Umesoma vitabu gani mwaka 2016?

Umesoma vitabu gani mwaka 2016?

Kwanza safi kwa kujiongezea ufahamu wa mambo . Vp hivyo vitabu vyako umenunua wap
bongo madukani ni ngumu sana kupata. tunaishia kuvipirate mitandaoni japo vingine ni free mitandaoni
 
Nimesoma vitabu vifuatavyo
1. The da vinc code
2. The alchemist
3. The strong man putin
4. Animal farm
5. The history of christianity
6. Perfumed Garden

Vyote ninavyo kwa pdf kwa anayehitaji.
 
Nimesoma Kitabu cha MWANZO (chote), Kitabu cha KUTOKA (chote) ninaendelea nina mpango wa kuimaliza Biblia yote.
 
Asante kwa vitabu naomba unisadie nawezaje kuvipata mim napenda kusoma sana vitabu tatizo ni jinsi gan ya kuvipata hivyo vitabu. Nisadie maduka mazur ninunue
1:Vitabu vingi vinapatikana katika maduka ya vitabu, Kwa dsm unaweza kwenda posta kuna bookshops pale mitaa sijaikalili utapata baadhi.
2:Vitabu vingine huwa vinamwagwa tu mabarabarani mchanganyiko maeneo ya ubungo na Posta pale karibu na Tume ya maadili kama sikosei unaweza kuwaona wale jamaa ukiwatajia jina wanaweza kukutafutia.
3:Vitabu vingine hasa vya kikristo unaweza kuvipata pale Mikocheni karibu na kwa Warioba kuna duka la vitabu nimelisahau jina lakini kuna kibao barabarani.
4: Vitabu vingine vinapatikana Ukishuka Victoria kama unaelekea Hospitali ya Kairuki mkono wa kulia. Kuna taasisi pale ila ninakumbuka kwa wanafunzi wa UDSM ukiwa na kadi/kitambulisho au Kuna Dr mmoja anaitwa Mrindoko anaweza kukupa ramani au ukaenda kujieleza mwenyewe. Pale huwa linakuja kontena la vitabu mchanganyiko unaweza kujipatia vitabu of your interest niliwahi kwenda zamani sijui kama bado inaendelea wanauza bei rahisi maana wanapewa kama misaada.

5:Vitabu vingine unaweza kuvisoma Online kupitia Google books

6:Vingi mimi huwa navigoogle .pdf nikisha kijua jina na mwandishi. Nitakisaka hadi napata copy na kukiweka kwenye notepad maanalum kwa kazi hiyo.
7:Vingine unavitafuta Amazon unakiagiza kwa kufuata utaratibu unapata. Au kama unarafikki nje ya nchi au SA unamwomba anapokuja akuletee copy ya kitabu unachokitafuta.
8:Unaweza pia kununua softcopy online au kujisajiri katika online libraries huko duniani ukawa na uwezo wa kupata access ya kitabu chochote.

9:VIngine unavipatata kwa wadau kama humu. Unaweza kuandika mwenye softcopy ya kitabu flani, na kati ta watu zaidi ya lakin nne huwezi kukosa. Njia nyingine ni kujiunga kwenye Reading clubs hata hapa bongo zipo huko utakutana na kila aina ya watu wenye vitabu vya kila aina.
10:Vitabu vingine unavipata kwenye mikutano ya kidini,Kijamii, siasa,au workshops, Mfano mimi The joy of encouregement nilienda kwenye mkutano flani wa kidini/protestants siku moja kwa lengo la kutafuta kitabu cha kununua na nikakinunua na kuondoka zangu.

Kuna options nyingi ya kupata vitabu hata bure ikiwezekana. Kuna vingine niliwahi kuwaandikia Email shirika moja huko us zamani za kuomba vitabu nikatumiwa box zima posta baada ya muda kidogo.

Hayo ndio maoni yangu wengine wanaweza kusaidia zaidi mkuu
 
Jamani nina shida na kitabu kizuri cha management
Na leadership
Naomba ushauri nisome kitabu gani
 
1:Vitabu vingi vinapatikana katika
4: Vitabu vingine vinapatikana Ukishuka Victoria kama unaelekea Hospitali ya Kairuki mkono wa kulia. Kuna taasisi pale ila ninakumbuka kwa wanafunzi wa UDSM ukiwa na kadi/kitambulisho au Kuna Dr mmoja anaitwa Mrindoko anaweza kukupa ramani au ukaenda kujieleza mwenyewe. Pale huwa linakuja kontena la vitabu mchanganyiko unaweza kujipatia vitabu of your interest niliwahi kwenda zamani sijui kama bado inaendelea wanauza bei rahisi maana wanapewa kama misaada.
wale jamaa wa Kairuki sijui walianza uhuni? nilienda wakasema wanauza kwa taasisi na si individuals. nafikiri pia walihamia kinondoni inayotazamana na Shule ya Mbuyuni. ni muda mrefu umepita toka niwacheki.
ubungo kwenye vitabu vya mtumba vya chini nilikuwa nanunua sana. vikubwa, vidogo vyote ilikuwa buku.
 
Safi sana mimi Mara ya mwisho kwenda pale ilikuwa 2011. Nilitumia jina la huyu Dr alikuwa ni mwanachama pale na kuna workshop flani aliiendesha akapazungumzia nikajiongeza.
Pale ubungo pako vzr unaweza kuibuka na kitabu ambacho posta ni 30000 au 50000 pale buku au 10000, ukiwa na link na wale jamaa na wengine wako posta huwa wanapanga chini wanaweza kukutafutia kitabu cha interest yako.
Nimekukubali mkuu kama na pale ubungo huwa unapita kuperuzi
 
Tusome vitabu vyote kadri iwezekanavyo lakini BIBLIA na QURAN viwe jirani mara kwa mara
Mimi 2016 nimesoma kile kinachoitwa MTAISOMA NAMBA....Ccm ni ile ile
 
Y
IMG-20170121-WA0008.jpg
IMG-20170121-WA0008.jpg
IMG-20170121-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom