Umeshawahi kununua dawa za kupunguza tumbo, kuongeza shape au nguvu za kiume mtandaoni? Unajua dawa hizo zimechanganywa na nini?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Uzito uliopitiliza, shape na nguvu za kiume na mambo ambayo yanasumbua sana watu na kuna baadhi wako radhi kufanya chochote ili atimize moja la hitaji lake hapo juu.

Dawa hizo nyingi hazitambuliki na mamlaka za dawa na chakula, wanaokuuzia wengi hawajui zimechanganywa na nini, na hata wanaodai kutengeneza dawa hizo wenyewe hawana utaalamu kuhusu tiba.

Baadhi ya michanganyiko hii inakuwa na sumu kutokana na ukweli kwamba wanaotengeneza hawana utaalamu wowote na baadhi hawajali nini kinachanganya hata kama kitamdhuru mtumiaji mradi yeye ameingiza pesa.

Unaweza usipate madhara hayo mara baada tu ya kutumia, lakini sumu ikabaki kwenye mwili wako baada ya miaka hata kumi huko ndio ukaanza kuona madhara yake.

Kwenu wakuu, umewahi kutumia dawa hizo kutoka mtandaoni? Unajua ni kitu gani hasa uliingiza mwilini?
 
Ni kazi bure mkuu, wabongo wengi wanaishi kwa hisia na kuchukulia mambo kiwepesi.

Mtu anashindwa kuamini hospitali, ina mifumo maalum iliyothibitishwa, anaamini maneno ya watu 'kwangu ilikua hivi' 'kwangu ilisaidia'

Na wanajazana kwa watumishi waombewe wapone, imani potofu bado ni tatizo kwa kweli.
 
Africa Ina dawa nyingi za miti Shamba sema ni secta haipewi research Kwa maksudi sababu miradi ya malaria TB n.k ni billion dollar business so hizo research hazipewi fund Ili dawa zitoke nnje Kwa kununuliwa Kwa dollar.
Chukua mfano kozi yoyote ya bure ya Herbology ktk mtandao , jielimishe na utangundua umezungukwa na dawa kibao hata hapo nnje kwako sababu tu hujui .
Kuhusu dawa feki ni kuwa usinywe dawa yeyote ambayo mmea wake haupo ktk Google maana kila mmea Duniani unajulikana na kiwango chake Cha sumu/toxicity.
Hizi dawa mbazo hazina maelezo ya aina ya miti iliyotumiwa ni za kuogopa
,usiguse.
 
Mara paap dawa inafanya kazi kinyume kwako matokea yanakuwa tofauti 😂 😂 😂 ... ila serious mkuu, kama unapanga kupungu kuwa na nidhamu ya kwenye chakula tu ...suala la shape hilo tumuachie muumba
😂😂 dawa inakata mafuta ya chips, full stop.
 
Nature ya binadamu haiko katika kukaa tu na kusubiri kufa… ila nyie wasabato endeleeni kusema soda ni kansa tupu, kunywa maji mpk figo zielee kisha zifail… wote tutapatana paradiso
Nimecheka kwa sauti aisee
 
Back
Top Bottom