Umesoma vitabu vingapi mwaka 2017?

Umesoma vitabu vingapi mwaka 2017?

Six Man

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
253
Reaction score
893
Nimeona orodha mbalimbali ya watu wakiorodhesha idadi ya vitabu walivyosoma mwaka jana. Katika wote walioandika orodha zao mwandishi Fadhy Mtanga anaongoza kwa kusoma vitabu 107 kwa mwaka jana pekee.

Nimeona orodha ya mbunge wa Kigoma Mh Zitto Kabwe, orodha ya rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na watu wengine kadhaa mashuhuri.

Kusoma vitabu ni jambo zuri na kujivunia kwakuwa vitabu ni chakula cha ubongo. Msomaji wa vitabu anaipumzisha akili yake kwa muda na kusoma akili za wenzake. Vitabu pia ni burudani murua kwa msomaji. Vitabu vinakukutanisha na watu ambao hukuwaza hata simu moja kukutana nao. Unataka kukutana na Bill Gate? Soma vitabu vyake. Unataka kukutana na Hussein Tuwa? Soma vitabu vyake. Unataka kukutana na Halfani Sudy? Soma vitabu vyake.

Tuwe jamii ya kupenda kusoma vitabu ili kujua mambo mbalimbali ulimwenguni.

Nikuulize wewe unayesoma uzi huu, umesoma vitabu vingapi mwaka 2017, tutajie kama unaweza na sio mbaya ukashauri wenzio vitabu vizuri vya kusom katika mwaka huu wa 2018.

Naitwa Six Man.
 
Nina vitabu vingi kwenye simu, ila kuvisoma sasa ndio taaaabu kwelikweli... Naweza nikaanza kusoma nikifika kurasa ya 100+ basi ndio sina hamu tena
 
Baadhi ya nilivyonavyo
 

Attachments

Back
Top Bottom