Umesoma shule ya bweni wewe?

dah! nakumbuka
wali-beche
ugali-bondo
uji-nyuka
ukoko wa wali-busati
andazi-kitomari(jina la mwalimu)
aisee Ifunda tech ntakukumbuka daima!
 

kolila sekondari tulikuwa tunaliita bonge
 
tanga tech. kwa mzee teti wali tuliuita cheche.....igali jiwe....
 
Duuu.....nyali(wali)....bondo(ugali)pola(uji) shybush chini ya mkuu Mbanga..siku ya mechi unatorokea mgodini ku refresh...daaaa.....mkuu ume rewind memory yangu mbali saaaana aisee

Mbanga baadae alikuja Tosamaganga baada ya Shybush.
 
nimekumbuka mbali sana dah skonga nouma
 
Hapo ukiwa form one lazima uwe dreva wa kiranja kumbebea msosi ili uweze kushiba

Pasesco walikuwa wanaitwa Special wa HP au Special wa Head Girl au Special wa Head Boy huyo kazi yake anakuwa anamtake care HP kwa mambo kibao ya kubebea vyombo vya Msosi na kumpelekea office yake kumuoshea Vyombo mtoni wakati mwingine kufua uniform au Kutandika Kitanda n.k msosi wa HP hujazwa Sana so wale maspcecial ndio wakati wao wa kujenga miili kwa Sembe na maharage wale wauza maparachichi,Ndizi,Tomasi,Peas na miwa(Miguva) lazima wamhonge HP baadhi ya bidhaa zao basi Maisha yanakuwa Matamu sana... HP anateua Special wake wa Form One mwenye mwili mdogo...
 
Kibiti boys high school lilikua linaitwa. Dongo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

mimi nilipita hapo wakati kibiti ni mchanganyiko ,shida ya maji ,bondo lilikuwa haliivi ,tulikuwa tunakwenda kuiba mihogo ya wandengeleko
 
Nimemiss sana hivyo vitu huwa najaribu kupika kama hivyo nyumban lakin haiwi tamu kama ile ya enzi zile...
 
Makumira High School tulikuwa tunaikwepa hii hitu Tunaenda Canteen kwa Mama Kadogoo au kwa Rich au kwa Solo Sahani ya Wali Sh Mia tu...

maharage ya pale salute!juu lazima ukutane na wadudu weupe na weusi...
 
hahahaha.....mnanikumbusha mbaalii
 
mbona ugali wenu ulikuwa mzuri sana? Pale msalato ugali wa sembe utadhani dona alafu una wadudu a.k.a fukuzi. Mchana makande jioni ugali. Alhamis na jumapili mchana ugali jioni wali, tulikuwa tunaita siku ya chakula. Wali unabakiza unakula siku ya pili tulikuwa tunaita kijogoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…