Mimi bahati mbaya niko mbali na mikoa ya kanda ya ziwa wanakopatikana wasukuma kwa wingi.Bahati nzuri jirani zangu ni wasukuma,sijawahi kuona wasichana vicheche kama wasukuma tena wanapenda kutembea na wanaume walioa wanachojali sana ni pochi yako tu.Labda tabia zao zimeathiriwa na malezi au kukaa mbali na sehemu ya asili ya wazazi wao.
Kitu kingine nilichojifunza kwa majirani zangu wa kisukuma ni kupenda ushirikina kupita kiasi.Kila baada ya muda mfupi kupita lazima walete mganga kutoka usukumani.
Tabia nyingine mbaya ya wasukuma ni ndugu jamaa na marafiki kujazana nyumbani,Pakajimmy ukioa msukuma jiandae kujenga nyumba kubwa kwaajili ya kupokea ndugu na marafiki kutoka ukweni.
Mazee, unapoint nzuri na zote ni valid.
Kuhusu ukicheche, sababu zinaweza kuwa nyingi. Kukaa mbali kama ulivyosema wewe ni mojawapo. Pili, labda umri na mazingira waliyomo yanaendekeza mambo hayo. Kama nilivyosema awali, iwapo wasichana watakuwa wamekuja na umri mdogo hapo, basi uwezekano wa kuwa hawajaishi au kuingiwa na mila za Usukumani ni mkubwa. Kingine, tukumbuke kuwa dunia ya sasa ni ya utandawazi. Hakuna jamii ambayo haiko affected na influence ya mambo ya kisasa kutoka Ulaya na kwingineko ambapo, mapenzi (yasiyoyakweli) au ngono zembe vimeathiri jamii pahala pengi. Si kabila au koo ambapo hutokuta mambo haya ya utandawazi yakiwa ni negative force kwa tamaduni zilizopo au kuzoeleka.
Kuhusu swala la ushirikina, hili jambo ni 50/50 IMHO. Kumbuka kabila la Wasukuma ni kubwa sana. Kuna koo na koo... nyingine nyingi hawaamini hata mambo ya Mungu (ukristo au uislam). Wana abudu miungu yao waijuayo. Isitoshe, dini za Uislam na Ukristo nazo zinatabaka kubwa tu huko. Hivyo basi, mambo ya ushirikina in general ni mambo ya society za Kiafrika. Kuna zile zisizokubaliana nayo na kunazile zinazoyaendekeza. Majirani zako watakuwa ni moja ya kundi la pili kwa maoni yangu.
Kuhusu undugu, hii ni kweli tupu. Lakini nadhani ni easily explainable. Ni mila iliyojengeka kutokana na halihalisi ya living in a land of plenty. Kuanzia ardhi, watu, vyakula, n.k. Wasukuma naturally (kama ilivyokuwa awali), wanamaisha ya kusaidiana, kufanyakazi pamoja na kushiriki kwenye hafla na shughuli nyinginezo kijamii bila kutengana. Hii imejengeka kwenye desturi zao, and sometimes kutokana na kuwa ni desturi ya muda mrefu, inatokea pahala inakuwa executed at wrong time and wrong place. Haswa swala la kuishi mbali na Usukumani linapohusishwa.
Hivyo basi, unaweza kuiita ni tabia mbaya au nzuri, nategemea. Ni mbaya kwa mambo na maisha ya mjini, lakini ni tabia ambayo ni nzuri au yenye mema iwapo, jamii zetu zisingeasirika na msukumo mkubwa kutoka mijini unaoingilia jamii zinazoenzi mila na desturi, haswa vijijini. Na ni kwa nadharia hiyo basi, nami nasema kuwa hii ni mila ya kuacha ife, maana maisha yamebadilika. Na wimbi la mambo ya kimjini na matatizo au forces zote zilizopo katika jamii sasa hivi, hata ujaribu vipi kuzuia zisikukumbe, bado zitajipenyeza. There are times when you have to allow to succumb to negative influences!