kwanza wanajichanganya waziri mkuu anasema kodi ya simu ni umeme vijijini, waziri kwenye bajet amesema kodi mpya kwenye mafuta ni ajili ya umeme vijijini
Hakuna kilichoharibika, kubwa umeme ufike kijijini kwetu.
kwanza wanajichanganya waziri mkuu anasema kodi ya simu ni umeme vijijini, waziri kwenye bajet amesema kodi mpya kwenye mafuta ni ajili ya umeme vijijini
una maana umeme utawaletea huduma za afya, maji, bara bara
Hizo zote siasa, Tatizo la midanganyika miradi au sera zinapoanzishwa serikali hitangaza sana lakini hutasikia taarifa za hatua za utekelezaji wake, aidha kama imefanikiwa au imefeli. Tena kama imefeli ndo kimya kabisaaa! Maisha bora kwa kila mtanzania iko wapi? Kilimo kwanza imefanikiwa? vipi kuhusu MKUKUTA, MKURABITA etc? Ok, umeme vijijini, pamoja na bei kuwa juu je mijini umetoshereza na watu wako happy?
Chukua chako mapema!
Dah! Sijuhi Akili ya wapi hii?
Ni sawa na Kujenga Viwanja vya ndege wakati mwenye ndege ni raisi tu na Huko kwenye viwanja hakuna hata Barabara.
Pia Kumbuka una peleka umeme wakati watu hata Maji safi/Machafu hakuna, Zahanati hakuna, Shule hakuna kama ipo ni gofu tu, hakuna walimu wala wanafunzi hawahudhurii.
][/B]Hapo futuhi wamechemka! Wao wamelenga karibu wakati serikali inalenga mbali miaka 10 na kuendelea. Sasa hivi vijijini kuna mabadiliko makubwa sana kuhusu makazi, jaribu kulinganisha kijijini kwenu miaka 10 iliyopita uone tofauti iliyopo na sasa. Serikali inafanya vizuri sana katika hili, siyo halali kubweteka eti mpaka makazi yawe bora ndo tuwapelekee umeme!! GO GO GO Muhongo. Jamani wakati mwingine mnyonge tumnyonge lakini haki yake tumpe! Umeme ni kichocheo kingine kinachowafanya raia kubadili makazi yao, chunguzeni kote kulikowekwa umeme vijijini mwone jinsi raia wanavyoshughulika! Sikutegemea kama usukumani nao wangezinduka kuhusu ujenzi wa nyumba bora!
Futuhi hapa wamejaribu kutuonesha picha kubwa ya nani anapanga vipaumbele vya mahali husika, ni wanannchi wenyewe au wasomi wachache wanaokutana mahotelini na kuamua kuhusu maeneo wanayoyajulia kwenye 'ripoti'. Vipo vijiji vingi tu ambavyo umeme si hitaji lao la msingi, kwao maji ndo hitaji la msingi, hawa hawahitaji umeme, wanahitaji MAJI safi na salama.
Hakuna dhambi mbaya kama ya kudhani unajua nataka nini kabla ya kuniuliza, hivi dhana ya kupeleka maamuzi kwa wananchi iko wapi linapokuja suala la kuamua 'tunataka nini kwanza au kwa wakati mmoja? Hata kama serikali ina 'nia' kweli ni wakati wa kukaa na wananchi na kuuliza vipaumbele vinginevyo ile sense ya ownership itapotea na hujuma ya huo umeme itakuwa ni kubwa kuliko.
Wamechekesha, ndiyo, ujumbe ufike na huu si wakati wa kunipangia nataka nini bila kuniuliza, BTW misingi ya utawala bora na ugatuzi wa madaraka unasema kuhusu ushiriki wa wananchi na hata wachache lazima haki zao ziheshimike (politics of limited objectives)
Mbna bar za makuti zina umeme
Serikali iko sahihi kupeleka umeme vijijini. Suala la makazi litakuwa motivated na maendeleo makubwa kama haya ya umeme. Na huwezi kusubiri raia eti wajenge nyumba ndiyo upeleke umeme, hiyo itakuwa ni akili ndogo. Umeme vijijini unafika nimeshuhudia sehemu kama Mdabulo, Rungemba, Ulete, umeme unapelekwa kuna maeneo kama Malangali kazi imeanza. So, nadhani serikali imedhamiria. Go go go Serikali. Wasioitakia mema nchi hii na wapinzani wa Serikali ndiyo wanapinga mkakati huu.
Tengua kauli!Mbna bar za makuti zina umeme
Habari za Isimikinyi? Hapo malangali mbona ni candidate wazuri tu wa umeme lakini can we afford?Issue ya maendeleo ni pana sana. Ukitaka wananchi wakupe wanayoyahitaji utakesha. Mwingine atakwambia barabara mwingine ukumbi wa dsco mwingine viwanja. Kwa hiyo lazima itazame ni vp vya msingi na vitstimulate maendeleo. Tatizo lenu nyie mnaokaa kwenye umeme na wapinzani ndiyo mnaopinga hii issue ya umeme. Tuoneeni huruma tumechoka kukaa gizani. Tena ngoja nijenge kanyumba ka bati kwa sbb umeme unakuja huku Malangali.
Hapo futuhi wamechemka! Wao wamelenga karibu wakati serikali inalenga mbali miaka 10 na kuendelea. Sasa hivi vijijini kuna mabadiliko makubwa sana kuhusu makazi, jaribu kulinganisha kijijini kwenu miaka 10 iliyopita uone tofauti iliyopo na sasa. Serikali inafanya vizuri sana katika hili, siyo halali kubweteka eti mpaka makazi yawe bora ndo tuwapelekee umeme!! GO GO GO Muhongo. Jamani wakati mwingine mnyonge tumnyonge lakini haki yake tumpe! Umeme ni kichocheo kingine kinachowafanya raia kubadili makazi yao, chunguzeni kote kulikowekwa umeme vijijini mwone jinsi raia wanavyoshughulika! Sikutegemea kama usukumani nao wangezinduka kuhusu ujenzi wa nyumba bora!
sisi tunaotembea vijijini tumeona haswa mikoa ya kusini umeme umepita lakini wananchi hawawezi kuweka.Serikali ifanye kazi moja ya kuongeza kipato cha kaya na ukitaka hvyo ni kuongeza kodi kwa matajiri na kuratibu masoko ya mazao vizuri kwa kutafuta soko la uhakika na kuboresha miundombinu vijijini. Kuongeza kodi nyingi kwa daraja la chini litaathiri daraja hili kujikwamua na kuingia daraja la kati na hili litafanya malengo ya millenia kutofikiwa. Siku zote purchasing power ikiwa kubwa kwenye nchi , uchumi unakuwa mzuri hata foreign market ikitetereka haitaathiri sana uchumi wa nchi. Mfano wa CHINA domestic market si nzuri kwa kuwa haikuwezesha pato la kaya vizuri na hii walifanya kwa kutoongeza mshahara kwa wafanyakazi wake na riba ya kutunza fedha benki kuwa ndogo na imewaletea shida sasa kwa kuwa foreign market imeyumba sasa. Tanzania inataka kuharibu domestic market kwa kutoza kodi nyingi kwa mlalahoi hvyo kutoweza kupiga hatua kwenda daraja la kati , maana daraja la kati ndilo lenye purchasing power kubwa
Serikali iko sahihi kupeleka umeme vijijini. Suala la makazi litakuwa motivated na maendeleo makubwa kama haya ya umeme. Na huwezi kusubiri raia eti wajenge nyumba ndiyo upeleke umeme, hiyo itakuwa ni akili ndogo. Umeme vijijini unafika nimeshuhudia sehemu kama Mdabulo, Rungemba, Ulete, umeme unapelekwa kuna maeneo kama Malangali kazi imeanza. So, nadhani serikali imedhamiria. Go go go Serikali. Wasioitakia mema nchi hii na wapinzani wa Serikali ndiyo wanapinga mkakati huu.
Kwa tozo la 1000 kila line ya simu kwa mwezi na huu ni mwezi wa saba ndo kwanza tarehe moja mwezi huu ule mswada umepita? Na umefika kijijini kwenu muda huu? Sidhani na si kutendwa na serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi ya Mdomoni!!!!!Kwetu ushaletwa mkuu. Hamna siasa
Mbna bar za makuti zina umeme
Hakuna umeme vijijini hapo suala ni kwamba ccm wanatafuta pesa za uchaguzi 2015 maana vyanzo vingine vinaonekana kustukiwa na raia. walianza na kutenga fedha nyingi za ukaguzi wa miradi ya maendeleo wakati kila mradi unaosimamiwa na serikali una bajeti yake ya ukaguzi. Mnyika akawastukia akawaumbua mchana kweupe sasa wakaona watoke kwa namna hii ya kutoza kodi kwenye simcard!!!!!!! ila naona nayo watu wameanza kuitolea macho sasa sijui itakuwaje??!!!
Habari wadau,
Mdau nilikuwa nnaangalia kipindi cha futuhi, kinachorushwa na Star Tv , wamezungumzia swala la umeme vijijini ingawa ni kwa vichekesho lakini nnamimi ujumbe umefika. Wamesema umeme vijijini, nyumba zenyewe za nyasi je watakuwa na sifa za kuwekewa umeme?
Wameongezea kuwa ni bora wapewe kwanza mifuko ya sementi ili waboreshe kwanza makazi yao.
wadau hapa kuna mambo yakujadili
1) makazi duni
2) kumudu gharama za umeme. e.t.c
Je wakazi wa vijijini wameandaliwa kupokea huo umeme ambao serikali inaupigia chapuo