Planet of Slums labda kinaweza kuwa ni kitabu kizuri.
Lakini hapa wanajamvi sijaona kitabu kinachotufundisha mtu jinsi ya Kumyanyua "Mwafrika".
Hatuoni vitabu vya "Current Affairs au Science and Technology au matters related to health, our well being na hata zaidi mambo yanayohusu KILIMO na pembejeo"
Vitabu vingi sana katika soko la vitabu ni propaganda, personal opinion/perspective/sensational.
Jinsi vitabu vinavyoandikwa, historia ya mwandishi, maisha yake binafsi ni muhimu sana kumjua. Kuna vitu tunavisoma ambavyo havitusaidi kwenye maisha yetu. Waandishi wengi ni wahuni na wavuta unga/bangi/mvinyo. Tumekutana nao.
Ukiingia Maktaba au dula la vitabu nchi za dunia ya Kwanza kama Marekani, vitabu kama vile kitabu cha Malcolm X au Stive Biko au Thabo Mbeki, lazima kiagizwe kutokana na umaarufu wake. Kuna Muamsho mkubwa sana duniani kwa kizazi cha sasa cha watu weusi, labda Tanzania hatulioni lakini WaAfrika wamekataa kulala na kulalishwa/mfumo onevu.
"Black Lives Matter".
Kuna Wazungu na utamaduni wa Ushoga, wanajaribu sana kuisukuma ajenda hii katika mavazi, maadili na hata sheria zinazotawala duniani kote.
Kuna vita biashara, dola chini ya kivuli cha damu, ajenda kugombanisha vikundi/mataifa na kuuza silaha, kubadilisha Utawala na kufaidika na Rasilimali. Ndio maana tunaona mtu anaandikiwa kitabu kuhusu Uislam na mzungu na kukisifia, tunacheka, maana hujuma na dhulma walizofanyiwa Waafrika na Afrika, ndio Waislam wanafanyiwa leo katika nchi zao. Muamar Gadafi hakushamuliwa na M23 au Malaria. Kila kikundi cha Ugaidi kina asili yake kwa Bwana Mkubwa.
Nani anasoma mfumo wa biashara ya Utumwa walivyoanza kukamatwa na kupekwa kwa nguvu na mpaka leo wanajipeleka wenyewe kwa nguvu za hiyari yao na wengi wamepoteza maisha yao kwenye bahari ya Mediterranean?
Kuna ajenda ya kuwafanya Waafrika kuwa"mazuzu" na kuwatawala kutumia dini zilizoanzishwa 1920 huko Marekani kwa rasmi kwa ajili hiyo.
Ukuu na Ubora wa Wazungu (White Supremacy) unapamba moto, kura zilizompa Bwana Tirampu Ushindi na sasa Ulaya inaweza kuelekea huko.
Nani anayesoma ni maana ya Mfumo wa Kizayuni, nia yake ya kuitawala Israel na Afrika?
Kuna kusoma Ujasusi na Uhalifu kwenye hii Mitandao na pia namna ya kufaidika na mitandao hii kibiashara.
Msisahau WikiLeaks.
Nani anasoma jinsi India na China walivyojikamua na kutoka kwenye Ujinga na Umasikini bila ya kuivamia Congo na kuweka waasi huko?
Nani anasoma adhari na madhara za kutumia jela kuzima Upinzani huko Bangladeshi?
Pan Africanism- Utashangaa sasa Fikra za Mwalimu Nyerere zimepamba moto sehemu nyingi hapa Afrika haswa kwenye taasisi nyingi. Vitabu vya Mwalimu Nyerere vimekuwa adimu sana. Kila Kiongozi wa juu anavisoma vitabu vyake.
Wangapi tunasoma maisha ya Nelson Mandela na kuwa na shauku ya kutengeneza amani duniani?
We have to connect to the real world, what makes the headlines, kuanzia bei ya petrol na mpaka bei ya chakula, thamani na faida ya ardhi yetu.
bila hivyo tutajikuta tumetawaliwa bila bendera na kung'ang'ania vitabu vimeandikwa kwa ajili ya biashara tuu na vingine kwa ajili ya kutupambaza.