Umewahi kuchapa wanao ?

Kwanza nikifikilia tu Kitendo cha kumchapa mwili wangu unaogopa..
1.Pale napoona amekosea nitamwita muda huo na kumwambia kosa lake na kumwambia asirudie
Na atajua kabisa mama amechukia leo
2.Kama alivyosema Superman watoto wanavyopenda cartoon sitamruhusu kuangalia na atajua kabisa hapa leo hali si shwari .
Nk Nk
 
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 19:18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Wakolosai 3:21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
1 Timotheo 3:4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

Hayo mambo yenu ya kukanya watoto utafikiri unalea nao utaambulia vibaka na wavuta bangi, Mtoto ukimwazibu kwa kosa alilofanya shida iko wapi, Tatizo lenu mnaweka wazazi wanaotiisha watoto wao kwenye kundi moja na child abusers! Huwezi kumchoma moto mwanao hata iwe kwa kosa gani, huwezi kumtia pilipili machoni kwa kisingizio cha kumadabisha huko ni kum-abuse

Eti wana taka kuwaiga wazungu wakati wao wameshindwa wanapalilia ushoga tu sahivi
 
Mtoto akikosea na nikiudhika sana ninamchapa. Ila huwa nashangaa baba yao hawachapi hata siku moja lakini wanamtii yeye kuliko mie mchapaji! Mie naweza kukataza jambo kwa kusema na kurudia lakini baba yao akiwaangalia tu kwa jicho la kukataza unaona mara moja wameacha. Duh! Itabidi na mie niache kuchapa.
 
Mimi kuchapa kwangu ni njia sahihi japokuwa uwaga naangaliaga sababu za kuchapa lakini imesaidia sana kuwanyoosha watoto ukizingatia wakati tuliopo ni ngumu kumdiscipline mtoto akiwa anakuwa ana influence ya vitu vingi.
Nimechapwa nilipokuwa mtoto na kwa kiasi fulani ilisaidia kuweka mipaka na nidhamu.
 
Mtoto akikosea na nikiudhika sana ninamchapa. Ila huwa nashangaa baba yao hawachapi hata siku moja lakini wanamtii yeye kuliko mie mchapaji! Mie naweza kukataza jambo kwa kusema na kurudia lakini baba yao akiwaangalia tu kwa jicho la kukataza unaona mara moja wameacha. Duh! Itabidi na mie niache kuchapa.
Kawaida sana kwa mama na mtoto! They always see their mothers not that intimidating
 
kiboko ni muhimu angalieni wattoto wetu kwa sasa wanaongoza kwa ujinga huwezi ukalinganisha na kipindi chetu kibo kilikuwa kina tufanya tusome kwa bidii na kuwa nautii lakini siku hizi mtoto utamwambia nini hata mazazi huruhusiwi kumkanya mtoto wako eti unamnyima haki yake wana na wapi
 
watoto wangu nawachapa!
wanafunzi wangu nawachapa!
mimi mwenyewe nilichapwa ndo mana nimefika hapa!manake nilikuwa mtundu,sisikii,napenda kucheza na mazagazaga kibao!ila sasa.....
sichapi mtoto mpka afahamu kosa lake ni lipi?
alikiri kuwa ni kosa!
ajue kosa lile zaidi ya viboko lingeweza kumgharimu nini!
siwekeshi adhabu!amekosea sasa kama kosa ni la kupewa adhabu ya viboko naitoa immediately
AKIFANYA VIZURI PIA NAMPONGEZA!ili nikimuadhibu ajjue kuwa amefanya lisilo sahihi!
 
Kwanza nikifikilia tu Kitendo cha kumchapa mwili wangu unaogopa..
1.Pale napoona amekosea nitamwita muda huo na kumwambia kosa lake na kumwambia asirudie
Na atajua kabisa mama amechukia leo
2.Kama alivyosema Superman watoto wanavyopenda cartoon sitamruhusu kuangalia na atajua kabisa hapa leo hali si shwari .
Nk Nk
kwa kuitumia cartoon kama punishment then unaipa sifa ya kuwa ni kitu cha thamani!matokeo yake unaweza kujikuta anakua akiamini hivo!
unakumbuka wakati tunasoma boarding tulikuwa tunapewa adhabu ya kulima mashamba!matokeo yake mi ukinitajia tu shamba najionea adhabu!hiyo ndo theory ya punishment na reinforcement inavofanya kazi!
 
Malezi yanaweza kuwa bora kwa kumchapa mtoto au kutomchapa...

inategemea sana....
wapo waliochapwa ikawasaidia
na wapo waliochapwa ikawaa athiri...

so sio jibu moja tu simple ....

it works for some,it doesn't for some..
 
kila jambo lina wakati wake na mazingira yake! Kwani nilazima kila historia uliyopitia wewe na wanao ni lazima wapitie hiyohiyo! Badilikene na wakati acheni mambo ya kizee na kizamani kuchapa watoto viboko.Mjerumani mwenyewe alianzisha viboko kwa waafrika alikuwa hachapi wanae, Kwani wao wamepungua nini? zaidi ni maadili mabovu tuu ya waafrika
 
Malezi yanaweza kuwa bora kwa kumchapa mtoto au kutomchapa...

inategemea sana....
wapo waliochapwa ikawasaidia
na wapo waliochapwa ikawaa athiri...

so sio jibu moja tu simple ....

it works for some,it doesn't for some..

Tatizo utajuaje adhabu ya kuchapa au kutokuchapa now, kama itamsaidia mwanao in the future?
 
Mimi nilivyokuwa mdogo nilikuwa mdokozi wa hela na kuku wa watu mtaani. Yaani kuku akipita tu nimepiga tukio! Ukiacha hela tu,kwenye maandazi na vim.bama. Maza akaninivalia njuga nilianza kulambwa stick mpaka nilinyooka na shule nikawa muhudhuriaji mzuri. Namshukuru kwa kuninyoosha ila huwa namlaumu kwa kuniachia makovu mengi miguuni. Mtoto anatakiwa achapwa kwa matukio ya kujirudia rudia lakini isiwe ni schedule.
 
du nilivoona kuchapa watoto kwenye jukwaa la mapenzi nilienda mbali sana, sasa nimeshusha pumzi!
 
Mtoto akikosea na nikiudhika sana ninamchapa. Ila huwa nashangaa baba yao hawachapi hata siku moja lakini wanamtii yeye kuliko mie mchapaji! Mie naweza kukataza jambo kwa kusema na kurudia lakini baba yao akiwaangalia tu kwa jicho la kukataza unaona mara moja wameacha. Duh! Itabidi na mie niache kuchapa.

wanajua viboko vya mama haviumi. Wakimuangalia dingi namsuli alonao wanapiga mahesabu siku akishika fimbo mifupa yote itavunjika. Aafu familia nyingi nimekuta hivyo, mama akiwa mchapaji dingi hachapi na dingi akiwa mwepesi wa kushika fimbo mama hachapi.
 
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 19:18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Wakolosai 3:21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
1 Timotheo 3:4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

Hayo mambo yenu ya kukanya watoto utafikiri unalea nao utaambulia vibaka na wavuta bangi, Mtoto ukimwazibu kwa kosa alilofanya shida iko wapi, Tatizo lenu mnaweka wazazi wanaotiisha watoto wao kwenye kundi moja na child abusers! Huwezi kumchoma moto mwanao hata iwe kwa kosa gani, huwezi kumtia pilipili machoni kwa kisingizio cha kumadabisha huko ni kum-abuse
Asante..... Umemaliza kila kitu.
 
Mimi nilivyokuwa mdogo nilikuwa mdokozi wa hela na kuku wa watu mtaani. Yaani kuku akipita tu nimepiga tukio! Ukiacha hela tu,kwenye maandazi na vim.bama. Maza akaninivalia njuga nilianza kulambwa stick mpaka nilinyooka na shule nikawa muhudhuriaji mzuri. Namshukuru kwa kuninyoosha ila huwa namlaumu kwa kuniachia makovu mengi miguuni. Mtoto anatakiwa achapwa kwa matukio ya kujirudia rudia lakini isiwe ni schedule.

Duh! Na wewe ulizidi! Sasa ukishadaka hao kuku wa watu ulikuwa unaenda kuwalia wapi?
 
mimi kwa kweli wanangu nachapa...... tena pale kwangu kuna kamsemo "mama anachapa"!
sishangai kusoma wababa wengi hawachapi watoto.... mimi sikuwahi kuchapwa na babangu mpaka nimetoka home.....
mdogo wangu ambaye alikuwa pasua kichwa aliwahi chapwa na baba mara moja tu
pale home nakumbuka siku moja nilikasirika sana kwa alichofanya mtoto..... nikaenda kuleta fimbo nikamkabidhi baba achape mtoto na hakuweza........kwa hiyo naelewa.
uzuri huwa sichapi mtoto anapokosea kwa mara ya kwanza. huwa namkalisha na kumwambia hiki sipendi. siku akijisahau akarudia na nimemwona, huwa anaenda kujitafutia fimbo kabisaaaaa, maana anajua haponi.
kuna rafiki hapo juu kaweka mistari ya Biblia Takatifu kuhusu kuchapa, na mimi nakubaliana na hiyo misitari, ni part ya mafunzo
 
kwa kuitumia cartoon kama punishment then unaipa sifa ya kuwa ni kitu cha thamani!matokeo yake unaweza kujikuta anakua akiamini hivo!
unakumbuka wakati tunasoma boarding tulikuwa tunapewa adhabu ya kulima mashamba!matokeo yake mi ukinitajia tu shamba najionea adhabu!hiyo ndo theory ya punishment na reinforcement inavofanya kazi!
wakati nasoma primary rafiki zangu walikuwa watoto wa matajiri (kule kwetu enzi hizo ilikuwa mtu akiwa na kaduka nyumbani kwake ni tajiri, lol!). wale watoto walikuwa mabinti tu wawili. walikuwa wakikosa wanapewa adhabu ya kuuza duka....... hiyo siku muuza duka ataambiwa asije anauza binti....... sasa huko ni bonus za pipi na biscuti, hii nayo ni adhabu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom