Umesoma shule ya bweni wewe?

Hiyo kitu unakuta raia anakula kidogo anabakisha ili aje amalizie baada ya prepo, akitoka watu wanaupindua pindua mzinga akirudi nguo zote na vitabu zimejaa maarage.
 
Da mwana umenikumbusha mbali sana, tanga scl enzi hizo kuna jamaa 2lwakuta wakiwa f4 akna chadog walikuwa wababe balaa ck moja ilipikwa nyama kuna jamaa yetu alikuw anaitwa masesa lufunga alikimbia na bakuli la nyama huku akikoswakoswa mawe akaenda kuficha kwa mwl sheikh said da hadi raha, nimewakumbuka sana akna emmanuel damas, mayala mwendesha, mbura chiragwile, john holela, arab, mbwana mohamed,shukuru na wengine wote, mambo ya kimuki yalikuwa noma!
 
Hiyo kitu haiwezi kuwa Tosamaganga mkuu, maana ugali mweupe halafu kama umepakuliwa kistaarabu fulani hivi. Enzi hizo tunapiga kitabu hapo kwanza bondo la dona jeusiii linapikwa saa moja au mbili kabla linapoa mpka linaota koti zito. Bahati yako mbaya Table Leader akiamka vibaya anakuwekea wewe koti lote na nyama ya ndani kidogo.

Kumbusha mimi mbaaaliiii.... Hapo nyuma ya tank la maji naiona DH kwa mbaaaali, bila kusahau wale mabeki tatu wa walimu wauza mboga mboga.
 
sie maharage ilikua siku ya jumatano tena ukijichelewesha unakosa, nilipata shida kupata maharage kwa 'msimu'
 

Hizi product za miaka ipi?,mie nilikuwa pale 1987 to 1990 bweni la Twiga wing ya chini kulia
 
Miaka hiyo ya nyuma vijana wa - Tosamaganga, wakiwa wame-assemble kwa matangazo ya asubuhi kabla ya kuingia madarasani. Kwa wale waliopita kwa A-level na O-level tuko pamoja!!!
 
Ngwale umenikumbusha mbali na hiyo picha ya Tosamaganga, sababu hapo kwa nyuma ni shule niliyosoma ya msingi ya Lyalamo. Ni majirani kabisa hapo
 
Du umenikumbusha Magamba sekondari enzi hizo Lushoto Tanga,sasa hivi imegeuzwa kuwa chuo kikuu cha SECOM
 
Mpwapwa Sekondari bondo mjengoni....mliosoma Mpwa Sek mnamkumbuka mpishi mzee Tobo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…