Noel wa ruben
JF-Expert Member
- Oct 11, 2020
- 364
- 509
Nimecheka kwa sababu bado umzima,pole Sana mkuu.Wakati bado niko mdogo nilikwenda kumtembelea bibi yangu aliekuwa akiishi mkoani Singida maeneo ya saranda.
Bwana kuzoea kidogo pale nikawa na rafiki yeye michezo yake kudandia treni likiwa linakuja mpk litakaposimama ndio anashuka na kujiskia raha/msela.
Sasa bwana sikuhiyo na mimi nikaenda kama siku 2 hivi nilifanikiwa na kuja kujisifu sisi ni masela.
Siku hiyo nakumbuka tumesubiri treni limetoka manyoni linashuka mlima ilikuwa usiku wa saa 2 tumevizia nikakamata chuma nipande weee bwana wee nilitereza miguu ikanasa nikawa nabembea kama tumbili huku chuma imekamata reli mteremko ule asee sijui Mungu aliniponyaje mpka leo sielewi nilijikuta chini ninatoka damu mwili umechubuka vibaya asee nilikaa hospitali muda mrefu ila nilipona. Siku hiyo nilijua ndio mwisho wangu.