Umeshawahi fikiria usiku wako wa kwanza kaburini?

Na wewe ulitakiwa uyachukue huko waliko ya toa wao.

Ushawahi kusoma "Elimu ya uhakiki wa habari ?"

Wewe huwa unatumia vigezo gani kuthibitisha kama habari fulani ni ya kweli au si ya kweli ?

Leo sitaki uniambie, "Nitakujibu siku nyingine"

Nipo ...
Mimi si msomi...nimekiri.

Naomba niishie hapo.
 
Uwa nikikaa natafakari sana juu ya usiku wa kwanza kaburini uwa nakosaga amani, namaanisha siku ya kwanza kuzikwa.

Natafakari juu ya hatma yangu na Allah itakuwaje? Dunia ya Leo ambayo ukiwa macho tu unatenda dhambi,ukilala unatenda dhambi.
1.rushwa
2.riba za mikopo.
3.michezo haramu ya kubet
4.mtaani huku tunazini kila siku mikia ya hatari.
Kweli nimeamini kizazi hiki ni kigumu sana.
Tafakari chukua hatua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba ni anze kwa kucheka kidogo "haha haha haha.." sasa mkuu niliwahi kuambiwa kuwa siku ya kwanza pale unapozikikwa kaburini, anasikia maongezi yote yanayo endelea na wewe pia uonatoa sauti watu hawakusikii, wanaosikia ni wanyama na wadudu.

Baada ya watu kukufukua unasikia watu nanaondoka, unazidi kupiga kelele hawakusikii. shughuli anazia hapo watu hawapo wanakuja wale wanyama na wadudu ambao uliwauwa kwa makusudi kwa mfano tandu, ndege kama kuku na wengineo wanaaza kukushambulia...

hiyo ndio siku ya kwanza...jiandae kukiona cha moto...
 
Hahahahhahahahha daaaaah.
Dunia ina viumbe wa ajabu sana sasa wew hapa Umeandika nini,unapo andika Quran ni mwongo wa watu wakina nani kwamba mimi sipo acha ubaguzi wa kifala halafu mimi najua Quran kupita hata wew, Binafsi kabla sijapitiwa na usingizi lazima nisome Quran pia kisha nifungulie kwenye simu nisikilize na huu ni utaratibu wangu.
 
Unajuwa haya mafundisho ya hizi dini ni ya kipumbavu sana kama hautumii akili kufikiri.Umeshawahi kujiuliza ulikuwa wapi kabla ya kuzaliwa jibu hakuna anayejuwa.Kwa sababu haukuwepo and the same ukifa unakuwa haupo

iPhone 7plus

Kwa kufikiri kwa kutumia kiungo sahihi cha kufikiri, kabla ya kuzaliwa kwako kulikuwa na uwezekano wa wewe kuzaliwa.
Kinyume chake unapokufa uwezekano wa wewe kuja kuwepo tena haupo.

Ili uwepo mara mbili inahitaji yale yote yaliyosababisha wewe uwepo yawepo pia. Jambo haliwezekani ndugu zangu! Babu/bibi zako wawepo, wazazi wako wawepo kwa wakati uleule ambao mimba yako ilitunga, mazingira yote yawepo kwa kila sekunde iliyokuwa ikipiga, WAKATI NAO UWE NI ULEULE JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI KABISA KWA KUWA WAKATI ULE ULISHAKUWA NI WAKATI ULIOPITA!

Tangu lini unaweza kuchukua video ya tukio fulani kinyumenyume? Huu ni mfano rahisi kwamba haturudi nyuma bali tunaenda mbele. Hii pia ni kanuni ya ulimwengu kwamba, wakati uliopita umekwisha kupita!

Au kwa lugha iliyo rahisi sana, tunapaswa kujua sisi ni wakati tunaoishi sasa....
 
Kwani kabla hujazaliwa huyo Allah ulikuwa unamjua.? Mbona unajisumbua kuwaza mambo ambayo utakapo kuwepo huko utakuwa hauna ufahamu lbd uwe haujafa lkn you can't sense anything ukiwa umekufa nothing to worry.
 
Dunia ina viumbe wa ajabu sana sasa wew hapa Umeandika nini,unapo andika Quran ni mwongo wa watu wakina nani kwamba mimi sipo acha ubaguzi wa kifala halafu mimi najua Quran kupita hata wew, Binafsi kabla sijapitiwa na usingizi lazima nisome Quran pia kisha nifungulie kwenye simu nisikilize na huu ni utaratibu wangu.

Mtume mtukufu (saw) "jiepusheni na ghadhaba", hapo inaonekana ndugu yangu umeshikwa na ghadhabu mpaka umeshindwa kuelewa nilichoandika, wewe umesema huwa unafungulia Qur'an na unaisikiliza hadi "usingizi unakuchukua"--- mimi nikakuambia kuwa haitakiwi kuifanya Qur'an kama chombo cha kuletea usingizi (kibembelezo), na nikakuambia kuwa kazi ya Qur'ani kwetu sisi watu ni muongozo ili tushike njia sahihi Mungu anayotaka tuishike. Hiyo ndiyo ilikuwa maana yangu.

Kuhusu kuifanya Qur'an kuwa kibembelezo, Allah (swt) anasema:-

Wa idhaa qaria alqur'an faastamiuulahu wa unswituu laalakum turhamuuna. (Ala'raf:204)

Yaani:- Na isomwapo Qur'an isikilizeni na mnyamaze ili mpate kurehemewa. (7:204).

Sasa wewe unafungua Qur'an badala ya kukaa kimya na kuisikiliza maudhui ya aya unajilaza hadi usingizi unakupitia!!, wewe unadhani hiyo Qur'an ni mziki?!!. Halafu unatamba eti unajua Qur'an kuliko mimi!!, kama ungaliijua hiyo aya hukuiona??, wewe unajua kuisoma tu lakini hujui kuitekeleza na kuizingatia.

Baadhi ya Aya zinazoeleza kuwa Qur'an ni muongozo kwetu (watu wote) ni:-

Luqman:2-4, Bani israel:9, na 105, Al baqara:2-3, nk.

Wa akhir dau'anaa alhamdulillah.
 
Naomba ni anze kwa kucheka kidogo "haha haha haha.." sasa mkuu niliwahi kuambiwa kuwa siku ya kwanza pale unapozikikwa kaburini, anasikia maongezi yote yanayo endelea na wewe pia uonatoa sauti watu hawakusikii, wanaosikia ni wanyama na wadudu.

Baada ya watu kukufukua unasikia watu nanaondoka, unazidi kupiga kelele hawakusikii. shughuli anazia hapo watu hawapo wanakuja wale wanyama na wadudu ambao uliwauwa kwa makusudi kwa mfano tandu, ndege kama kuku na wengineo wanaaza kukushambulia...

hiyo ndio siku ya kwanza...jiandae kukiona cha moto...

Hivyo ni visa na ngano walizobuni watu wasiojua sawasawa elimu ya dini na hususan mambo yaliyofichikana kwa madhumuni ama ya kuwatisha watu au kuwafanya watu waiogope sana siku ya kufa na wajitahidi kufanya mema ili adhabu hizo za kubuni zisiwashike wawapo "kaburini"--- (it is a mere out of figment of their own imagination )
 
Back
Top Bottom