Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Moja kati ya Game Kali sana ya kucheza kupitia simu au kompyuta yako basi ni hii the Walking Dead season 1, 2,3 na 4. Ni game nzuri yenye msisimko wa kipekee utakao kufanya ukicheza unafurahi kinoma.
Game hii iliundwa na kampuni inaitwa Telltale ni kampuni nzuri ya kuunda Game nzuri balaa wakishirikiana na LCG entertainment, ndani ya Game ya the walking Dead ni game ya mazombie yenye graphics Kali balaa Iliyo na mission za kibabe.
game hii mara ya kwanza iliachiwa mwaka 2012 ,season ya kwanza ikiwa na Episode 5, ambapo utaweza kucheza kwenye playstation 3, android, iOS, Xbox, windows, linux, Mac os, Xbox360, Nintendo na Playstation 4.
Game inahusu mazombi ambapo Mji wa George Washington ambao ulipatwa na kirusi na kuhalibiwa na mazombie ilipelekea watu wengi kuathirika
lakini story inaanzia kwa jamaa anaitwa Lee Everett ambaye alikamatwa na polisi wakati anapelekwa kituoni gari inapata ajari na kuingia kwenye maporomoko
kwa bahati mbaya askari aliyekua anampeleka lee anang'atwa na mazombi.
Sasa utaanza kumchezesha lee kujinasua kwa askari huyo ambaye amegeuka zombie ila hii utamu wake unakuja baada ya lee kugeuka zombie utamchezesha mtoto anaitwa Clementine ni Game Kali sana ukicheza uta enjoy.
⚡ graphics Kali
⚡ Game nzuri ++ sauti tamu haswa ukivaa Headphones 🎧
⚡ Ina cheza kwenye vifaa vingi mnoo
⚡ ni ngumu na unatumia akili nyingi 🔥