Umeshaombwa soda airport?

Umslpogaaz

Member
Apr 14, 2008
94
56
Mambo ya soda airport!

Soda airport.jpg
 
sasa wakale wapi? we kama unayo unawapa tu .. sasa unakuta mibongo mingine inaenda kukwea pipa na chenji za taksii, tumia pesa ikuzoee.
 
Mimi askari airport ya egypt aliniomba dola 10 iliyokuwa nimeiweka katika makolokolo yale yanayopita kwenye mashine wakati wa ukaguzi....wafanyakazi wa airport ufikiri kila msafiri anazo!!!
 
Mimi askari airport ya egypt aliniomba dola 10 iliyokuwa nimeiweka katika makolokolo yale yanayopita kwenye mashine wakati wa ukaguzi....wafanyakazi wa airport ufikiri kila msafiri anazo!!!

Tena nasikia airport ya Cairo ni balaa. Kama safari yako inaanzia pale usipotoa bakishishi begi lako wanabaki nalo pale.
 
Kinshasa Airport hawaombi; wanadai. Kwenye sehemu ya ukaguzi niliulizwa: "uko tayari kulipa upite bila kukaguliwa au tumwage vitu vywko vyote kwa ukaguzi?"

Ndo tunakoelekea hata sisi, believe me. Kipe chama cha Mabwepande miaka 10 mingine baada ya JK utaona!
 
Sina utaalamu wakusoma picha ila kwa upeo wangu, Njaa ni hali ya ajabu sana inaweza kukuvua utu wako. Hebu mwangalie huyo afisa uhamiaji! Duh.
 
Hawa sea urchins wanapangusa hata ile shilingi 2,000 or so inayobaki katika kulipia kodi ya airport kama hujaja na chenji kamili na umetoa 20,000. Halafu hawana hata noma wanafanya hivyo baada ya kukuharass sana tu.
 
hilo la kubaki na begi sifahamu aisee ila jamaa wana njaa hao.....

Jamaa wana njaa kwelikweli, kuna jamaa mmoja alifika pale wakaanza kumuomba dollars sasa akawa ana dola kubwa kubwa alitaka awape kidogo kwahiyo akaacha kuwapa wakamwambia "ok". Aliposhuka Dar begi lake halikuwepo. Na kabla ya hapo alishataarifiwa na wenzake wazoefu wa kwenda huko kuwa ahakikishe anawapa yeye akadhani ni utani.
 
Duh....Aminia...basi si bora wa bongo wao wanaomba soda tu....!!!
 
Back
Top Bottom