Kbd
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,260
- 447
When you lead someone on a path knowing very well the end wont be pleasant for them ,you sure like hell deserve credit for it.Watu wengi wanawake kwa wanaume wanapoingia kwenye mahusiano kwa sababu ambazo ni za kibinafsi mf. sex...pesa...sifa na mengineyo hua wanajua vizuri sana kwamba baada ya wao kupata walichotaka na kuridhika lazima watakua wamewakorofisha/wachanganya wale waliotumiwa kutimiza haja na mahitaji yao kwa namna moja ama nyingine.
Mwanaume/mwanamke anaeingia kwenye mahusiano kwa sababu hizi za kibinafsi alafu akamwaminisha mwenzake kwamba anampenda na ana malengo nae mwenzake anajitolea mengi kuhakikisha mahusiano yao yanachanua.Muda...pesa...marafiki au hata ukaribu wa ndugu unaweza kutolewa kafara kwaajili ya hili alafu siku ya siku mtu anakwambia bwana ehhhh mi nimeshakuchoka au sikupendi tena na kama kaamua kukumaliza anakwambia kabisa nia yangu ilikua kupoteza muda tuna wewe huku nikisubiria wa kunifaa...pole/samahani kwa kukutumia.Muda ulishaenda...waliokupenda kweli ulishawatolea nje sasa nao hawakuhitaji tena...marafiki ulishapoteza kadhaa kwasababu ya mpenzi....pesa ulishatumia nyingi kumsomesha/kumfungulia biashara then unajulisha/gundua kwamba wote ulikua mchezo tu....KWANINI USIONE KWAMBA UMEHARIBIWA MAISHA???!
Mwanaume au hata mwanamke aliye ndoani anapomwaminisha mwenzake yeye ndo yeye kumbe mkewe/mume yuko shule au kamuacha nyumbani mpaka mwenzie anakolea na kuamini ndoa itakuwepo ni muda tu na mipango...ghafla mimba imenasa alafu anakuja ambiwa nna mke/mume mimi ujie....na miaka ilishakata hisia zilishachezewa KWANINI HUYU MTU ASIONE KWAMBA KAHARIBIWA MAISHA in terms of malengo na mipango???!
Mume/mke au mchumba yuko mbali anatuma vijisenti kila mwezi angalau nao siku moja wawe na kwao alafu anarudi kukuta pesa zake zilikua zinamlisha mwanamke/mwanaume mingine au imejengwa akifika anaambiwa hana chake anaingizwa mwingine ndani KWANINI HUYU MTU ASIONE KAHARIBIWA ukizingatia kwamba hata viakiba vyake alivitoa akijua faida ipo?!
Yapo mengi sana yanayompa mtu ruhusa/haki ya kuona ameonewa au hata kuharibiwa malengo na mipango yake aliyojiwekea awali.Ndio kwa kiasi flani hata mkosewa anaweza kua amechangia kwa kutokua wangalifu ila ni wangapi kati yetu wenye bahati ya kufikiria kwa kutumia kichwa badala ya moyo linapokuja swala la kuanguka mapenzini?!Sio wengi....na ndio maana mioyo haiishi kuvunjwa kwahiyo usihukumu kila anaesema hivyo kwamba ni uzembe wake....jua kwanza historia ya aliyomkuta.
Kuhusu wanaoitisha kujiua kwakweli nashukuru sijakutana nao....ila hua najiuliza hua wanapoamua kujia kweli hua wanapania kumkomoa nani haswa maana namjua mzee aliyejiua kwaajili ya mapenzi na mpaka leo hua hata siwezi kuimagine yule mama na wanae watakua wanajiskia vipi kujua yeye ndo msababishi a watoto kujua mama ndie msababishi!
Asante sana Lizzy........umesema yooote niliyotaka kuyasema. Ukweli kuharibiana maisha kupo na watu wengi wamekuwa victimize na hili. Ubarikiwe dia.