Tajiri wa Magomeni
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 4,274
- 2,921
Pole Sana.haukupata ulemavu wowote?Mimi ya kwangu hii iIikuwa mwaka 2007 kipindi hicho nipo form two katika mojawapo ya mikoa ya nyanda za juu kusini, siwezi kusahau radi ilivyokosa kunitoa uhai mimi pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzangu. Nakumbuka siku hiyo ilikua tupo kwenye foleni ya kupata chakula cha mchana na siku hiyo mvua ilikua inanyesha kubwa sana ambayo ilikua inaambatana na radi kama kuna wenyeji wa hiyo mikoa hasa Njombe wanaweza kuwa mashahidi kule huwa kuna radi za hatari sana.
Wakati nipo kwenye foleni ninachokumbuka niliona mwanga mkali uliombatana na mngurumo wa radi, nilihisi kupigwa na kitu kizito kifuani na kurushwa kutoka pale nilipokua kwenda umbali wa mita kadhaa, baada ya hapo kilicho endelea sikuweza kufahamu zaidi ya kujikuta nipo hospital na drip za maji, nilikaa pale hospital kwa siku mbili nikiendelea kuongezewa maji mwilini pamoja na sindano tena nakumbuka hizi sindano nilikua nachomwa kwenye mishipa ya mikononi na jina lake ni kristapeni, sindano zinauma hizi kamwe siwezi kusahau.
Hili tukio siwezi kulisahu kiukweli sababu mpaka leo ile radi imeniachia baadhi ya makovu hasa maeneo ya kifuani kwa sababu ni kama ilinichubua nikawa na vidonda, nakumbuka walikua wanakuja watu kutoka maeneo jirani kunipa pole kwa sababu ilikua ni kama bahati kusikia mtu amenusurika baada ya kupigwa na radi lakini pia siku hiyo hiyo mimi nilipopigwa radi kuna sehemu ndani ya mkoa huo huo iliua watu wengine wakiwa shambani.
Nakumbuka nilvyorudi shuleni kila mtu hakuwa anaamini kama ningeweza kupona, samahani kwa uandishi mbovu nimeona nijaribu kufupisha sababu ni mengi siwezi kuandika yote hapa.