Umeshawahi cheza hili game?

Umeshawahi cheza hili game?

nikiwa mtoto siku moja tunatoka shule kijana mmoja akanichokoza. nilikuwa sijawahi kucheza na mtu mchezo huu. niliishia kurusha hewani tu kwa staili za hu! hwa! kama za bruse Lee wakati ule. siku hiyo wapambe wakanipamba nikapambika wengi wakaside nami mstari ukachorwa pambano likaanza. kwa vile upande wangiu ulikuwa na washabiki lukuki nilitoka na ushindi sambamba na manundu. kesho yake tulikiona cha moto kwani walimu walishatonywa kuhusu mchezo ule!
 
siupendi kabisa,jirani yangu mwanae aliaga dunia kwa sababu ya huu mchezo eti wanapigana kama kina cheka
 
huu mchezo cutak kabsa,kpnd nko darasa la 3 nliingilia mzk wa dem 1,nlpasuka
 
hii umenikumbusha nilivyokuwa primary skuli nilishawai kucheza hili game na mkurya mmoja nilichezea kichapo ile mbaya jamaa lilikuwa fiti, nilikuwa sijawahi shindwa ila tokea siku hiyo mkurya yoyote nilikuwa nam-respect.
 
Nifafanulie kwanza ni kulegezwa kwa aina gani ili nijue kwanza afu ndio nijue kama niko tayari au la,nisije nikakubali kichwakichwa mie.
Mkuu ni kweli kabisa steringi huwa hauwawi,lakini huwa analegezwa!

Je uko teyari kulegezwa?
 
Hapo lazima uhakikishe una jiwe mfukoni,mambo yakiwa magumu unapiga kitu cha ngumi ft jiwe ushindi dk sifuri tu:becky:
 
Nifafanulie kwanza ni kulegezwa kwa aina gani ili nijue kwanza afu ndio nijue kama niko tayari au la,nisije nikakubali kichwakichwa mie.
Mkuu ni kuchoshwa tu kwa kawaida katika mapambano!
 
Back
Top Bottom