Umefeli somo la michezo physics ,chemistry utaziweza??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umefeli somo la michezo physics ,chemistry utaziweza???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Aug 7, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,153
  Likes Received: 5,587
  Trophy Points: 280
  Big up brthers and sisters

  Naona mko safi Jumapili natumaini itakwenda shwari, Ni vizuri unapoanza kufikiria ndoa ujue kuna majukumu kadhaa kama mwanandoa ujue jinsi gani ya kuyashinda. Husika na kichwa cha habari hapo juu kuna watu wanapata bahati ya kupata kazi nzuri wakiwa kwenye nyumba ya baba na mama lakini ukwel ukiona familia inavyoishi unatamani kulia na kumuuliza mungu kwa nini huyu bwana usimpe uhamisho tu ikajulikana wazazi wako wenyewe.

  Kuna mifano mingi tu ndugu zanguni imesomwa hapa kuna waliokuja toka UK na kuanza kumwaga pesa kwa mamiss bila kusoma nyakati leo wanalia na ukiangalia familia zao zinavyoishi yaani wazazi wao ni aibu ndugu yangu. Tenda kila kitu lakini ogopa lawama za wazazi
  hilo ni somo la michezo kwa waliosoma enzi hizo.

  Sasa basi ukiwa kama unafanya kazi nzuri hulipi kodi wewe ni kujazia chakula wazazi wapike wale. Hembu jiulize kama hata kununua mchele maharage, njegere, choroko kwako ni shida, je ukimweka mtoto wa mtu asiyejua maana ya kulala na uji kama ulivyokuwa ukinywa pombe na kuku na wazazi wakijipikia uji?

  Iwapo umeshindwa kulipa kodi nyumba na bado ukashindwa kuwanunulia wazazi wako hata vijinguo unahisi huk unapoenda kulipa kodi utaweza kumnunulia hata malapa ya yebo yebo mkeo kweli?

  Sisemi umwache hapana nakufundisha ujue jinsi gan ukiwa kwenu ni vyema ukajifunza kutunza familia na hayo hayo maisha ndio yanarudi kwenye nyumba ya ndoa unachofanya ni kuongezea special kwa mkeo. Nahisi si vyema kuwa na familia inayomkaribisha shetani, so ni wakati muhimu sana kuwa makin.

  Hii ni mitihan ya dunia unapopata nafasi ya kufanya kazi ukiwa kwenu jifunze kushiriki kwenye matunzo hata kama dadako yuko una mama yuko usaidie, haijalishi wewe unakula pale jitoe na ukiwa mgumu katika hili nakuhakiikishia utakuwa msukule wa ndoa yako na hapo ndio maana wengi wanawake wanaanza kwenda nyumbani kwa wazazi kumbe wamejificha na minjemba pale Kigilagila

  Haya nakutakia akili njema uishi kwa akili kwenye maisha yako ya ndoa.
  Kila la kheri
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante sana kwa busara zako
   
Loading...