Umeshawahi kunusurika kifo? Tuelezane ilivyokuwa, kama njia ya kumshukuru Mungu

Tangia mdogo nnaelement za ufundi ufundi Sana
Sasa siku moja mpangaji amehama akawa ameweka Ile bed switch (kaswich kadogo kakuning'inia unapolala)
Alipoondoka akasepa zake...akaziacha
Ile mnyabi kuingia nkasema yeeesi nmepata waya,
Nkapanda juu ya sturi nkakate na meno dah..............................kuzitia mdomoni nizikate dah acha tu

Ndio maana Hadi leo akiri yangu kama haijastable hivi
Mungu mwema mazee
mimi nilikuwa nachubua nyaya kubwa za umeme na wembe.Mungu Ni Mwema Sana Tena Sana
 
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu, nilinusurika KUFA maji mwaka '88 Bagamoyo Enzi hizo ile Beach ikiitwa BADECO duh nilizindukia hospital baada ya kushindwa kuogelea nikiwa nimelewa konyagi...... Na mwaka huu mwezi wa pili nimepata ajali mbaya ya gari ila Mungu ni mwema nilitoka salamaView attachment 1526349
Duh, Ashukuriwe Mungu
 
Tangia mdogo nnaelement za ufundi ufundi Sana
Sasa siku moja mpangaji amehama akawa ameweka Ile bed switch (kaswich kadogo kakuning'inia unapolala)
Alipoondoka akasepa zake...akaziacha
Ile mnyabi kuingia nkasema yeeesi nmepata waya,
Nkapanda juu ya sturi nkakate na meno dah..............................kuzitia mdomoni nizikate dah acha tu

Ndio maana Hadi leo akiri yangu kama haijastable hivi
Mungu mwema mazee
 
Niliwahi kupanda bus nikiwa nimepewa lift na kondakta ambae ni rafki yangu baada ya muda alikuja kunihamisha ile siti niliyokaa, alaf akakakaa dada mmoja ilikua ni ile siti ya staff pale mbele karibu na mlango,,, haikupita dakika 15 bus ikapinduka miongoni mwa abiria walio fariki alikua Ni yule dada niliyempisha sit akakaa,, Kuna zile chuma za pembezon mwa barabara ndo iliingia ndani ya gar ikamchoma akafa palepale,,,,
aisee
 
Ilikuwa mwaka 1994 nasafiri toka Moro kwenda Dar, nimekata ticket basi la Hood nikaingia nikakaa na siti ilikuwa upande wa kulia maeneo ya katikati, muda kidogo anaingia dada fulani akiwa na ticket ya siti ileile niliyokaa. Zogo kidogo konda akaja na dada ndiye alikuwa wa kwanza kuingia kwenye gari alitoka kutafuta mahitaji kurudi ndo ananikuta mimi.Konda akaona ni makosa yao so akaniamuru nipande gari inayofuata, nilichukia kidogo maana ilinigharimu muda kusubiri hii ya pili kujaa so ile gari ikatangulia.Ile tunaanza safari tunapokea taarifa ile gari imepata ajali wamegongana na Greda upande mmoja wa basi umefutwa wote,tulipolifikia nikaona kabisa upande uliopitiwa na greda ni uleule niliokuwa nimekaa mimi kabla ya kushushwa.
Alikufa jirani yangu upanga
 
Haya mambo ya kuwapa lift watu Ni bora uwe kauzu tu.ishu ya gari uliponaje?
kaka yangu mie walimbebea laptop yake..kiukweli wengi wetu unakuwaga ni uswahili tu kuna wakati usafiri unakuwa wa shida sana yaani lakini mtu unapita kituoni umeweka mziki wako mkubwa tu lakini ndani ya gari niko mwenyewe ...unajua ukimpa mtu lifti mmmhhh utaishia njiani..wengne unampa lifti anataka yeye awe muongeaji kuliko mwenye gari
 
niliendaga kuogelea pale south beach kigamboni aisee..sasa nilienda na washkaji zangu ambao nilikuwa nasoma nao IFM walikuwa wa4 sasa katika kuogelea kuna rafiki yangu ambaye tulienda wote kati ya wale wa4 anaitwa islam bwana akaniona navoogelea kwenye maji lakini kuna wakati mie sikumwona kama ananiona nikawa nmeingia majini sasa bwana mmhh nikajikuta nimeingia upande ambao chini sifiki na juu sichomozi bwana ww..niliomba Mungu huku nikitupatupa mikono yangu juu mtu yyte anione aniokoe ndo islam akaniona na kunishika lakini baada ya hapo..islam akasema nilikuona ulivokuwa unaingia ndani ya maji nikawa muoga na kukuangalia..namshukuru sana mwanangu yule maana lasivyo ningekuwa nmeshatangulia

tukio lingne wanaokufahamu njia panda wazo pale mataa bwana kuna siku naenda skuli mida ya mchana hivi...kwa sie wakazi wa huku tegeta pale njia panda wazo kunatokea ajali mara chache sana lakini ikitokea lazima watu waondoke na ajali hiyo..sasa palikuwa ndio stendi ya mabasi miaka hiyo kama 2011 hivi bwana ww nikadandia basi langu pale nikatoka sasa nmefika tankbovu ndo nasikia napigiwa simu na bmkubwa bwana ww ukowapi nikamwambia niko tankbovu akanambia kuna ajali hapo imetokea njia panda wazo watu wamefariki wengne majeruhi..niliponea hapo tu

haya mambo ni tunaepukana na kifo kwa kuwahi au kuchelewa njee ya muda halisi lakini siku ikifika ya kwangu nitaenda eneo la tukio muda sahihi na wakati sahihi ...tujiweke mbele zake muda wote..tusali muda wote pia
 
Fanya service nzuri ya gari yako, Mkuu.
1.mie nlipinduka na gari chali tyres juu nilichubuka mkono tu,
2.ya pili gari niliteremka nayo toka mlimani tyre ya mbele ikachomoka ikaenda piga ngema tukatoka salama.
3.Siku nyingine tyroid hand ikachomoka gari ikanipeleka porini tukatoka salama.
4.Naenda kihansi huko tena gari ikochomoka tyre ya mbele nikaingia porini nikatoka salama
5.Nyingie nimesafiri usk usingizi ukanishika wkt jamaa zangu niliwaambia nyie msilale mniangalie nisipitiwe na usingizi bwana wote tukalala nilisikia ngu..nimegonga karavart tukaingia poeini tulitoka salama.
6.Nilitoka mikumi rough road ya kilombero aisee gari naona inaenda porini tyre tena imechilomoka break karavart.

Basi namshukuru Mungu hata kwisha kwa ile kazi maana sio ajali zile.
 
Back
Top Bottom