Umewahi kuchapa wanao ?


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,873
Likes
8,029
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,873 8,029 280
Kama jibu ndio kwanini ulilazimika kuwachapa badala ya kuwa adhabu mbadala na kama huwachapi unawapatia nidhamu vipi?
 
MR. ABLE

MR. ABLE

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
1,477
Likes
6
Points
135
MR. ABLE

MR. ABLE

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
1,477 6 135
USIULAZIMISHE MWILI UAMBUKIZE SIKIO.
Kumchapa mtoto ni shambulio la kudhuru mwili na pengine asibadilike badala yake awe sugu,
hivyo kwa mimi huwa namuonya tu au namgombeza kwa kumwambia maneno makali yenye kumchoma mpaka anatamani ningemchapa tu shaishe kuliko kuendelea kuyasikia maneno yangu.
 
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Messages
3,614
Likes
46
Points
145
HorsePower

HorsePower

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2008
3,614 46 145
Kama jibu ndio kwanini ulilazimika kuwachapa badala ya kuwa adhabu mbadala na kama huwachapi unawapatia nidhamu vipi?
Jibu ni Yes, nilishawahi, lakini kabla ya hapo niliwahi kujaribu sana kuwaonya watoto kwa vikao na kuongea nao sana na kuwaelekeza na kuelimisha madhara ya kile walichokifanya. But walikuwa wanayarudia, nikakosa namna nikaamua siku moja moja kwa makosa makubwa niwatandike viboko. Kwa kweli njia hii pamoja na kwamba inaumiza mwili ila kwa baaadhi ya watoto imepunguza sana kasi zao za utundu usio na tija. Ninavyoona mimi si vibaya sana kumchapa mtoto kwa kipimo na kwa makosa ambayo njia ya kawaida imeshindwa kuyatatua!
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,088
Likes
368
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,088 368 180
Kuchapa ni adhabu kama adhabu nyingine,
Kwa hiyo mie adhabu ya kuchapa niliiona inafaa zaidi kwa mazingira niliyokuwepo.

Kwa nini kuchapa kusiwe adhabu mbadala ya hizo adhabu zingine??
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,088
Likes
368
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,088 368 180
Adhabu ya kuchapa inataka kupewa kipaumbele kama dhambi ya kuzini kulingana na matakwa ya jamii

Lakini je, kila mara kuchapa ndio adhabu mbaya zaidi kuliko zote??
Nilishawahi shuhudia mtoto kafeli darasa la saba, mzazi akampa adhabu ya kutompleka shule ya sekondari ya private, je adhabu nii athari zake zinalingana na kama angepewa adhabu ya kuchapwa walau viboko 6??

Ni kama sasa kuzini kunapigiwa kelele weeee, lakini athari zake za moja kwa moja kwenye jamii zinalingana athari za ufisadi, rushwa, dhuluma, kunyimwa haki, uchafuzi wa mazingira na na aina hiyo??

Hii nikiangalia kwa jicho la 'miradi' ya watu na ulaji, naweza ielewa vema zaidi labda.
Hizi ni harakati za NGO's ziweze kuishi na watu waingize siku, LAKINI zina manufaa ya aina yake
Lakini sio mzizi kabisa wa maumivu ya watoto wote katika jamii.
 
isambe

isambe

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
2,063
Likes
909
Points
280
isambe

isambe

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
2,063 909 280
Mimi adhabu ninayo wapa ni kunifulia Soksi zangu.
 
Eliphaz the Temanite

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
2,890
Likes
462
Points
180
Eliphaz the Temanite

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
2,890 462 180
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 19:18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Wakolosai 3:21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
1 Timotheo 3:4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

Hayo mambo yenu ya kukanya watoto utafikiri unalea nao utaambulia vibaka na wavuta bangi, Mtoto ukimwazibu kwa kosa alilofanya shida iko wapi, Tatizo lenu mnaweka wazazi wanaotiisha watoto wao kwenye kundi moja na child abusers! Huwezi kumchoma moto mwanao hata iwe kwa kosa gani, huwezi kumtia pilipili machoni kwa kisingizio cha kumadabisha huko ni kum-abuse
 
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
383
Likes
23
Points
35
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2012
383 23 35
USIULAZIMISHE MWILI UAMBUKIZE SIKIO.
Kumchapa mtoto ni shambulio la kudhuru mwili na pengine asibadilike badala yake awe sugu,
hivyo kwa mimi huwa namuonya tu au namgombeza kwa kumwambia maneno makali yenye kumchoma mpaka anatamani ningemchapa tu shaishe kuliko kuendelea kuyasikia maneno yangu.

wewe usitake kutuletea sheria zako za ulaya hapa hatuziwezi,kuchapa mtoto anapokosea ni rukhsa hata shuleni tulikuwa tunachapwa na tulikuwa tunakoma haturudii makosa sasa wewe unasema ni shambulio shambulio gani hilo??
Mi naupinga sana huu ulimbukeni wetu sisi waafrika kuiga iga kitu bila kuchunguza na kuacha mila zetu,huko laya kumchapa mtoto ni kosa kisheria na wao tangu ujima walikuwa hawachapi watoto,lakini wa2 wote waliobakia huwachapa watoto wao kama njia ya kuwafundisha,si watoto wote huwa wanaonyeka kwa mdomo wengi wao hata hueme vipi anarudia ksa lile lile,sasa kwa nini usimchape,mi mwenyewe nilichapwa wakati nasoma madrassa na kama nisingechapwa nisingeiweza jinsi ilivyokuwa ngumu.shule nilichapwa pia mana nilikuwa mtundu sana na kupenda kucheza mno kuliko kitu kingine vichapo viliniweka sawa.
 
Nambukwa

Nambukwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2009
Messages
243
Likes
14
Points
35
Nambukwa

Nambukwa

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2009
243 14 35
Mimi muumini wa viboko!!!
Maneno yana mahala pake na aina yake ya makosa, viboko navyo vinahusika sana katika kuleta adabu na mwelekeo
Viboko si kila wakati, na kuna kosa hata mtoto mwenyewe anajua hili adhabu yake viboko.
Unampatia vya kumtosha
kila mtu hapa ana story jisnsi viboko vilivyomuokoa.
 
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
36,088
Likes
368
Points
180
Kongosho

Kongosho

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2011
36,088 368 180
Adhabu stahiki inaendana na mazingira

Kwa mtoto aliyekulia Masaki na kumiliki nymba 2 USA kama Natalia shosti wake King'asti
Ndio ataelewa adhabu ya kuambiwa 'Go to your room', mie wa Tandale ukiniambia "go to your room' unakuta nimechapa usingizi wangu kama kawaida.

Au unanikataza kuangalia TV kwa wiki? TV yenyewe napiga chabo kwa mjumbe wa mtaa.

Je, unipe adhabu ya kujaza pipa la maji?? Mbona hii ni wajibu wa mtoto kusaidia kazi za nyumbani atokapo shule? Na sitaki mtoto aone kazi za nyumbani ni adhabu, nataka aone ni wajibu wa binadamu kufanya kazi kwa kila stage ya maisha.

Hata mie ni muumini wa kuchapa kwa kiasi kulingana na kosa


Hata familia kuna utaratibu wa kimahakama, mtu hawezi iba kuku akahukumiwa kunyongwa, na tunajua mtoto mdogo anapelekwa gereza la watoto. Kadhalika nyumbani mtoto anapata kichapo kulingana na umri na kosa lenyewe hata kama hana wakili wa kukitegemea.

wewe usitake kutuletea sheria zako za ulaya hapa hatuziwezi,kuchapa mtoto anapokosea ni rukhsa hata shuleni tulikuwa tunachapwa na tulikuwa tunakoma haturudii makosa sasa wewe unasema ni shambulio shambulio gani hilo??
Mi naupinga sana huu ulimbukeni wetu sisi waafrika kuiga iga kitu bila kuchunguza na kuacha mila zetu,huko laya kumchapa mtoto ni kosa kisheria na wao tangu ujima walikuwa hawachapi watoto,lakini wa2 wote waliobakia huwachapa watoto wao kama njia ya kuwafundisha,si watoto wote huwa wanaonyeka kwa mdomo wengi wao hata hueme vipi anarudia ksa lile lile,sasa kwa nini usimchape,mi mwenyewe nilichapwa wakati nasoma madrassa na kama nisingechapwa nisingeiweza jinsi ilivyokuwa ngumu.shule nilichapwa pia mana nilikuwa mtundu sana na kupenda kucheza mno kuliko kitu kingine vichapo viliniweka sawa.
 
Last edited by a moderator:
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
80
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 80 0
Mmmhh,sina watoto ila nikikumbuka tajriba yangu, sijawahi kupewa adhabu yoyote ile nyumbani, sikupigwa wala kugombwa wala adhabu nyengine

Hapa kwangu nimetoka na maswali mawili

1. Mtoto hufanya kitu gani hadi akahitaji kupewa adhabu?
2. Na hizo adhabu mbali ya kupigwa bakora, nyengine ni adhabu gani?
 
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
383
Likes
23
Points
35
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2012
383 23 35
Mimi muumini wa viboko!!!
Maneno yana mahala pake na aina yake ya makosa, viboko navyo vinahusika sana katika kuleta adabu na mwelekeo
Viboko si kila wakati, na kuna kosa hata mtoto mwenyewe anajua hili adhabu yake viboko.
Unampatia vya kumtosha
kila mtu hapa ana story jisnsi viboko vilivyomuokoa.
Nakumbuka wakati npo mdogo enzi hizo nakaa tanga raskazoni nilikuwa nasoma primary bombo nilikuwa nakaa na mdingi tu basi alikuwa ananipenda na kunidekeza kinoma,basi mi shule nilikuwa sielewi kabisa hata kuandika wala kuhesabu sijui,darasa la pili hilo!!! mama alipokuja akaona vile akanichukua nikakaa kwake akaanza kunifundisha si viboko hivyo bwana ukigeuka cha mgongo mzee ikabidi nikomae ukisinzia mzee umefinywa duh!! wiki mbili tu najua kusoma na kuandika na kuhesabu,nasoma gazeti!!! sasa bila viboko unafikiri mi ningesoma kwanza kitendo cha kwenda shule tu ilikuwa mtihani mkubwa sana kwangu yani nilikuwa nataka kucheza tu muda wote!! primary nilikuwa kila siku nikiamshwa saa 12 asubh kwenda shule sikosi sabab ya kutotaka kwenda shule asi mama alikuwa anakuja kuniamsha na viboko vya ****** mwenyewe yule shule!!mbaka nimemaliza form 4,form 6 hapo nikwanajitambua mwenyewe baadae chuo kikuu huko mwenyewe sasa wewe unadhani bila viboko mi leo siningekuwa napiga deal za ujambazi???
 
Bei Mbaya

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
2,264
Likes
231
Points
160
Bei Mbaya

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2010
2,264 231 160
mtoto wa kiafrika bila au kwa bakora aweza kuwa nunda
 
Jidu

Jidu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Messages
1,179
Likes
322
Points
180
Jidu

Jidu

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2011
1,179 322 180
"NA MBORA WA MZAZI NI YULE ANAYENING'INIZA FIMBO YAKE NYUMBANI KWAKE KWA AJILI YA KUWARUDI WATOTO WAKE PINDI WANAPOKOSEA"HII NI TAFSIRI YA SIMULIZI TOKA KWA MTUME MOHAMAD(Swalla Allaahu 'alayhi wa Sallam).
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,404
Likes
38,581
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,404 38,581 280
Usimnyime mtoto kiboko.
Pia mkono ukupigao ndio ukufunzao.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,404
Likes
38,581
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,404 38,581 280
Mimi adhabu ninayo wapa ni kunifulia Soksi zangu.
ndio zile ulizotuadhibu nazo pale uwanja wa Taifa baada ya kuvua viatu uwanja mzima ukawa haukaliki kwa uvundo!!! kweli watoto wako watanyooka kwa style ya adhabu hii
 
isambe

isambe

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
2,063
Likes
909
Points
280
isambe

isambe

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
2,063 909 280
umeona eeh!na siku hiyo machine inazimwa,ngoma ni kupekecha kwa mkono na sabuni ya unga kidoogo,sasa hivi wamebadilika discipline kwa kwenda mbele,ilifikia wakati nikawaambia adhabu itabidi iongezwe, nikawaambia nitakuwa na enclude na soksi za mnyasa gardener!!
 
Superman

Superman

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2007
Messages
5,702
Likes
107
Points
160
Superman

Superman

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2007
5,702 107 160
Kama jibu ndio kwanini ulilazimika kuwachapa badala ya kuwa adhabu mbadala na kama huwachapi unawapatia nidhamu vipi?
Sibu sjawahi.

Nawapa adhabu mbadala. Mfano:

1. Hakuna kuangalia TV nenda kalale ujifunike shuka kabisa. hapo ni Mchana na Cartoon Network inaendelea. maumivu kwa dogo ni balaa ni bora kuchapwa. Hakika hatarudia kosa.

2. Adhabu nyingine niliyowahi kutoa ni kumtenga. Unampa kiti chake unamwambia kae kwenye kona sitting room ila haruhusiwi kusema neno lolote wala kuongea na zaidi ya kusikiliza. Sasa imagine hapo kama kuna stories za kuchekesha au kuna programme yoyote nzuri. Ni adhabu tosha.

3. Nyingine za kufikirika ni: safisha chumba chako; Fua nguo zako hakuna kwenda kucheza nk nk.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
80,852
Likes
46,329
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
80,852 46,329 280
Sijawahi kumchapa mtoto hata siku moja.
 

Forum statistics

Threads 1,237,036
Members 475,401
Posts 29,276,163