Umewahi kujiuliza kwanini upo hapa?

Mimi najua kwanini niko hapa.

Vipi wewe unajua kwanini uko hapa au ushawahi kujua majibu ya maswali yako unayapataje ?

Akili salama lazima ijue ya kuwa duniani tunaishi kwa malengo na si kwa bahati mbaya,sababu hiyo bahati mbaya hakuna anae weza kuithibitisha.
Mufti unajua kwanini upo hapa..Au unajifariji.!?
 
Safi kabisa,je hudhani kama chanzo cha sisi kuwepo hapa kinatakiwa kijulikane na ndio kitakuwa na majibu ya kwanini sisi tupo hapa na kwanini vilivyomo hapa duniani vina uhusiano kati ya kimoja na kingine ?
Swali zuri. Labda aliyetuweka hapa bado hajataka fumbo lifumbuliwe hata kizazi cha tatu na cha nne kipite. Kumbuka wamepita wengi waliokuwa na nadharia za ajabu vichwani mwao ambazo zingeletwa ktk uhalisia pengine dunia isingekuwa hapa
 
Kwanini unasema hili ni fumbo ?
Hao wali pita kwani hapakuwa na walio kuwepo kabla ya walikiwa na majibu ya swali hilo ?
Unaweza kutupa mfank wa nadharia hata moja kwayo iliyokufanya ufikie hitimisho hilo hapo mwisho wa maneno yako ?
 
Sijui kama nitakuwa sahihi kuiita hypothesis nadharia. Kama ndivyo nenda kwenye millennium prize problems ukajinyakulie US$1,000,000 endapo utafanikiwa kusolve Yang–Mills existence and mass gap
 
Mabadiliko mbalimbali yaliyoikumba sayari yetu yangetosha kutengeneza mabuku makubwa jiographia na historia na kutoa elimu sahihi wapi tumetoka na wapi tunaelekea.

Na juu ya yote kwanini tuko hapa tulipo hapa sasa. Kinyume chake uongo, uzushi vimekuwa muhimili wa elimu yetu ya zama zote.
Elimu "zenu" zipi?

Ikiwa huelewi kwanini upo hapo ulipo hiyo nayo utaiita elimu?
 
Elimu "zenu" zipi?

Ikiwa huelewi kwanini upo hapo ulipo hiyo nayo utaiita elimu?

Hivi ninyi mnakuwaje na uhakika wa pahala mlipo kwa kutegemea masimulizi ya mababu zenu na kujihakikishia kwamba mpo sahihi kiasi kwamba mnaweza kuwasadikisha na wengine ..!?

Ninacho kishangaa mimi ni kule kujiamini kwenu kwa misingi inayobadilika kwa kila mtu na tafasiri yake_ni kongwa kiasi gani kujiweka kwenye state ya kiwango hicho..!?
 
DINI YA KWELI YA MWENYEZI MUNGU NI IPI?

Kila mtu huzaliwa katika mazingira au hali ambayo si chaguo lake mwenyewe. Hupachikwa dini ya familia yake au mtazamo wa taifa lake toka mwanzoni mwa kuwepo kwake katika dunia hii. Wakati anapofikia ujana wa (miaka 13 – 20), kwa kawaida hulazimika kuamini kwamba imani ya jamii yake ndiyo imani sahihi ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo. Ingawa wakati fulani baadhi ya watu wanapokuwa wakubwa na wakaona imani nyingine huanza kuuliza na kuhoji ukweli wa imani yao. Wale wanaotafuta ukweli mara kwa mara hufikia mahali wakachanganyikiwa wanapogundua kwamba kila dini, dhehebu, au falsafa hudai ndio njia pekee iliyo sahihi kwa mwanadamu, kwani makundi yote hayo yanahamasisha watu kufanya matendo mema. Sasa ni ipi imani sahihi? Zote haziwezi kuwa sahihi, kwani kila moja hudai kuwa nyingine zote si sahihi. Sasa katika hali hiyo, yule anayetafuta ukweli vipi ataweza kuchagua njia iliyosahihi?
 
Sasa katika hali hiyo, yule anayetafuta ukweli vipi ataweza kuchagua njia iliyosahihi?

Naona kama umeishia njiani na umenisaidia nyongeza ya maulizo

Iweje uwe na uhakika wa ukiaminicho kuwa ni sahihi na ukajihisi huru kukielezea..!?

Huoni ni kama kulazimisha uhuru wa fikra wenye uhakika kwenye misingi dhaifu ya dhana, wenye kuweza kukupelekea kujiamini kwenye madhara..?
 
Mwenyezi Mungu ametupa sote akili na uwezo wa kutuwezesha kufanya maamuzi sahihi na ya maana. Nayo ni maamuzi muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Mustakabali wake unautegemea uamuzi huo, kufuatana na hilo, kila mmoja wetu lazima achunguze ushahidi uliotolewa bila kupendelea ndipo achague kile kinachoonekana kuwa ni sahihi mpaka pale ushahidi mwingine utakapotokea.
 
Hivi ninyi mnakuwaje na uhakika wa pahala mlipo kwa kutegemea masimulizi ya mababu zenu na kujihakikishia kwamba mpo sahihi kiasi kwamba mnaweza kuwasadikisha na wengine ..!?

Ninacho kishangaa mimi ni kule kujiamini kwenu kwa misingi inayobadilika kwa kila mtu na tafasiri yake_ni kongwa kiasi gani kujiweka kwenye state ya kiwango hicho..!?
Inastaajabisha
 
[
Mabadiliko mbalimbali yaliyoikumba sayari yetu yangetosha kutengeneza mabuku makubwa jiographia na historia na kutoa elimu sahihi wapi tumetoka na wapi tunaelekea.

Na juu ya yote kwanini tuko hapa tulipo hapa sasa. Kinyume chake uongo, uzushi vimekuwa muhimili wa elimu yetu ya zama zote.

Mimi niko hapa leo asubuhi hii kwa sababu nimekuja kutafuta mahitaji, yanahitajika nyumbani. Asubuhi baada ya chai, nilichukua kikapu na kunyosha njia mpaka supermarket, na ndiyo maana niko hapa supermarket. Kama sijajibu swali lako, tafadhali naomba ufafanuzi, ningepenfda kuchangia zaidi
 
Tupo hapa sababiu tulipatengenza tuwepo, na tutaendelea kuwepo kwa vile tulikuwepo, na tupo. jione wewe niwa milele, humu duniani
 
Tupo kwasababu ipo sababu ya sisi tuwepo tulipo lakini tupo tulipo kwasababu kuna sababu ambazo hatuzifahamu zinatufanya tuwepo tulipo, ina maana kuwa kutozifahamu sababu hizo ndiyo zinatupa sababu ya kuendelea kuwepo tulipo, kama tungezifahamu hizo sababu tusingekuwa na sababu ya kuwepo tulipo ina maana tungetafuta mahali pengine palipo sahihi zaidi. Elimu na Maalifa yote ya dunia yangefunuliwa kwa kila mtu, dunia ingekuwa sio sehemu salama ya kuishi kwa kuwa Elimu na Maalifa yasiyokuwa na mipaka huishia kwenye maangamizi na hii ndio sababu inayochochea amri na utii kwa kufanya bahadhi ya watu wajue na wawe na bahadhi ya vitu ili kuwe na madaraja (classes), ambayo yataleta uongozi (amri na utii).
Sasa ili kusiwe na hombwe pale ambapo pamenyimwa Elimu na Maalifa ya kweli lazima itafutwe Elimu na Maalifa m'badala hivyo ndipo panapozuka Elimu na Maalifa nusu, yaliyopotoshwa au yaliyofumbwa kabisa.
Na jambo zuri ni kuwa kuna taasisi za dini ambazo zinatufanya tuwe wanyenyekevu, watiifu na wenye kufata amri (kuwa vipofu kuufikia ukweli) na hii inatupa sababu ya kwanini tupo tulipo...Tumtumikie Mungu aliyetuumba.
cc mkuu Kiranga
 
Back
Top Bottom