Umeshawahi kunusurika kifo? Tuelezane ilivyokuwa, kama njia ya kumshukuru Mungu

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,442
11,935
Salaam

Maisha yana mapito mengi mazuri na mabaya na pia yapo yale ambayo unaona kabisa hiki ndiyo kifo chako ila unajikuta hai tena bila kutarajia!

Binafsi nimepitia mengi na namshukuru Mungu kuniepusha, leo nitashea nanyi. Twende pamoja.

Wakati bado ni kijana wa miaka kama 20 hivi nilikwenda likizo kijijini kwa dada yangu ili kubadilisha mazingira kidogo, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kwenda huko na wenyeji wa huko asilimia kubwa ni ndugu hivyo nilipangiwa nikalale kwa kijana wa rika langu ambae pia alikuwa mwanafunzi kipindi hicho.

Huyo mwenzangu hakuwa mtu wa matembezi kabisa muda wote ni ndani kujisomea tu hivyo nikaungana na vijana wengine ambao pia ni ndugu kwenda kuangalia video kwenye banda nyakati za usiku, ilikuwa kama saa nne kasoro hivi na kumbe muda huo wanaweka picha za ex kwa siri lakini na hii ni baada ya watoto kutoka.

Tulibaki watu wachache tu na picha likaanza ila ghafla tukashangaa mtu anakuja mbio huku akiwa na panga akajichanganya na sisi! Mara wakavamia polisi kama nane na bunduki na huku wananchi wakiita kelele ya wizi!

Hapo sote tulitoka nduki kutokana hakukuwa na usalama tena, kwa bahati mbaya wenzangu wote walipita chochoro pamoja na yule mwizi ila mimi kutokana na ugeni wangu nikakimbia njia iliyonyooka kuelekea nyumbani...ghafla nikaunganishiwa mimi na jeshi kubwa la wananchi wakiniitia mwizi wakiwa na silaha za kila aina na kunifuata speed sana!

Nilikimbia mpaka ninapolala nikamuita jamaa dirishani afungue lakini alikuwa akiitikia tu, jeshi linakuja cha kufanya sikijui ila nikapata akili ya kuingia kwenye uwa wa chooni na hakuna hata mlango nikabana huko na jeshi likapita na kusonga mbele huku wakisema huyu tumuue wenyewe asiingie mikononi mwa polisi.

Nilinusurika ila hii siku kwangu ilikuwa ni nzito sana na bado ni nzito mpaka sasa pamoja ya kuwa imeshapita miaka mingi.

Pia nilishanusurika kukatwa kichwa kipindi kile cha watu wanaouwa na kutoweka na vichwa, hapa sitaki kukumbuka pia. Na mkasa mwengine ni ule wa kuwapa watu lift kwenye gari na ghafla kamba ikarushwa kutokea siti ya nyuma waninyonge wachukue gari ikiwa bado mpya kabisa!

Namshukuru Mungu kwa yote nipo bukheri wa afya.

Iwapo na wewe yamekukuta yeyote tueleze tujifunze na kumtukuza Mungu.

Alamsiki!
 
Niliwahi kukabwa na wahuni maeneo ya Buguruni katika harakati za kutafuta papa la bei chee.

Ile nimechukua bodaboda inipeleke eneo la tukio, kumbe bodaboda boy ni agent wa vibaka, wakaniungia msafara mpaka eneo la tukio.

Jamaa wakanipeleka zile chocho zao karibu na police post pale, wakanifanikiwa kuchukua BukU mbili, na kunilamba makofi mazito kama nyundo ambayo sijawahi kupigwa tangu miaka hiyo.

Nashukuru hawakunipiga na silaha yoyote yenye ncha kali kama zile wanazotumia MATAGA.

Ujana una mengi sana.
 
Nilishawahi kunywa vile sio vikombe ni jagi zile za maji..😅
Almanusra nife ila nilikurupuka nikapiga mbizi za ajabu halafu niliokuwa naoga nao majinga Yale yalinikimbia yalipoona huyu mtu kwisha habari.. ila nami nashukuru kwa nguvu zangu nilitoka na huo ndo ukawa mtiketi kwa wote kusema turudini nyumbani..😂

Maji mpk leo nakuheshimu.
 
Nilipokuwa mdogo niliwahi kutumbukia kwenye pipa la maji (Yale mapipa ya zamani ya chuma kwa wanaoyafahamu)

Lile pipa lilikuwa na maji nusu nikataka kuyachota bahati mbaya nikawa siyafikii, nikachukua stuli mbili nikaweka kwa kubebanisha nikapanda kuyachota maji,.

Bahati mbaya stuli zikateguka nikatumbukia kwenye pipa kichwa kilitangulia miguu ikawa juu,,,,hadi leo huwa sielewi kwa kweli Mungu huyuuu!!!!
 
Wakati bado niko mdogo nilikwenda kumtembelea bibi yangu aliekuwa akiishi mkoani Singida maeneo ya saranda.

Bwana kuzoea kidogo pale nikawa na rafiki yeye michezo yake kudandia treni likiwa linakuja mpk litakaposimama ndio anashuka na kujiskia raha/msela.

Sasa bwana sikuhiyo na mimi nikaenda kama siku 2 hivi nilifanikiwa na kuja kujisifu sisi ni masela.

Siku hiyo nakumbuka tumesubiri treni limetoka manyoni linashuka mlima ilikuwa usiku wa saa 2 tumevizia nikakamata chuma nipande weee bwana wee nilitereza miguu ikanasa nikawa nabembea kama tumbili huku chuma imekamata reli mteremko ule asee sijui Mungu aliniponyaje mpka leo sielewi nilijikuta chini ninatoka damu mwili umechubuka vibaya asee nilikaa hospitali muda mrefu ila nilipona. Siku hiyo nilijua ndio mwisho wangu.
 
Utundu huuu jamani
 
Nilipokuwa mdogo niliwahi kutumbukia kwenye pipa la maji (Yale mapipa ya zamani ya chuma kwa wanaoyafahamu)

Lile pipa lilikuwa na maji nusu nikataka kuyachota bahati mbaya nikawa siyafikii, nikachukua stuli mbili nikaweka kwa kubebanisha nikapanda kuyachota maji,.

Bahati mbaya stuli zikateguka nikatumbukia kwenye pipa kichwa kilitangulia miguu ikawa juu,,,,hadi leo huwa sielewi kwa kweli Mungu huyuuu!!!!

Duh
 
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu, nilinusurika KUFA maji mwaka '88 Bagamoyo Enzi hizo ile Beach ikiitwa BADECO duh nilizindukia hospital baada ya kushindwa kuogelea nikiwa nimelewa konyagi. Na mwaka huu mwezi wa pili nimepata ajali mbaya ya gari ila Mungu ni mwema nilitoka salama.

IMG_20200227_130820.jpg
 
Sitasahau nilivyokoswa koswa kuchomwa na kuti la kuni, nakumbuka nilikatiza kwenye gari ambalo walikuwa wanashusha kuni, basi jamaa kuni ikamponyoka huku ikinilenga mimi hatimae nikapishana nayo kidogo kwenye paji la uso, aisee yule jamaa alikua kashika kichwa kabisa akiamini kauwa

Kwa uwezo wa Mungu nikanusurika,

Part2 sitosahau nilivyonusurika kugongwa na roli

Nilikaa maskani napiga story ghafla akaja mama mmoja alinitaka nikamnunulie hindi la kuchoma ng'ambo ya barabara, nilivuka safi kabisa wakati wa kwenda, wakati wakurudi ikawa kasheshe niliona roli la mchanga linakuja kwa kasi wakati huo nipo ktk ya barabara nikajikuta naishiwa nguvu hatimae lile roli likawa kama kuna mtu kalizuia lipunguze speed then nikavuka

Yote na yote yule mama alipanga kunitoa kafara kumbe, sitosahau kwakweli.
 
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu, nilinusurika KUFA maji mwaka '88 Bagamoyo Enzi hizo ile Beach ikiitwa BADECO duh nilizindukia hospital baada ya kushindwa kuogelea nikiwa nimelewa konyagi. Na mwaka huu mwezi wa pili nimepata ajali mbaya ya gari ila Mungu ni mwema nilitoka salamaView attachment 1526349
Mkuu mimi ile Badeco sasa kwa mbele karibu na beach Magambani sekondari nilizama nikala vikombe kama viwili lakini Yesu akasema bado kusudi langu nawe halijaisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom