Umeniharibia maisha! ...what?

mmnnhhh,

Kamanda MTM, nadhani kina dada wengi hata wa humu JF watakuja wakali hapo kwenye wadada wanajua cycle ya mayai yao. Ni mara ngapi ushasikia tarehe zimebadilika? Nadhani kwenye suala la mwanamke kupata mimba nasi wanaume tunapaswa tuchukue jukumu la lawama. Nawasifu sana wale kina dada ambao at all cost kuepusha hili watalazimisha matumizi Condom.

Mwanaume, iwe ni boyfriend au mume nadhani nasi tunapaswa kujifunza menstruation circle za wenzetu, ...nasi tukajua zipi ni Ovulation days, zipi ni danger days na zipi ni safe days...kumwachia mama/au "mchuchu" jukumu hilo ni sawasawa na kuchezea shilingi chooni. Je, akikutega...?

Suala la mtoto through unplanned pregnancy inaniwia ngumu na uchungu kuita hiyo ni "kumharibia mtu maisha."
Am always anti Abortion. Nipo makini sana linapokuja suala la kufanya mapenzi bila kinga. Inapotokea mwenzangu amepata ujauzito, nauchukulia ujauzito huo +vely, ...ni blessing ya mapenzi yetu. It happenned to me, na nilimu- encourage partner wangu azae, na hivi leo na mtoto mkubwa ninayejivunia.

Unless kuna mtu atakuja na definition nzuri, i.e mwenyewe alijipangia nini mpaka unplanned occurance ndio iwe sababu ya kumlaumu mwingine amemharibia maisha! Kabla ya hapo, ajiulize wakati wa kufanya uchaguzi wa maamuzi yake, alifikiria faida na hasara ya tendo lake, au aliingia kichwa kichwa tu?
Yaani kweli kabisa mwanaume anapaswa kujua mzunguko wa mwanamke wake, kuna wakati sie nasi ni ving'ang'anizi sana mwanaume akiwa strong anakataa kabisa kukutana siku hizo mbaya, nakumbuka mie nilikuwa siwezi kabisa kuhesabu siku zangu hatarishi ila bf wangu ambaye sasa ni mume alikuwa kipaumbele kunihesabia ili nisipae ujauzito, ila kuna siku nang'ang'ania utadhani nini sijui inabidi jamaa ajitahidi mwishowe aruke vihunzi lol mtoto nilikuwa mbishi hatar, sasa hapo ningepata ujauzito ningesema nimeharibiwa maisha kweli
 
Yaani kweli kabisa mwanaume anapaswa kujua mzunguko wa mwanamke wake, kuna wakati sie nasi ni ving'ang'anizi sana mwanaume akiwa strong anakataa kabisa kukutana siku hizo mbaya, nakumbuka mie nilikuwa siwezi kabisa kuhesabu siku zangu hatarishi ila bf wangu ambaye sasa ni mume alikuwa kipaumbele kunihesabia ili nisipae ujauzito, ila kuna siku nang'ang'ania utadhani nini sijui inabidi jamaa ajitahidi mwishowe aruke vihunzi lol mtoto nilikuwa mbishi hatar, sasa hapo ningepata ujauzito ningesema nimeharibiwa maisha kweli

HA HA HA!

...we mwana wee....ulikuwa unang'ang'ania eeh?!

Anyway, kusema ungekuwa "umeharibiwa" wakati mwenyewe ulikuwa unang'ang'ania hiyo ingekuwa unakataa responsibility ung'ang'anizi wako!

Ulikuwa unataka kujiharibia maisha bana, thx God shemeji aliliona hilo na mapema.
 

HA HA HA!

...we mwana wee....ulikuwa unang'ang'ania eeh?!

Anyway, kusema ungekuwa "umeharibiwa" wakati mwenyewe ulikuwa unang'ang'ania hiyo ingekuwa unakataa responsibility ung'ang'anizi wako!

Ulikuwa unataka kujiharibia maisha bana, thx God shemeji aliliona hilo na mapema.
Kuna wanaume wako makini sana aisee
 
Yaani kweli kabisa mwanaume anapaswa kujua mzunguko wa mwanamke wake, kuna wakati sie nasi ni ving'ang'anizi sana mwanaume akiwa strong anakataa kabisa kukutana siku hizo mbaya, nakumbuka mie nilikuwa siwezi kabisa kuhesabu siku zangu hatarishi ila bf wangu ambaye sasa ni mume alikuwa kipaumbele kunihesabia ili nisipae ujauzito, ila kuna siku nang'ang'ania utadhani nini sijui inabidi jamaa ajitahidi mwishowe aruke vihunzi lol mtoto nilikuwa mbishi hatar, sasa hapo ningepata ujauzito ningesema nimeharibiwa maisha kweli
Duh inaonekana ulikuwa mtundu enzi zako
 
.
Kwa uchambuzi huu, naamini tunarudia kule kule kwenye tahadhari za ku bank emotions zote kwa mwenza wako.
Hii inasaidia kuokoa ile 'emotional blackmailing.' Au wenzangu mna mtazamo gani?
Yeah thats the way....., lakini if only it was that easy....., Easier Said than Done...... and the facts remains.....
"Those we Love the Most, Hurt us The Most......"
 
When you lead someone on a path knowing very well the end won‘t be pleasant for them ,you sure like hell deserve credit for it.Watu wengi wanawake kwa wanaume wanapoingia kwenye mahusiano kwa sababu ambazo ni za kibinafsi mf. sex...pesa...sifa na mengineyo hua wanajua vizuri sana kwamba baada ya wao kupata walichotaka na kuridhika lazima watakua wamewakorofisha/wachanganya wale waliotumiwa kutimiza haja na mahitaji yao kwa namna moja ama nyingine.

Mwanaume/mwanamke anaeingia kwenye mahusiano kwa sababu hizi za kibinafsi alafu akamwaminisha mwenzake kwamba anampenda na ana malengo nae mwenzake anajitolea mengi kuhakikisha mahusiano yao yanachanua.Muda...pesa...marafiki au hata ukaribu wa ndugu unaweza kutolewa kafara kwaajili ya hili alafu siku ya siku mtu anakwambia “bwana ehhhh mi nimeshakuchoka“ au “sikupendi tena“ na kama kaamua kukumaliza anakwambia kabisa “nia yangu ilikua kupoteza muda tuna wewe huku nikisubiria wa kunifaa...pole/samahani kwa kukutumia“.Muda ulishaenda...waliokupenda kweli ulishawatolea nje sasa nao hawakuhitaji tena...marafiki ulishapoteza kadhaa kwasababu ya mpenzi....pesa ulishatumia nyingi kumsomesha/kumfungulia biashara then unajulisha/gundua kwamba wote ulikua mchezo tu....KWANINI USIONE KWAMBA UMEHARIBIWA MAISHA???!


Mwanaume au hata mwanamke aliye ndoani anapomwaminisha mwenzake yeye ndo yeye kumbe mkewe/mume yuko shule au kamuacha nyumbani mpaka mwenzie anakolea na kuamini ndoa itakuwepo ni muda tu na mipango...ghafla mimba imenasa alafu anakuja ambiwa “nna mke/mume mimi ujie“....na miaka ilishakata hisia zilishachezewa KWANINI HUYU MTU ASIONE KWAMBA KAHARIBIWA MAISHA in terms of malengo na mipango???!

Mume/mke au mchumba yuko mbali anatuma vijisenti kila mwezi angalau nao siku moja wawe na kwao alafu anarudi kukuta pesa zake zilikua zinamlisha mwanamke/mwanaume mingine au imejengwa akifika anaambiwa hana chake anaingizwa mwingine ndani KWANINI HUYU MTU ASIONE KAHARIBIWA ukizingatia kwamba hata viakiba vyake alivitoa akijua faida ipo?!

Yapo mengi sana yanayompa mtu ruhusa/haki ya kuona ameonewa au hata kuharibiwa malengo na mipango yake aliyojiwekea awali.Ndio kwa kiasi flani hata mkosewa anaweza kua amechangia kwa kutokua wangalifu ila ni wangapi kati yetu wenye bahati ya kufikiria kwa kutumia kichwa badala ya moyo linapokuja swala la kuanguka mapenzini?!Sio wengi....na ndio maana mioyo haiishi kuvunjwa kwahiyo usihukumu kila anaesema hivyo kwamba ni uzembe wake....jua kwanza historia ya aliyomkuta.

Kuhusu wanaoitisha kujiua kwakweli nashukuru sijakutana nao....ila hua najiuliza hua wanapoamua kujia kweli hua wanapania kumkomoa nani haswa maana namjua mzee aliyejiua kwaajili ya mapenzi na mpaka leo hua hata siwezi kuimagine yule mama na wanae watakua wanajiskia vipi kujua yeye ndo msababishi a watoto kujua mama ndie msababishi!

Lizzy! am impressed na analysis yako...!
Kwakweli umeitafsiri 'kuharibiwa maisha' vizuri mpaka nimeshawishika kukubaliana nawe.
Ngoja nitafute loopholes kwenye maelezo yako, usisahau na kajiasili ka ubishi!

 
Hakuna wa kuharibu maisha ya mwenzie, kutokujua kusoma alama za nyakati ndiyo kunakufanya une umepotezewa muda. Hivi kweli kwa karne hii mwanaume au mwanamke anaweza kukupotezea muda? kivipi?

Wanawake bwana tuna matatizo mengi tu, sometimes mwanaume anajitahidii kukuonyesha kwamba hakutaki wewe unajida huoni end of the day unasema umeharibiwa muda wako? Acha ujinga na upumbavu, soma alama za nyakati, ukiona vipi kula kona mapemaaaa, na wanaume vivyo hivyo usipoteze muda kwa mtu asiiyekupenda.

Siyo lazima nikwambie sikutaki, vitendotu vikufanye uwe na uelewa wa ziada. Pole sana wale mnaopoteza mida halafu mnasingizia wenzenu eti wamewapotezea muda.
 
Lizzy! am impressed na analysis yako...!Kwakweli umeitafsiri 'kuharibiwa maisha' vizuri mpaka nimeshawishika kukubaliana nawe.Ngoja nitafute loopholes kwenye maelezo yako, usisahau na kajiasili ka ubishi!
Hahha...Mbu embu weka Umanyema bench leo tu maana ukizipata ntaharakisha kuziziba yani utakesha hapa leo!!!
 
Ukiipata hiyo loophole kwa hili bandiko nitaamini kweli u mmanyema kwa ubishi

LOL! ...huyu Lizzy mjanja sana, amefunika loopholes zote kwa sentensi hii ;

ni wangapi kati yetu wenye bahati ya kufikiria kwa kutumia kichwa badala ya moyo linapokuja swala la kuanguka mapenzini?!Sio wengi....
...in other words, ameturudisha kwenye lawama ile ile ya uchaguzi wa kutumia akili badala ya kuusikiliza moyo wengine husema 'roho,' ---moyo ambao hutoa tahadhari kutokana na past experiences....

Jamani, sote tumezaliwa na sixth sense,...kuna mambo na ishara utaoteshwa ndotoni,...kuna mambo roho itasita,...iwapo uta overrule ishara zote hizi, halafu lawama ukaenda mtupia Lizzy kwa 'kukuhakikishia' mapenzi kumbe ni usanii, itakuwa unakosa kuchukua responsibility ya maamuzi yako!...

hebu chukulia mfano huu;
  • Kipofu haoni, lakini anaiamini fimbo/mbwa wake!
    Guide-Dogs-Help.jpg
    ...
  • Chumbani kwako; funga mapazia, zima taa, kisha jifunge kitambaa machoni kisha utafute mlango utoke...
Tuna macho, pua, mdomo, masikio na viungo kamili lakini tunajisahau jinsi gani vyote hivyo vinavyotambua hisia, itakuwa
hisia ya amani, hatari, tahadhari nk ambavyo ni roho tu yenye uwezo wa kutambua?...Huu ni utambuzi kwenye Spiritual level...!

Listen to your instincts, ingawa si kila tahadhari inaashiria hatari....!
Baada ya 'kutendwa' utamsikia mtu anakumbukia, "tena nilihisi mimi basi tu nikapuuzia...!"
 
Hahha...Mbu embu weka Umanyema bench leo tu maana ukizipata ntaharakisha kuziziba yani utakesha hapa leo!!!

if there comes a day nikamlaumu wife wangu kwamba kaniharibia maisha, basi ntakua nina matatizo makubwa coz i participated in the process

and if she come and say nimemuharibia maisha.... ntakubali coz women are alwayd right!!
 
Mbu sweetie
Nafikiri kuna haja ya watu kuwa na utashi wa kudefine 'mapenzi' ni nini? nini maana ya kupenda/ Tatizo kama hili hutokea pale mtu anapodefine kupenda kuwa ni kumpata mtu ambaye atamkabidhi mwili, moyo, roho na kila kitu chake kwa jina la mapenzi badala ya kuidefine kama kupata mwenzi ambaye ataweza kusaidiana naye kusukuma gurudumu la maisha ya kimapenzi hapa duniani but it doesnt means substituting your very own soul kwa ya mwenzio!! Akikata kamba unajiona huna tena thamani.

Nafikiri tusipende kulalamika ......Umeniharibia maisha.........It is I that I allow that
Remember ....No one screw your life, unless you gave them the screw driver!

Ila wewe unanitisha! what is it??!




umeongea poa MJ1,
Hebu angalia na hii signature yako,
kisha itafakari katika huu mustadha wa ''Umeniharibia maisha''

.............Give more love, than what you receive........................
Mjukuu Mtiifu; 2011


 
Mkuu..mimi nadhani vitu vyote vinatokana na Journey of love”.. unajua wakati mapenzi yanaanza yanakuwa kama asali..yaani watu wanachanganyikiwa na wengine wanakosa hata uwezo wa kufikiria mazuri na mabaya..yaani hasa kina dada wanashindwa kujua kama porojo za wanaume ni zina ukweli au vipi..as a human instinct ..wanaume wamejaliwa uwezo wa kucheza na akili za kina dada hivyo ni sehemu ndogo ya kina dada wanakuwa ngangari na mtego huu.. Sasa, ukiangalia vizuri suala la kuharibiana maisha lipo sana toka kwa kinadada ..kuwaambia kinakaka..kwani kinadada wanapenda kiukweli wakati asilimia kubwa ya wanaume wana .. “artificial feelings ambazo zinasukumwa sana na tamaa za mwili.

Mimi nafikiri..Katika kipindi hiki ambacho mapenzi ni asali hapo ndipo porojo za wanaume zinapom-maliza mwanamke..wakati mwanamme anatunga porojo ili alidhishe tamaa yake ..masikini mdada anapenda kwa ukweli ..na zile sense za kuhisi hatari zinakuwa zimezima..Sasa mwanaume akishashiba ..ile graph ya mapenzi inashuka ghafla..na mwanamke anazinduka toka katika usingizi..huu ni wakati wa panic anaweza fanya lolote..lakini kama akitulia ile panic itaisha.. kwa upande wa mwanaume kwa sababu alikuwa na artificial life’ hatotilia maanani..hivyo basi hata rafiki ya kike akimwambia amemuharibia maisha haitoingia kichwani kwani yeye alikuwa anataka kitu fulani tena kwa muda fulani..yaani hata msichana kama hatajiua hii haitaingia akilini kwa mwanume ..yaani hata msichana hakikuambia maisha yake hayana thamani yaani ni kumpigia mbuzi gitaa ..kwani ni kweli maisha ya msichana yalikuwa hayana thamani toka mwanzo..kilichokuwa na thamani ni mwili..

Lakini, in contrast..kama wote wawili..mlipendana kiukweli..na mkapanga mambo mengi kwa ajili ya baadaye..halafu ikatokea kitu nje ya uwezo wenu kutofanikisha malengo yenu..Kama dini..wazazi..n.k..Hapo wote wawili mtayumba kisaikolojia..na hata kama mtapata wapenzi wapya hapo baadaye..lile jeraha halitofutika kamwe..


..............ubarikiwe kiongozi, umegota kwenye ukweli kabisa.............
good analysis..............
 

Nice Gaga,

hapo kwenye kosa la kujiingiza kwenye mahusiano kwanza, kisha unaanza kumsoma mtu ndio kosa mojawapo!
Lakin i hebu twende mbele tukirudi nyuma.
Mfano; wazee wetu wa miaka ya 60s kurudi nyuma, wengi hawakuwa Boyfriend na Girlfriend kwenye ujana wao. Wengi wao walikutanishwa through mawifi, mashemeji, mashangazi nk...
Wengi wao walioana na kuja fahamiana ndani ya ndoa. Wengi wao wameleana mpaka vifo vinawatenganisha.

Tatizo lipo wapi miaka hii ya leo kiasi kwamba "tunaona kuna umuhimu wa kufahamiana kwanza" kabla ya kuoana?
Je, ni muda gani unahitajika kumfahamu mwenzako ndipo muoane? na kujiridhisha nini mnataka maishani?


Bado nataka kuamini nhili neno 'umeniharibia maisha' halina maana yeyote kwa anayelitamka ila kukupandikizia lawama.

Mbu umenigusa hapo kwenye kijani- nafikiri kwa kuwa zamani kulikuwa hakuna mwingiliano mkubwa kama sasa, wazee wetu walikuwa na kitu tunaita Social intercorse...yaani unakuwa hujaonana na mtarajiwa wako lakini alikuwa tayari anafahamika kiukoo (hao wake/waume watarajiwa walikuwa wanachaguliwa kutoka katika koo zilizokuwa zinafahamika) so hata ukimwuoa unakuwa (na jamii nzima) inaelewa kuwa ana tabia nzuri na hatokusumbua. Sasa hivi tunakutana katika michanganyiko ya kila aina, mwingiliano wa makabila, matabaka kila kitu umekuwa mkubwa sana si rahisi koo kwa koo zikafahamiana kiviiiile, so ni muhimu kuchukua muda kufahamiana na mwenzio
2. Maadili pamoja na 'upofu' wa uhuru na haki za kijinsia uliwafanya mama zetu kuwa na uvumilivu wa hali ya juu. Nimeweka upofu kwenye quotes kwa sababu ni upofu ambao ninaamini kuwa ulikuwa na faida sana katika kudumisha ndoa na maadili ya kipindi kile. Kizazi cha sasa sie kwanza maadili hakuna- tunalelewa na 'ulimwengu' na si jamii au familia kama walivyobahatika wazee wetu. Pili 'akili' ya kuwa mimi ni huru, nina haki sawa na mwenzangu, asinibabaishe .....ndio inayopelekea tuwe makini katika kupata mwenza.

Kuhusu muda gani tutumie, hiyo ni subjective to wahusika kwa sababu mnawezachukua hata miaka, kama kuna mwenye hila anawezaificha hadi mkioana (ingawa mie huwa nasema ukiamua kumchunguza mtu utamjua tu) sema kipindi hicho ambacho wengi wetu tunafikiria ni cha kuchunguana hujisahau na kukifanya ndo kipindi cha kujaribu maisha ya ndoa!! Utakuta wakati wa uchumba mtu anafanya madudu lakini badala ya mwenza kukaa na kuyatafakari yale madudu na kuchukua hatua..yeye analia na kusamehe kwa kujifariji kuwa ....tukiingia ndani atabadilika!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
umeongea poa MJ1,
Hebu angalia na hii signature yako,
kisha itafakari katika huu mustadha wa ''Umeniharibia maisha''

.............Give more love, than what you receive........................
Mjukuu Mtiifu; 2011



bacha kweli kabisa hiyo give more love than what you receive kwa upande mmoja ndo screw diver iwapo unapogive unategemea return sawa! kama ukigive na kutegemea akupende zaidi (asikutende) basi ikiwa kinyume chake ni wazi 'umeniharibia maisha' inaweza ikatokea BUT if you give more than what you expect from him/her hata akikutenda utashukuru kwa kusema I did what I could, haikuwa riziki yangu na pia utaishia kujilaumu tu na si kumlaumu!!
 
Jaman jana tu mwenzenu aliyekuwa mpz wangu wa miaka kansalit na mwaka huu ndio nimefanikiwa fanya nae mapenzi kwani alikuwa bikla na tumefanya tendo hili mara 2 tu chakushangaza mwezi ulio pita alisafili kwenda hom kwao kwan tuna kaa wilaya tofauti baada yakufika huko nikapigiwa sim na aliwekuwa mpz wake wa zaman kabla yangu akiniambia kuwa mpnz wangu ana tembea na rafiki yake na siku ana piga cm aliwakuta mara ya 3 wakitoka guest house mi nikaamua kumuuliza akanijibu ni maneno tu ya watu alafu hapo hapo akampigia sim jama aliyenipa taarifa na kumtukana sana kisha aka mpigia huyo jamaa yake mpya kumuuliza kama ameniambia japo mimi hatufahamiani sasa mtu kama huyu haja nialibia kweli tumekuwa wote kwa miaka 3
 
Jaman jana tu mwenzenu aliyekuwa mpz wangu wa miaka kansalit na mwaka huu ndio nimefanikiwa fanya nae mapenzi kwani alikuwa bikla na tumefanya tendo hili mara 2 tu chakushangaza mwezi ulio pita alisafili kwenda hom kwao kwan tuna kaa wilaya tofauti baada yakufika huko nikapigiwa sim na aliwekuwa mpz wake wa zaman kabla yangu akiniambia kuwa mpnz wangu ana tembea na rafiki yake na siku ana piga cm aliwakuta mara ya 3 wakitoka guest house mi nikaamua kumuuliza akanijibu ni maneno tu ya watu alafu hapo hapo akampigia sim jama aliyenipa taarifa na kumtukana sana kisha aka mpigia huyo jamaa yake mpya kumuuliza kama ameniambia japo mimi hatufahamiani sasa mtu kama huyu haja nialibia kweli tumekuwa wote kwa miaka 3

............Dwork1 sasa hapo umeharibiwa maisha gani?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom