke"mwanamke" nikiwa darasa la tatu tu.

shuleni nilikuwa mpenda sifa sana,halafu maarufu shule nzima nikiwa la kwanza tu.natongoza mpaka wadada wa darasa la saba wengine wanaambizana wanacheka nikipita,hwaelewi huo ujasiri nautolea wapi!!!!

tukiwa darasani nakumbuka demu mmoja ambaye niko naye darasani alikuja akanambia nini sijui??vile namwona mshamba sio hadhi yangu maana namingo na wakubwa nikamjibu mbovu,darsa zima likacheka wakaanza kumzomea,nisijue ana kinyongo na mimi nikaja kumuuliza nini sijui'akaninyooshea kidole nikakiputa kwamba aache dharau mimi sio wa kunyooshewa kidole,aisee kilikuja kibao hicho,sikutegemea kwakweli.
kujaribu kujibu mashambulizi aaah wapi!!nilichelewa akanikamata mikono,nyanyua juu akanishusha kama gunia juu ya dawati,mademu huwezi pigana naye ukiwa karibu atakuaibisha.
halafu yeye ni kama aliishaanza kuvunja ungo alinizidi pound kiasi fulani.

nilichapika kweli shati vifungo vyote kuleee,nakuja kuamuliwa sina hamu.
saa nne mapumziko napewa pole tu na warembo wangu wa madarasa mengine maana nilikuwa sitamaniki.
 
Mimi sio mgomvi na sidhani Kama nitakuja kupigana kwa umri huu niliofikia.
Ila nakumbuka nikiwa school Kuna jamaa alikuwa na misifa sanaa siku akayakanyaga kwa muhuni flani katokea sijui Nachingwea huko, aseew jamaa alikula punch moja akasimamisha pambano anaomba mashabiki tumnyang'anye jiwe jamaa kumbe ni ngumi akahisi kapigwa na jiwe. Alichekwa mpaka na madogo wa o-level.
 
Nakumbuka nilivyokuwa form1 ata wiki sijamaliza Kuna jamaa wawili form3 walikuja kutupiga mkwara Darasani kuwa Kila mtu saa4 lazima atoe 200 ya sadaka Kuna jamaa alikuwa kakaa mbele kabisa Yuko bize anaandika Hana mda na hayo matangazo basi mmoja wa wale jamaa akamsogelea nakumshika shika kichwani huku akimfokea "kwahiyo wewe unajidai kuwa bize na definitions zako hizo" yule jamaa akasimama alimtia yule sharo ngumi Moja ya shingo jamaa akaenda chini kuamka akashindwa akazima mwenzake akakimbia ikabidi tuanze kupiga kelele za kushangilia walimu na viranja wakaja wakampa first aid wapi wakampeleka hospital Toka siku hiyo kuanzia form6 walikuwa wakimwogopa huyo njemba kilikuwa kijeba kimekomaa alafu kina vigimbi
 
Nikiwa form one jamaa wa form two kaja kunichokoza kinjuka njuka. Na jamaa kubwa siwezi kupigana nalo. Jamaa alijichanganya siku moja nilikamata kisu from no where, aisee nilimkosa kisu cha shingo mpaka jamaa alikuja kuniomba msamaha nikamwambia nilikuwa nakata koromeo bahati yako. Toka siku hiyo heshima ikawepo ile kutesana kijingajinga ikaisha.
 
Back
Top Bottom