Umeshawahi kumuheshimu mlinzi wa eneo lako la kazi?

kiben10

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
616
789
Mwanamke mmoja aliyekuwa anaitwa Nancy alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha kusambaza na kusaga nyama.

Siku moja, baada ya kumaliza ratiba yake ya kazi, aliingia kwenye chumba cha baridi (friji) cha nyama ili kukagua kitu, lakini kwa bahati mbaya, mlango ulijifunga na akakwama ndani bila msaada.

Ingawa aliita kwa nguvu na kupiga mlango kwa nguvu zake zote, kilio chake kilisikika bila kusikilizwa kwani hakuna aliyeweza kumsikia.

Wafanyakazi wengi walikuwa tayari wameondoka, na nje ya chumba cha baridi, ilikuwa haiwezekani kusikia wala kuona kilichokuwa kinaendelea ndani.

Baada ya saa tano kupita, akiwa karibu kufa na amekata tamaa, hatimaye mlinzi wa kiwanda anafika na kufungua mlango.

Nanvy alinusurika kwa miujiza siku hiyo.

Alimuuliza mlinzi ilikuwaje akaja kufungua mlango, jambo ambalo halikuwa kawaida yake kufanya maama sio sehemu yake ya kazi.

Mlizi alieleza: "Nimefanya kazi kwenye kiwanda hiki kwa miaka 35, wafanyakazi wengi wanakuja na kuondoka kila siku, lakini wewe ni mmoja wa wachache wanaonigia na kunisalimia "Habari" asubuhi na kusema "Kwaheri" usiku unapoondoka baada ya kazi. Wengi ujifanya kama hawanioni.

Leo, ulipoingia kazi kama kawaida yako ulinisalimia "Habari", lakini jioni baada ya saa za kazi, niligundua kwa kushangazwa kwamba sikusikia "Kwaheri tutaonana kesho" kutoka kwako. Hivyo, niliamua kukutafuta kila mahali.

Ili nipate salamu yangu "Habari" na "Kwaheri", kwa sababu zinanikumbusha kuwa mimi ni mtu.

Kwa kutokusikia kwako kuaga leo, nilijua kuna kitu kilikuwa kimeenda hovyo. Ndio maana nilikuwa nikikutafuta kila mahali."

Kuwa mnyenyekevu, penda na heshimu wale wanaokuzunguka kamwe huwezi kujua kesho itakuletea nini.

Mwisho
 
Walinzi wameungana kutunga stori ili heshima ipande.

Not today nyinyi Suma JKT. Mnazuia mtu asiende kumuona ndugu yake kwenye death bed
 
Nikisema mengi itakuwa kujisifia, ila na mimi ndio hivyo kwa jinsi nilivyo nao kila siku lazima waje kunisalimia wasiponiona nje, naheshimu na kuthamini mchango wa kila aliye karibu yangu.
 
Hawa hawa wa kitayosce security ? Ukiwasalamia sana wanaanza mazoea ya kukupiga vizinga, hapo bado haujawatuma chakula wakadonoa mnofu wa nyama .

Kiukweli nitawasalamia ila sio kila siku wana mazoea mabaya sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom