Umemfumania, sasa unasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umemfumania, sasa unasemaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 10, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Jana niliweka mada hapa kuhusu fumanizi au kutoka nje ya ndoa. Na leo ningependa kuzungumzia jambo hilo.
  Hebu fikiria kuwa umedhibitisha kwamba mwenzako sio mwaminifu, yaani ametoka au anatoka nje ya ndoa, utafanyaje? Je, utaondoka, utalipa kisasi na wewe, au utachukua hatua gani?

  Kuna mambo ambayo ukiona kwamba yamejitokeza, baada ya fumanizi, unapaswa kujua nafasi yako kwenye uhusiano wako. Kutokea hapo ndipo unapoweza kuamua kama uondoke au hapana.

  Kwanza, hebu jikague, Je, umevunjika moyo kupita kiasi? Unadhani itakuwa bora kuvumilia? Unadhani kumvaa na kumwambia umechoka na unataka kuondoka itakuwa ni kujiongezea mfadhaiko zaidi?

  Pili, unadhani utaendelea kubaki katika ndoa kwa sababu za kidini? Unataka kufanya kitu kilicho sahihi daima? Uko tayari kuendelea kudhalilika na kuwa hatarini kwa sababu ya imani yako ya kukukataza kuvunja ndoa? Je ni kwa imani yako au wasiwasi wako umelazimika kubaki? Nijuavyo mimi, kosa la kutoka nje halitetewi na dini yoyote linapokuja swala la kuvunja ndoa.

  Tatu, unadhani unalazimika kubaki kwa usalama wa watoto? Unadhani ni wewe pekee unawajali watoto na mwenzio hawajali? Inawezekana na mzazi mwenzio pia ni mpenda watoto? Unadhani kuachana kutawaletea watoto matatizo zaidi? Una wasiwasi na maisha ya watoto kama utaamua kuondoka? Kumbuka kuishi kwenye vurugu za ndoa huwavuruga watoto kuliko watoto kuishi na baba au mama wa kambo mwenye upendo.

  Nne, unadhani hakuna uwezekano kabisa katika ndoa hii? Umekwama? Umenata kama ulimbona huwezi kuondoka? Unaweza kufikia muafaka kwamba umejitahidi kwa uwezo wako wote kumrekebisha mwenzio lakini wapi. Hivyo umeamua kuishi hivyo hivyo?

  Tano, unadhani huwezi kuondoka? Kuna kitu unachodhani kinakuletea ugumu wa kuanza safari? Kuanza maisha mapya? Huna uwezo wa kujiamulia? Kumbuka kwamba, huenda ni mazoea tu yanayokuzuia au utegemezi wa kipato. Lakini, kila binadamu ameletwa duniani ili asimame kama yeye, na siyo kama kipande cha mwenzake.

  Sita, unataka kumlinda? Kuna kitu kibaya unachodhani kinaweza kutokea kama utaamua kuondoka? Ataweza kuishi peke yake? Kama utaondoka unadhani itakuwa ni njia ya kumpeleka shimoni zaidi? Umeamua kubaki ukijua kwamba baada ya muda tatizo lenu linaweza kutatuliwa? Inawezekana likatatuliwa, lakini inawezekana wewe ni mtu wa kuumia kwa sababu ya wengine bila sababu.

  Saba, unaendelea kuishi naye kwa sababu kuna hatari kumwambia unataka kuondoka? Unadhani atalipuka kwa hasira utakapomwambia unataka kuondoka? Una wasiwasi kwamba una haki ya kuamua kuhusu maisha yako na kuna sheria zinazokulinda.

  Je, hujafikiria namna ya kuanza maisha mapya? Hii ni tofauti na hofu ya kuanza maisha mapya. Labda maisha yako, yake na ya watoto yameambatanishwa kupita kiasi, hivyo inakuwia vigumu kujinasua? Pia kuambatanishwa huku labda ndiko kunakokufanya hata usiwe na chembe ya wazo la kutaka kuondoka? Umewahi kufikiria kuhusu utashi wako, ujuzi wako, ndoto zako, matumaini yako na mustakabali wa maisha yako bila yeye, au bila watoto?

  Chukua muda wa kutosha kufikiri kwa makini na uyajibu maswali hayo yote ukishayajibu utakuta unatoa uamuzi sahihi utakaokupeleka kwenye maisha uyatakayo. Kumbuka, kila binadamu hukosea na kusamehe kwa aliyekosewa. Lakini kusamehe hakuna maana ya kuendelea kuumia au kuumizwa na uliyemsamehe.

   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  summarise maelezo mkuu.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,056
  Likes Received: 6,504
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi bila shaka umefumaniwa tena na hg, sasa kazi kwako mwangukie mkeo, akikubali atakusamehe, la sivyo kimekula kwako.
   
 4. K

  Karry JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  pole unaoneka yamekukuta
   
 5. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kama umefumania hiyo ni straight red card no diskasheni mkuu
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Umeongea kwa kina............nitarudi kuipitia upya!
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mambo magumu sana haya na reaction ya aliyefumania huwa haitabiriki,kikukweli mpaka yakukute ndo utajua ufanye nini.ila kimsingi kwa maisha ya leo na maradhi haya mkifumaniana mi naona bora muachane tu.
   
 8. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, umeandika gazeti mkuu, kwa sasa hivi nimeshindwa kumaliza hivyo nitarudi baadaye.
   
 9. v

  valid statement JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  kufumania usifanye mchezo mdau...inaumaaaa!!
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nini vileeee
   
 11. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  ivi hii itahusika kwa marafiki pia au ni kwa wanandoa tu?
   
Loading...