Twaha Kiduku apigwa ubingwa wa mabara WBF;nilinyofoa video zangu zote YouTube Ili Twaha Kiduku hasizione-Bondia Asemahle Wellem.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Twaha Kiduku is the most decorated fighter for now here in Tanzania kupoteza pambano kwa Msouth African kijana mdogo Asemahle Wellem"predator"kunatupatia picha ya kwamba boxing ya Tanzania bado ni ya mwaka 1947 wakati Power Ilanda na Power Mabula wakishindana kuvuta gari kwa meno,Twaha Kiduku is the best Super middle boxer this part of Africa. No 1 Tanzanian Champion!Asemahle Wellem is the best Super middle boxer this part of Africa. No 2 in South Africa.

Tunapoiongelea Afrika kusini kwenye ulimwengu wa masumbwi tuanze kwa kutambua Afrika kusini imetoa bondia bora kabisa duniani,bingwa wa dunia mkanda wa IBF heavyweight alimpiga Axel Schulz mwaka 1995,zaidi ya yote Francois Botha ndiye bondia alienda kwenye pambano la kifo dhidi ya Mike "iron" Tyson kwa ajili ya mkanda wa World heavyweight mwaka 2000 na 2002. Francois Botha amepigana na Wladimir Klitschko,Lennox Lewis, Michael Moorer na Evander Holyfield, Francois Botha anatoka Afrika ya Kusini anapotoka Bondia Asemahle Wellem aka Predator kwa uzoefu wa mapambano 200 ya ridhaa na 6 ya kulipwa,bondia Asemahle Wellem anastahili kuwa bondia hatari,lakini bondia Asemahle Wellem anakiri Twaha Kiduku ni bondia hatari na kwa kumuogopa kambi ya bondia Asemahle Wellem walinyofoa video za Asemahle Wellem kwenye YouTube ili Twaha Kiduku asizione,mpaka hapo utakubaliana nami ya kwamba Twaha Kiduku ni bondia hatari, Asemahle Wellem anasema"I learned him,that's why I beat him".

Nini kifanyike;

Ngumi ni kazi,ngumi ni ajira,ngumi ni biashara,mabondia wetu wote wajue hilo,Bondia Asemahle Wellem ni bondia mwenye akili sana,urefu wake ulimfanya aweze kudance na kumthibiti Twaha Kiduku katika nyanja zote,nafasi pekee ya Twaha Kiduku ilikuwa ni kumuweka ndani ya boksi lakini Bondia Asemahle Wellem alikuwa akitoka kwenye boksi kwa akili kubwa sana,na alikuwa akitoka kwa punch nyingi kubwa za mfululizo ni sawa na mtu aliyekiona kiama chake,alifanya hivyo hivyo kila mara Twaha Kiduku alipomuweka kwenye kona,Asemahle Wellem alitoka kwa punch nyingi za mfululizo na kukimbilia katikati ya ulingo, Mabondia Watanzania wanatakiwa wawe na akili hiyo.

Katika tasnia ya masumbwi kuna fitna duniani,tumezoea kubebwa ukiwa nyumbani lakini mpinzani wako akikuoutsmart,akikuzidi hakuna namna ya kumnyika ushindi ndio ilivyotokea kwa Bondia Asemahle Wellem aka Predator,tutoke huku twende kwenye skills na ubunifu na fitna za teknoloji,ni ajabu Bondia Twaha Kiduku hakuwahi kuona pambano hata moja la Bondia Asemahle Wellem ambae tunaambiwa ni kijana mdogo aliyecheza mapambano sita tu ya kulipwa lakini tunaambiwa amecheza mapambano 200 ya ngumi za ridhaa kwa sababu video zake zote zilichomolewa YouTube kwa sababu Moja tu Twaha Kiduku hasizione,hii ni hatari na kwa namna tulivyomuona Bondia Asemahle Wellem bila shaka anastahili jina la "Predator" urefu wake ngumi yako haiwezi kufika kwake,akidance outbox na kushambulia mfululizo akionekana mwenye dharau kuona kapata pambano mchekea.

Twaha Kiduku amepambana sana ni bondia mzuri sana tutaona pambano la pili,kwa kutomjua bondia Asemahle Wellem baada ya video zake kunyofolewa YouTube ilimfanya bondia Twaha Kiduku kumkabili Asemahle Wellem jinsi alivyokuja,mara zote alikuwa akimuwinda Asemahle Wellem kumpiga ngumi za ushindi ‘Counter Punch’ kwenye kona za ulingo lakini ngumi hizo hazikufanikiwa kwa kiasi kikubwa mbele ya bondia Asemahle Wellem aliyejua nia ya Twaha Kiduku na alicheza style yake ya "outbox" kutoka nje ya box kwa punch kali za mfululizo na alipoona hana uwezo wa kupiga punch alitumia mbinu za kushika (kukumbatia) pindi anapowekwa kwenye kona za ulingo.

Nilisimama kama shabiki wa Bondia Twaha Kiduku mwanzo mwisho nikiwa na matumaini atapiga ile ngumi yake inayotoka kama risasi ya Gobole la kutoka vilima vya Uluguru na mzinga ila sikuiona🤣Ufupi ulimzingua sana,ila kwa urefu wa Dulla Mbabe angekuwa na akili na maarifa ya Twaha Kiduku angeweza kupenyeza ngumi kwa Asemahle Wellem ila kila alivyomuwinda apige jamaa alimsoma na alikuwa mbele ya akili ya Kiduku na hakurusu wala kumpa nafasi Twaha Kiduku apige ngumi,Bondia Asemahle Wellem anasema alikaa nakuusoma mchezo wa Bondia Twaha Kiduku na kurudia video zake zote kwa muda mrefu kisha kocha wake akamuelekeza jinsi ya kumkabili,kwa hiyo Twaha kapigwa na akili tu 😂 kweli mzungu ni mzungu tu,unajua Afrika kusini imejengwa kwa akili ya mzungu,imetawaliwa na akili ya mzungu na Bondia Asemahle Wellem ametumia akili ya mzungu kumpiga Bondia Twaha Kiduku.

Nimalizie kwa kusema,bado Twaha Kiduku is still the most decorated fighter in Tanzania for now,mbali na Mwalimu Power Ilanda bado bondia Twaha Kiduku anahitaji kupiga kambi ya Francois Botha kule Afrika ya kusini kama anataka awe mithili ya "Predator" Asemahle Wellem ambae ni bondia namba mbili Afrika ya Kusini na ndie tegemeo la kesho la Waafrika ya kusini katika ulimwengu wa masumbwi.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;
Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Twaha Kiduku ana mawenge sana. Hata kwenye lile pambano lake na Dullah Mbabe kipindi kile, ilibakia kidogo tu atandikwe baada ya kupoteza network kichwani kwenye raundi za mwanzo.
 
Twaha hatumi akili kupigana anatumia miguvu mingi,anakwenda kama lingombe tu

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom