Musoma Tech/Alliance enzi hizo! Dishi la maharage na ugali yakitolewa mwenye kubeba la harage anakimbilia South mwenye la ugali anakimbilia North sasa either upate ugali au harage. Harage zenyewe sasa! Ktk harage 1 kuna wadudu kama 6 hivi! Ugali unga kama umeoza hivi,
siku ya wali masomo mwisho saa sita, mapema watu wanatoka kwenda kuuvutia pumzi. Kichekesho ni pale utakapo pata huo wali, kwanza ni kama ngumi ya mtoto, ration master, kiranja wa bwalo na wapishi wanaiba zaidi ya nusu ya ration then wanaongeza mchanga. Nusu wali nusu mchanga. Siku ya wali inageuka kua kwaresma.
Ukipata kijitamvua cha samaki unaficha plate 2.
'Maisha ya boarding noma, utafikiri kambi ya mafunzo' Jmo