Umeshawahi kunusurika kifo? Tuelezane ilivyokuwa, kama njia ya kumshukuru Mungu

Sahihi kabisa
 
Nishakupata we ndo ulimkaba mdogo wg akiwa dereva tax afrikana Dogo kwa ujasili akalipeleka kwenye ngema mwenzio alipigwa kibiriti palepale we ukakimbia ni mitaa ya abarikiwe Njia ya kwenda jogoo ,wewe nazani wizi umeacha Sasa hivi
 
Mkuu hata mimi imewahi kunitokea wenzang wakanikimbia..... Dah lkn Mungu ni mkubwa nilifanikiwa kujiokoa
 
Wew umetisha mkuu
 
mwaka 2000 sita sahau nilipewa panga nikanoe kwajili ya kukatia mti, wakati nishalinoa narudi home nikawa nalichezea kwa kulitupa chini linaganda kwa kusimama kwenye ardhi,njia nzima ndio ukawa mchezo, ile nakaribia home si nikalitupa tena chini ,,,,,daaa sitasahau panga lile ligonga jiwe likanirudia shingoni, bahaati nzuri likanichapa na upapa kwenye koromeo, nilipata wenge nusu kukata moto....Wiki nzima chakula kikawa hakipiti mwendo wa uji tu' Mungu mkubwa alikunipiga kwenye makali
 
Duuh! Pole sana kweli hapo ulinusurika.
 
bado unanunua?
 
vipi watoto wazuri huwa unawapa lift?
 
Tukio la kwanza, gari ilikuwa ya wizi?
 
Ubabe, dhulma na unyanyasaji ni hulka ya wanajeshi wetu!
 
Mara ya kwanza tulikuwa watatu tukiwa chini ya miaka 7 tulinusurika kufa maji, tulimpoteza mwenzetu wa miaka minne. Ile picha jinsi alivyokuwa anaomba msaada tumsaidie haijafutika kichwani kabisa japo nimevuka 30 lakini kumbukumbu ni kama tukio la juzi tu.
Mara ya pili radi ilipiga kama mita 15 toka nilipo, ile shoti si ya mchezo, sitaisahau.
 
Kwa hiyo hilo papa ungelimlipa buku mbili
 
Kwanini hamkumsaidia mwenzenu jamani 😱😱
 
Ulikimbia na kujificha hadi lini?
 
Dah! Nimekujibu kwa urefu Bushmamy but comment haijatokea, naona uvivu kurudia, kwa ufupi narudia.
Tukiwa chini ya miaka 7, mimi na watoto wa dada tulishauriana tukaoge mtoni wakati wazazi wetu wakiwa shambani.
Kwa bahati mbaya kina cha maji kiliongezeka kutokana na mvua. Tulipofika mtoni, ile sehemu ambayo huwa tunaingilia tukaona maji ni mengi zaidi halafu yana kasi.
Tukamwambia dogo ambaye alikuwa na miaka minne hivi abakie pale pale, kisha sisi tuzunguke upande wa pili kupitia daraja.
Sasa wakati tumezunguka upande wa pili, ile furaha ya kumwona dada yake na mjomba wake (mimi) upande wa pili, ikamfanya aingie kwenye maji ili atufate.
Sehemu aliyoingia ilikuwa na kina kirefu kwa siku ile kama nilivyosema kutokana na mvua.
Tulishuhudia akiomba tumsaidie huku akienda, alipojaribu kusimama maji yalimpiga ngwala hadi akapotea. Tulitamani tusogee but ilikuwa ni hatari zaidi kwetu. Tukachukua tu nguo zake tukaenda nyumbani kutoa taarifa.
Kumbukumbu huwa hazinipotei kabisa kwa sababu alikuwa ndugu na rafiki.
 
Nimecheka hadi nikashikwa na kizunguzungu cha ghafla!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…