Umeshawahi kunusurika kifo? Tuelezane ilivyokuwa, kama njia ya kumshukuru Mungu

kaka yangu mie walimbebea laptop yake..kiukweli wengi wetu unakuwaga ni uswahili tu kuna wakati usafiri unakuwa wa shida sana yaani lakini mtu unapita kituoni umeweka mziki wako mkubwa tu lakini ndani ya gari niko mwenyewe ...unajua ukimpa mtu lifti mmmhhh utaishia njiani..wengne unampa lifti anataka yeye awe muongeaji kuliko mwenye gari
Sahihi kabisa
 
Ngoja namie nilete
1.2008 nilikuwa naenda tabora na gari binafsi mie ndio dereva tukapita manyoni via itigi kufika katikati ile gari ilichomoka sterling arm ikapinduka mara mbili huwez amini hakuna hata aliye chunika Kati ya watu wanne tuliyokuwepo ndani ya gari

2.20014 mwezi wa tano nilinusurika kufa kwa kuchomwa Moto mitaa ya mbezi jogoo baada ya kuiba gari ila mwana mmoja alipigwa kibiriti
naomba niishie hapa
Nishakupata we ndo ulimkaba mdogo wg akiwa dereva tax afrikana Dogo kwa ujasili akalipeleka kwenye ngema mwenzio alipigwa kibiriti palepale we ukakimbia ni mitaa ya abarikiwe Njia ya kwenda jogoo ,wewe nazani wizi umeacha Sasa hivi
 
Nilishawahi kunywa vile sio vikombe ni jagi zile za maji..
Almanusra nife ila nilikurupuka nikapiga mbizi za ajabu halafu niliokuwa naoga nao majinga Yale yalinikimbia yalipoona huyu mtu kwisha habari.. ila nami nashukuru kwa nguvu zangu nilitoka na huo ndo ukawa mtiketi kwa wote kusema turudini nyumbani..

Maji mpk leo nakuheshimu..
Mkuu hata mimi imewahi kunitokea wenzang wakanikimbia..... Dah lkn Mungu ni mkubwa nilifanikiwa kujiokoa
 
1.mie nlipinduka na gari chali tyres juu nilichubuka mkono tu,
2.ya pili gari niliteremka nayo toka mlimani tyre ya mbele ikachomoka ikaenda piga ngema tukatoka salama.
3.Siku nyingine tyroid hand ikachomoka gari ikanipeleka porini tukatoka salama.
4.Naenda kihansi huko tena gari ikochomoka tyre ya mbele nikaingia porini nikatoka salama
5.Nyingie nimesafiri usk usingizi ukanishika wkt jamaa zangu niliwaambia nyie msilale mniangalie nisipitiwe na usingizi bwana wote tukalala nilisikia ngu..nimegonga karavart tukaingia poeini tulitoka salama.
6.Nilitoka mikumi rough road ya kilombero aisee gari naona inaenda porini tyre tena imechilomoka break karavart.

Basi namshukuru Mungu hata kwisha kwa ile kazi maana sio ajali zile.
Wew umetisha mkuu
 
mwaka 2000 sita sahau nilipewa panga nikanoe kwajili ya kukatia mti, wakati nishalinoa narudi home nikawa nalichezea kwa kulitupa chini linaganda kwa kusimama kwenye ardhi,njia nzima ndio ukawa mchezo, ile nakaribia home si nikalitupa tena chini ,,,,,daaa sitasahau panga lile ligonga jiwe likanirudia shingoni, bahaati nzuri likanichapa na upapa kwenye koromeo, nilipata wenge nusu kukata moto....Wiki nzima chakula kikawa hakipiti mwendo wa uji tu' Mungu mkubwa alikunipiga kwenye makali
 
mwaka 2000 sita sahau nilipewa panga nikanoe kwajili ya kukatia mti, wakati nishalinoa narudi home nikawa nalichezea kwa kulitupa chini linaganda kwa kusimama kwenye ardhi,njia nzima ndio ukawa mchezo, ile nakaribia home si nikalitupa tena chini ,,,,,daaa sitasahau panga lile ligonga jiwe likanirudia shingoni, bahaati nzuri likanichapa na upapa kwenye koromeo, nilipata wenge nusu kukata moto....Wiki nzima chakula kikawa hakipiti mwendo wa uji tu' Mungu mkubwa alikunipiga kwenye makali
Duuh! Pole sana kweli hapo ulinusurika.
 
Niliwahi kukabwa na wahuni maeneo ya Buguruni katika harakati za kutafuta papa la bei chee.

Ile nimechukua bodaboda inipeleke eneo la tukio, kumbe bodaboda boy ni agent wa vibaka, wakaniungia msafara mpaka eneo la tukio.

Jamaa wakanipeleka zile chocho zao karibu na police post pale, wakanifanikiwa kuchukua BukU mbili, na kunilamba makofi mazito kama nyundo ambayo sijawahi kupigwa tangu miaka hiyo.

Nashukuru hawakunipiga na silaha yoyote yenye ncha kali kama zile wanazotumia MATAGA.

Ujana una mengi sana.
bado unanunua?
 
kaka yangu mie walimbebea laptop yake..kiukweli wengi wetu unakuwaga ni uswahili tu kuna wakati usafiri unakuwa wa shida sana yaani lakini mtu unapita kituoni umeweka mziki wako mkubwa tu lakini ndani ya gari niko mwenyewe ...unajua ukimpa mtu lifti mmmhhh utaishia njiani..wengne unampa lifti anataka yeye awe muongeaji kuliko mwenye gari
vipi watoto wazuri huwa unawapa lift?
 
Ngoja namie nilete
1.2008 nilikuwa naenda tabora na gari binafsi mie ndio dereva tukapita manyoni via itigi kufika katikati ile gari ilichomoka sterling arm ikapinduka mara mbili huwez amini hakuna hata aliye chunika Kati ya watu wanne tuliyokuwepo ndani ya gari

2.20014 mwezi wa tano nilinusurika kufa kwa kuchomwa Moto mitaa ya mbezi jogoo baada ya kuiba gari ila mwana mmoja alipigwa kibiriti
naomba niishie hapa
Tukio la kwanza, gari ilikuwa ya wizi?
 
Mikasa yangu ni ya zamani sana, enzi hizo wasomaji wengi itakuwa walikuwa bado hawajazaliwa.

Siwezi simulia mikasa mingi sana ya majaribio ya kuuawa vitani yaliyonipata kwenye 'operesheni Kagera'.

Ila ninasimulia mkasa mmoja tu kama ku support thread.

Vita vilipomalizika mwaka 79' rais wa wakati huo Julius Nyerere, aliingia mkataba wa kiulinzi wa miaka miwili na serikali ya Uganda.

Hivyo tukabakizwa huko ingawa wengine walirejea nchini Tz baada ya vita kumalizika mwezi wa7, 79'.

Kituo changu kilikuwa ni Arua, kaskazini mwa Uganda sehemu inaitwa Rhino Camp, si kambi ya faru isipokuwa ni jina tu, mji wenyewe ni mdogo ni kama kitongoji, upo pembezoni mwa mto Nile mashariki mwa mji wa Arua.

Tulizoezwa na wananchi kuletewa taarifa kama kuna sehemu wapo majambazi wenye kutumia silaha ama askari wa Amini.

Tukipewa taarifa huwafuatilia na kuwakamata ama kuwaangamiza wakileta ubabe.

Baadaye kazi hiyo mimi na jamaa zangu kama wawili hivi tukaigeuza ni fursa.

Ikawa sasa hizo taarifa hatusubiri kuletewa, tukaanza kuzitafuta wenyewe kwa kuweka wapelelezi wetu na wakishatuletea, hatuzifikishi kwa wakubwa, tunafuatilia wenyewe kukamata kisiri, kupora ama kuua hao majambazi na hao askari watoro waliojificha bila ya kuwafikisha hata sehemu inayohusika.

Siku ya tukio, 'informer' wetu akatuletea taarifa kuwa kuna sehemu yupo askari wa Amini kajificha.

Nikachukua genge langu tukiwa watatu, bila kutaarifu wakubwa zetu, sisi hao na silaha zetu, risasi na mabomu ya mkono ya kutosha mifukoni ili huyo askari tukamkamate kama kuku, kisha tumpore na kumdhalilisha akileta ubishi tumalizane naye.

Tulipokaribia umbali flani yule kiherehere wetu akatuonesha hiyo nyumba kisha akasepa.

Nyumba hiyo bila shaka ilikuwa ni ofisi flani kutokana na mazingira tuliyoyakuta.

Tulipofika nje tukajipanga, wenzangu wawili wakasimama kwenye kona pande mbili, mimi nikaenda dirishani kuchungulia.

Nilivyochungulia nikamuona jamaa yuko bize kishenzi,anapekua nyaraka za makaratasi kwa kutumia mkono mmoja, mkono mwingine kashika bastola aina ya chinese 9mm.

Wenzangu nikawapa ishara ya kwamba nimeshayaona mawindo, hivyo wakae tayari.

Nilivyosheheni silaha nilijaa dharau, nikaona huyo jamaa nimshitue nitakavyo, tena kwa dharau, furaha yangu nione anavyoweweseka kisha nimshitue kwa risasi na kelele za maneno ya kumuamuru atupe silaha yake chini haraka.

Ebanaee, kumbe hilo lilikuwa ni kosa la mauti!

Nilivyomshitua kwa sauti 'wewee', kimbembe ndipo kilipoanzia'!

Huyo jamaa alikuwa ni askari aliyefuzu mafunzo yake kwa ukamilifu kabisa, ama alikuwa ni full commando, maana sauti yangu ilipomalizikia, ikaendana na ufyatuaji wake wa risasi kwangu direct.

Alikuwa ni mtu mweledi wa kutumia silaha, maana risasi yake ilinilenga katikati ya paji la uso nilipokuwa nimemchungulia pale dirishani!

Nilihisi kuchanganyikiwa, ama kwa hakika nilichanganyikiwa!

Matendo matatu yalikwenda kwa pamoja: sauti yangu, sauti ya risari toka kwa adui, kishido kikubwa sana kilichoambatana na cheche usoni mwangu, muda huo huo nikajikuta chini, nikahisi jamaa kaniua!

Kilichosaidia pale ni uzoefu wa kanuni ya kupigwa, lakini kusema kweli nilikuwa nimegwaya pakubwa.

Ni kwamba, ukisikia mlio kwa vyovyote haujafa na haujaumia, mzima wewe, badili eneo ulipokuwa kwa kugaragara zig zag kisha chunguza, ndivyo nilivyofanya!

Dah!

Nikapeleka kiganga usoni kukagua damu, hakuna!

Nikaropoka kwa hasura huku nikiweweseka: 'yaani hata mimi unataka kuniua!'

Wakati nipo chini ninahema kwa wasi wasi na nisijue kilichotokea ndani ya sekunde moja, jamaa zangu wakazunguka kwa kasi upande wa pili, walipochungulia wakamwona jamaa kajibanza kwenye kona kama swila tuli na silaha yake mkononi vile vile akijua kwamba kaua!

Ndipo wakamlamba chuma akasota chini na ikawa ndiyo mwisho wake.

Sasa tulipokuja kuchunguza pale dirishani ni kwamba, jamaa alinilenga vizuri sana, kilichokuja 'kuharibu' ni ile risasi kupiga kwenye nondo ya dirisha, hadi ile nondo ilipinda ndiyo ikawa manusura yangu, vinginevyo leo nisingelijua hata Jf inafanana fananaje!

Nina visa vingi sana vya enzi zetu hizo, vingi ni vya kutisha na kutia huruma, ila sasa niishie kwenye huu mkasa mmoja.
Ubabe, dhulma na unyanyasaji ni hulka ya wanajeshi wetu!
 
Mara ya kwanza tulikuwa watatu tukiwa chini ya miaka 7 tulinusurika kufa maji, tulimpoteza mwenzetu wa miaka minne. Ile picha jinsi alivyokuwa anaomba msaada tumsaidie haijafutika kichwani kabisa japo nimevuka 30 lakini kumbukumbu ni kama tukio la juzi tu.
Mara ya pili radi ilipiga kama mita 15 toka nilipo, ile shoti si ya mchezo, sitaisahau.
 
Niliwahi kukabwa na wahuni maeneo ya Buguruni katika harakati za kutafuta papa la bei chee.

Ile nimechukua bodaboda inipeleke eneo la tukio, kumbe bodaboda boy ni agent wa vibaka, wakaniungia msafara mpaka eneo la tukio.

Jamaa wakanipeleka zile chocho zao karibu na police post pale, wakanifanikiwa kuchukua BukU mbili, na kunilamba makofi mazito kama nyundo ambayo sijawahi kupigwa tangu miaka hiyo.

Nashukuru hawakunipiga na silaha yoyote yenye ncha kali kama zile wanazotumia MATAGA.

Ujana una mengi sana.
Kwa hiyo hilo papa ungelimlipa buku mbili
 
Mara ya kwanza tulikuwa watatu tukiwa chini ya miaka 7 tulinusurika kufa maji, tulimpoteza mwenzetu wa miaka minne. Ile picha jinsi alivyokuwa anaomba msaada tumsaidie haijafutika kichwani kabisa japo nimevuka 30 lakini kumbukumbu ni kama tukio la juzi tu.
Mara ya pili radi ilipiga kama mita 15 toka nilipo, ile shoti si ya mchezo, sitaisahau.
Kwanini hamkumsaidia mwenzenu jamani 😱😱
 
Aisee sitasahau nikiwa kijana wa miaka 20hivi nihitimu kidato Cha nne nikiwa mtaa tu nasubiri matokeo damu ikiwa inachemka , nagegeda mabinti Kama Nina pepo hivi , Mara nikampa ujauzito mtoto wa watu , wazazi ni moto Atari natafutwa kila Kona, issue ushafika adi polisi, nikaanza maisha ya kukimbia kimbia , nkapoteza dila kabisa, ela Sina adi nkafikia hatua ya kuanza kuunza nguo zangu ili ni survive, niliuza nguo zote nikabaki na kaptura ambayo mwanzo ilikua suruali kabla ya kukatwa km ujuavyo mitoko ya vijana wa mtaan nikiwa pamoja no t short moja tu kuu kuu pamoja na yebo yebo,

Bs sikuhiyo baada ya kutoka pango nililokua nimelala mida ya saa kumi hivi mapema ili watu wasinikute maana nilikua nalala kwenye kibanda flani ambachp hua wanauza nyanya na mazaga mengine, asubuhi hiyo niliwaza kwenda kufua nguo hizo nilizovaa adi zikauke kwenye mto wa jirani , kwa kua sikua nafahamu njia nzuri za kufika nilijikuta nakatisha kwenye nyumba za watu , bahati mbayaa njia niliopita mbele ilikua haiwez kukutoa nkajikuta kwenye geti la mtu, fasta nataka kurudi nilikotoka nakutana na watu wanakuja upande ule nilikokwama nikasikia mmoja akisema mwingine si huyu alijificha huyuu nilijiesemea tu MUNGU NITANGULIE, waliniweka mtu Kati na kuamsha majirani wengine, nilijitetea Sana adi kulia machozi mengi huku nikishikilia miguu ya Mama mmoja hivi nikimuomba anisamehe mm si mwizi nilipotea njia tu, watu walianza kurusha ngumi lakini Yule mama alinionea huruma na kuanza kulia kua wasinipige ikabidi nitaje adi shule niliosoma nilitaja adi walimu na mkuu wa shule pamoja na vilanja bs walinichapa MAKOFI tu na kuniacha niende zangu MUNGU MWEMA sitosahau hii ishu.
Ulikimbia na kujificha hadi lini?
 
Dah! Nimekujibu kwa urefu Bushmamy but comment haijatokea, naona uvivu kurudia, kwa ufupi narudia.
Tukiwa chini ya miaka 7, mimi na watoto wa dada tulishauriana tukaoge mtoni wakati wazazi wetu wakiwa shambani.
Kwa bahati mbaya kina cha maji kiliongezeka kutokana na mvua. Tulipofika mtoni, ile sehemu ambayo huwa tunaingilia tukaona maji ni mengi zaidi halafu yana kasi.
Tukamwambia dogo ambaye alikuwa na miaka minne hivi abakie pale pale, kisha sisi tuzunguke upande wa pili kupitia daraja.
Sasa wakati tumezunguka upande wa pili, ile furaha ya kumwona dada yake na mjomba wake (mimi) upande wa pili, ikamfanya aingie kwenye maji ili atufate.
Sehemu aliyoingia ilikuwa na kina kirefu kwa siku ile kama nilivyosema kutokana na mvua.
Tulishuhudia akiomba tumsaidie huku akienda, alipojaribu kusimama maji yalimpiga ngwala hadi akapotea. Tulitamani tusogee but ilikuwa ni hatari zaidi kwetu. Tukachukua tu nguo zake tukaenda nyumbani kutoa taarifa.
Kumbukumbu huwa hazinipotei kabisa kwa sababu alikuwa ndugu na rafiki.
 
Daaah..huu uzi umenikumbusha mbali sana enzi hizo nikiwa na umri wa kama miaka 13 hivi.Tulikuwa tunaishi karibu na ghorofa kubwa za shirika la nyumba basi tukawa na tabia ya kwenda kucheza kule kwa staili ya kuteleza kwenye kingo na kuangukia chini..Sasa bwana siku iyo wakati tunacheza mimi niliteleza nikaangukia kwenye chemba ya choo nikadumbukia huku najiona kabisa mpaka usawa wa kifua,ghafla akatokea mzee mmoja mjeda akaja kuniokoa.Nilivyoachiwa nilipata wenge kali sana na mavi yangu mwili mzima nikakimbia kuelekea nyumbani spidi ya Usaini Bolt wale wenzangu niliwakuta njiani nao wanakimbia niliwakimbiza walivyoniona walipiga mayowe makali sana kama wamekutana na msekule..Sitoisahau hii siku
Nimecheka hadi nikashikwa na kizunguzungu cha ghafla!
 

Similar Discussions

69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom