Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Hapo kwenye kisa cha kwanza cobra.
Kuna aina nyingi za cobra. Cobra anaerusha mate ni aina moja tu anaitwa Mozambique spitting cobra (Moza)
Angekua ni Moza angekua amekurushia mate muda mrefu sana na asingekukosa.

Kuhusu chatu yeye hana sumu ila ni hatari sana.
 
kuna siku nimeenda kijijini sasa katika harakati nikapata demu mmoja hivi tukawa tuko sehemu tuna kulana tumemaliza tukawa tuna sindikizana taratibu bila shida sasa tukafika mahali tukaagana wakati mimi naondoka na njia moja hv ya nyasi ndogo naona ghafla nyoka wawili wanatokea upande wa kushoto. wakati manzi ananiangalia nikiwa naondoka akashangaa nakimbia shambani bila mipangilio naenda mbele naona mwingine aisee nilipotelea bondeni bila kupenda akili imekuja kurudi niko kilometa mbili nahema natetemeka maana yule nyoka alikuwa wa kijivu na amesimamisha kichwa aisee manzi alikuwa nanishanga.

nafika home nimesahau kama nilitoka kupiga show na nimeingia ndani nahisi kila kona kuna nyoka acha kabisaaa
 
Ukiwa unakimbia matukio hatarishi Kama la nyoka,miguu inakuwa haigusi chini. Kiufupi unakuwa unapaa.
 
Aisee,

Me nilidhani alinionea huruma maana nilishaanza kulia na kutaharuki.
 
Kwan mikoa ya kusini suala la cobra sio habar ya kushangaza maana wamepakana na msumbiji, kule wanapatikana cobra maarufu duniani wanaitwa MOZAMBIQUE SPITTING COBRA, Ni hatar na nusu[emoji4]
Na haya matukio yote niliyosimulia kasoro la Dangote yametokea kusini kwa mzee Membe RIP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…