Umeniharibia maisha! ...what? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeniharibia maisha! ...what?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Jun 19, 2011.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]"...ndio! umeniharibia maisha yangu!"


  ...hebu niwaulize nyie wana JF Tusaidiane mawazo, maoni na ushauri kuhusiana na hili.

  Je?

  Nini mtazamo wako mtu anapokwambia umemharibia maisha!
  Tatizo nini?
  kwanini ujifikirie maisha hayana tena thamani bila fulani?

  Tujadili
  kwanini kinyongo, chuki, fitna, wivu, hasira, yakichanganyika na mapenzi yanachangia walio wengi kupoteza matumaini ya maisha.

  Je,
  utauchukuliaje msiba wa aliyekuwa wako, aliyejiua sababu "umemharibia maisha!," au,
  Je,
  unamchukuliaje mwenza wako ambaye anakwambia atajiua kwani maisha yake hayana thamani bila wewe?

  Nini suluhisho kukabiliana na 'mtihani huo'

  [​IMG]...lengo, nia na madhumuni ya topik hii ni kuwapa insight ya mental health
  (kuboresha.)
  Kwa wenye mioyo dhaifu, natanguliza ombi la msamaha kama nitakuwa nimewakwaza kwa njia moja au nyingine.

  Nataka kuamini kwamba kila mmoja wetu amejaaliwa utambuzi na uchaguzi.
  Unapochagua, ina maana pia unajikubalisha matokeo yatayotokana na maamuzi yako.
  Kumtupia mwenzako lawama ya "amekuharibia" ina maana hukuwa makini kwenye utambuzi na uchaguzi wa
  maamuzi yako.

  Ni jinsi gani twaweza boresha utambuzi, uchaguzi na maamuzi yetu
  kwenye maisha na mapenzi kwa ujumla?

  WHAT DO YOU WANT IN LIFE?
   
 2. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkiwa makini kwenye maamuzi yenu katu hili halitakukumba kamwe, hii yote inatokana na maamuzi mabaya uliyofanya awali mpaka kupelekea kupoteza miaka mingi kwa mtu ambaye hata hana nia ku ku spend the rest of his/her life with you,mwisho wa siku anakumwaga na kujiona umeharibiwa maisha kumbe katika uhalisia umejiharibia mwenyewe kwa kutokuwa makini, unajua mpoteza muda utamjua tu mapema, sasa wengine wamekuwa na hope kwamba kuna siku atabadilika, wakati kuna msemo wa kuwa mja haachi asili yake
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  mimi kwa upande wangu hakuna kuharibiwa maisha...

  Labda kupotezewa muda....
  Ntarudi tena, ngoja nitafakari!..
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mbu sweetie
  Nafikiri kuna haja ya watu kuwa na utashi wa kudefine 'mapenzi' ni nini? nini maana ya kupenda/ Tatizo kama hili hutokea pale mtu anapodefine kupenda kuwa ni kumpata mtu ambaye atamkabidhi mwili, moyo, roho na kila kitu chake kwa jina la mapenzi badala ya kuidefine kama kupata mwenzi ambaye ataweza kusaidiana naye kusukuma gurudumu la maisha ya kimapenzi hapa duniani but it doesnt means substituting your very own soul kwa ya mwenzio!! Akikata kamba unajiona huna tena thamani.

  Nafikiri tusipende kulalamika ......Umeniharibia maisha.........It is I that I allow that
  Remember ....No one screw your life, unless you gave them the screw driver!

  Ila wewe unanitisha! what is it??!
   
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Mtazamo wangu mtu akiniambia nimemharibia maisha:Kwa mtu ninayempenda sidhani kama nitamharibia maisha,kama kumharibia maisha anayozungumizia ni kumpotezea malengo kama vile masomo au mimba n.k,ambayo haikutarajiwa basi nitakuwa karibu naye na kumsaidia kadri ya uwezo wangu ila yeye ajue kwamba amechachangia kiasi gani nimemharibia maisha yake?na alikuwa hajui matokeo?kama sio mwelewa basi lawama zake hazisaidii maana yeye pia alichangia ktk kuharibu maisha yake.

  Kwanini nione maisha hayana thamani?:Mimi kama Excellent naamini maisha yangu yana thamani sana na ninajua huyo mtu nilikutana naye tu na kabla yake nilikuwa na mfumo wangu binafsi wa maisha,kwahiyo hakuna kitakachobadilika maana najua maisha nikupambana ktk situation yoyote.

  Kwanini kinyongo,chuki,fitina,wivu,hasira?:ni aliniharibia maisha,nadhani atakapokuwa mbali na mimi nitakuwa nimeutua mzigo wa mwiba na sitakuwa na chuki,fitna wala wivu au hasira.

  Msiba wa mtu uliyemharibia maisha unaumiza sana,kama ulimharibia maisha mfano ulimbaka,H.I.V n.k lazima moyo uumie na daima hilo litakushitaki na hutapata amani wala utulivu wa moyo kwa kumharibia mtu ambaye ni innocent.

  Mwenza wangu akiniambia atajiua maana maisha yake hayana thamani bila mimi:ukweli ni kwamba akinisaliti halafu aniletee hiyo kauli then tutaona ni jinsi gani maisha yake hayana thamani bila mimi.

  Suluhisho kukabiliana na mtihani huo:Suluhisho ni kuwa makini katika uhusiano wa kimapenzi,kufanya ngono salama,kuwa waaminifu,kuaminiana,kuthaminiana na kuboresha mapenzi kila siku.Pale inapotokea mwingine kapata tatizo kwa ajili ya mwingine mchukuliane,kuelewana,kutafuta suluhisho pamoja na siyo kumkimbia mwenza wako wakati wa matatizo.
   
 6. RR

  RR JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Mbu kudos kwa hili...
  Najiuliza mara kwa mara juu ya jambo hili, japo zaidi nawazia upande wa pili zaidi, upande wa mwachaji. ni zipi haki za mtu aliyemchoka mwenza wake?
  kwa kawaida mwanzo wa mapenzi ni mutual, ni jambo la pande mbili, ila kuachana mara nyingi ni jambo la upande mmoja.....mwachaji anaanzisha ama anatafuta sababu za kuachana.
  Kwa nini mwachaji anabebeshawa zigo la lawana za kuacha? kama amechoka uhusiano si yampasa kutoka?
  najua umelenga kumsaidia anayeachwa!

  btw: falsafa yangu ya mapenzi ni kupenda kwa muda uliopo, naamini hakuna binadamu awezae kunifanya nichukie maisha yangu, isipokua mimi mwenyewe.
   
 7. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Duh hiyo bold imenikamata sana, well mi nadhani ni mtu kushindwa kuelewa au kujua anataka mwnza wa aina gani, anajiingiza kwa mtu na kuanza kumsoma wakati anakuwa tayari kwenye mahusiano, cha muhimu ni mtu ku focus, kujua nini ni nini, na kitu gani hakipendi......kuchagua mwenza sio jambo la kukurupuka, wengi wetu tunafanya maamuzi ya haraka na kuja kujuta badae, tunapokatishwa ndio tunaanza kujutia maamuzi yetu, mwisho nahitimisha "hakuna kuharibiwa maisha na mtu ni wewe mwenyewe ndio ulijiharibia" kwa kushindwa kuchagua nazi mpaka ukapat koroma
   
 8. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Nadhan hakuna kitu/kitendo kinachoitwa kuharibu maisha, wanaosema wameharibiwa maisha HAWAJUI MAANA YA MAISHA!..
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nadhani ni aina flan ya uselfish.... Maisha mmeishi pamoja iweje ulalamike yako ndo yameharibiwa? Na unapotishia kujiua lengo lako ni nini?


  I have bn there and believe me usipokuwa makini utajikuta unastick kwa mtu si kwa kuwa unampenda la hasha ni kwa kuwa unaogopa kumwacha kwani atajiua!
   
 10. CPU

  CPU JF Gold Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MJ1 umeelezea vizuri sana.
  Kwa definition hii utaona kwamba hawa watu WANAJIHARIBIA MAISHA wenyewe.
  Na unapompa ushauri kabla ya tatizo, unaweza kuonekana unataka kumbomoa
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  fab Shantel!

  hapo kwenye ipo siku atabadilika hapo!....'hope over intelligence and experience!'
  Ipi ni njia sahihi kuweza kubalance hiyo equation?...

  Mapenzi ni nini?

  Tafsiri yangu; Mapenzi ni pamoja na mwenza wako anavyoweza kukufanya ujiskie (unapendwa.)
  La msingi, unapopendwa nawe unawajibu wa kumaintain ama kuzidisha yaliyokufanya upendwe.

  Jiulize, Mpenzi wako alikupendea nini awali?
  Don't take love for Granted.
   
 12. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Easier said than...
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mbu unajua unapkutana na mtu kama huyu na mawiliWapo wale wanaotikisa kiberiti na wale wanamaanisha kweli. Wanaotikisa kiberiti ndo hao wanaorusha matangazo hewani kuwa watajiua wakati wanaomaanisha anaweza asilipaishe ila akakupa signal. So ni muhimu kuwa makini kabla ya kuamua! Wale wanaotikisa dawa yao ni kuwapuuza tu kama husikii vitisho vyao but unachukua taadhari.
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...how relieveing having a soulmate like you!

  Mwj1,...life experience imeni shape kwa mengi, na miongoni mwa mawimbi na dhoruba nilizopitia ni pamoja na
  mwenza ambaye baada ya makasheshe, na mimi kusitisha mahusiano nae..aliwahi nitamkia 'najiua!, maisha hayana thamani tena!'...I was shocked!

  Nilijifikiria hiyo itakuwa sababu ya kuisaidia polisi, nilijifikiria hiyo itakuwa sababu ya mimi kunyoshewa vidole na ndugu, jamaa na marafiki kwamba nilisababisha kifo cha fulani,...nikarudisha moyo nyuma...nikasamehe,...nikajiona mie ndio mkosa kwani nimekosa roho ya utu. Nikawa nami ni sehemu ya tatizo lililochangia yeye kunikosea.

  Tangia hapo, kila matatizo yalipokuwa yanatokea nami kufikiria kuhitimisha mahusiano, vitisho viliendelea hivyo hivyo,...Nikaendelea kuwa 'prisoner' wa maamuzi yangu.

  Lakini, ipo siku nikajisemea, ipo siku alimeza panadol...hakufa, ipo siku alisaga chupa hakunywa,...ipo siku alitaka jitupa wakati naendesha gari...je? ni kweli ana nia ya kujidhuru au nami ananiweka majaribuni?

  It's an emotional blackmailing!
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duh we bwana nafikiria kuku'rudishia' proposal yako! We have too many things in common loh hahhh

  Yes kwa hapo ilikuwa emotional blackmailing... Nimejifunza what RR hav just put down, enjoy the love while it last....if it last forever I concider myself blessed and if it last shortly I consider my self lucky. Life has to go on and no one is responsible for your life, only you.
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Excellent my sisy.....No one screw your life, unless you gave them the screw driver!

  Ila kuna circumstance fulani fulani ambazo watu hustahili hizo lawama za umeniharibia maisha yangu...mfano,ndo kama Excellent alivyosema kumbaka mtu kama mtoto wa shule ukamuachisha masomo kwa mimba au Ukimwi,mwanandoa kutoka nje ya ndoa na kuleta magonjwa au matatizo mengine,kweli kwa wanakuwa wameharibu maisha ya wenzao.....mara nyingi kwenye mahusiano hili linamaanisha,mtu kapotezewa muda au expectation alizokuwa nazo kwa partner wake hazijafikiwa au kama kuepuka kuwa responsible na maamuzi yake kwa hiyo anaishia kulaumu na kutoa vitisho.
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mkuu una maanisha anaeacha asilaumiwe? lawama lazima ziwepo coz kuna upande wa pili ambao umeathirika na kitendo chako, na kila mtu ana haki ya kujisikia au kufanya afanyalo ili ajisikia au ujumbe ukufikie kwamba kaumia kiasi gani, then utampa reason kazi inabaki kwake, kwa mwenye upeo atafurahi kwamba umemwambia umemchoka kwa sasa, ila king'ang'anizi ndio atakuja na single ya kujiua
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  Mkuu RR!

  Nice to see you back for good, ama? haha! well,....lengo ni kubadilishana mawazo, iwapo muachaji na muachwaji atafaidika ndio furaha yangu.

  Kabla ya kuzungumzia muachaji na muachwaji, nigusie hili pia linahusu wale waliokataliwa.
  Kuna watu iwapo waliambiwa, "haiwezekani mimi kuwa nawe!"...hununa na kuanisha cold wars, i.e Chuki, fitna, majungu, etc...yote ni katika kumfanya mhusika ajiskie kana kwamba ametenda dhambi kubwa, au dhambi mbaya sana!

  Kupenda ni jambo la hiari, huwezi mtu kulazimisha kupendwa...ama? ni mapenzi gani hayo ya shingo Upande?
  Unataka na kumlazimisha mhusika eti ajaribu aone kama nae atakupenda, Mapenzi yanajaribiwa?....
  Emotional Blackmailing haisaidii lolote zaidi ya kuvunja urafiki, undugu na mahusiano kuanzia makazini, majumbani na mitaani...

  Kuna umuhimu wa muachwaji kujifunza kupokea maamuzi magumu hata kama hayapendezi. Hiyo ndio maturity.
  Kuomba kuachwa taratibu ili isiume au kutishia kujidhuru naamini kabisa ni ukosefu wa umakini katika maamuzi.
  Uingereza na nchi zilizoendelea wana mental Health Charity kuwasaidia watu wanaokumbwa na msongo huo wa mawazo.

  ...Huku dunia ya tatu, ni wakati na jinsi gani twaweza jifunza maamuzi mazuri?
   
 19. CPU

  CPU JF Gold Member

  #19
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu
  Mimi hii imenitokea MARA 2 recently
  Kwanza wanaanza kujiapiza NAFUTA NAMBA ZAKO ZOTE
  Then baadae anakuja na NAONA BORA NIFE TU, SIWEZI KUISHI BILA WEWE CPU, UKISIKIA NIMEKUFA USISHANGAE, NIMESHAKUAGA RASMI.
  Finally inakuja "Kumbe kweli umeshani-delete kwenye mind yako"
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hahahh CPU duh kweli limekutokea.... Ila reminder si kina dada tu ambao hukimbilia huko bali kuna wakaka pia haah
   
Loading...