Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,430
UMEICHOKA NDOA YAKO?
Asubuhi nilituma post hapa kuhusu ndoa, natamani tubadilishe mitazamo tuliyonayo wengi kuhusu ndoa. Watu wanalalamika kuwa ndoa ni ngumu, siwezi kupingana na hili, kwa sababu hakujawahi kutokea ndoa rahisi duniani (usinibishie).
Unaolewa na mtu ambaye amelelewa na kukuzwa kwenye mazingira tofauti na wewe, mafunzo na taratibu za maisha kwenye jamii au familia yao ni mbingu na ardhi ukilinganisha na za kwenu. Urahisi utatoka wapi? Hata Adamu hakukua na Eva, hakujua Eva amekuja saa ngapi duniani kama ambavyo Eva hakujua Adamu alikuja lini duniani.
‪#‎KIFUPI‬ unaoa au kuolewa na mtu usiyemjua, usijidanganye kuwa mlisoma wote, mlicheza wote mtaani kwenu au mliimba wote kwaya. Humjui! Unamfahamu kama mwanakwaya, class mate wako lakini humjui kama mume/mke, maana hajawahi kuwa mumeo au mkeo, urahisi unatoka wapi?
‪#‎TUNAPOKOSEA‬ narudia nilichosema asubuhi, mwanzilishi wa ndoa ni Mungu, ndoa ni taasisi, aliyeianzisha anajua ni namna gani anataka iwe, ni bahati mbaya ndoa zetu nyingi zina mume, mke na watoto lakini hazina Mungu!
Umeichoka ndoa? Imekuumiza? Imekufanya upoteze matumaini? Nitafute!