ha ha ha, pole
i can imagine...
Sijui nilie sasa hivi for u
ila kwa sasa hata nikisutwa siogopi
Hahahaha. .Niliwahi kusutwa pia humu jf na jamaa mmoja alikuwa anajiita wa kusoma! Baada ya kupigwa ban akaja na jina la complicator nikamgundua! Heheh nilivyomuweka hewani alinisuta nikashindwa kuthibitisha kuwa ni yeye!
Lol! Ushakuwa sugu wa kusutwa eeh!
Hujasutwa na matarumbeta na maandazi ya iliki wewe, utacheza mirindimo yoote uimalize.
Mie I can keep a secret like a witch! Kuna siri ya rafiki yangu aliniambia like 15 yrs ago, anashangaa hadi leo hajawahi isikia kwa mtu manake it was dirty like dirtttyyy!
Ila a few times nilizofanya umbea ambao haukuwa serious sijawahi kusutwa. Na hii binduki, ntaua mtu!
HahahahahahaKuna dada mmoja nilisoma nae form1 to 6.
Huyo alikua mbea jamani.
Wakati tupo o level Mkiongea tu limefika,akiitwa kusutwa anakimbilia kwa walimu. Mkianza kuhojiwa anaanika yote...anamalizia
'mi nilimwambia mwenyewe ili aache watu wasimseme'
kimbembe A'level mazingira ya kwenda kushtaki kwa ticha hayapo,basi kwenye kusutwa anawataja wote na mliyoyaongea,mnabaki wadogo... Badae anakufata kukuuliza kama umekasirika anakuomba msamaha.
Ila mkiteta lazima atafikisha tu.
Kuficha siri wakati mwingi ni bora kuliko umbea, ila je ukificha siri ambayo inaweza ikamtoa ama kumkwepesha mtu mwingine na matatizo je? Mi kuna moja naifikiria hapa sijui nilifanya sahihi kunyamaza au la? Mhusika anisamehe bure.
@Dearest hehehe una bahati wewe.
Hahahaha yani mpaka mimi sikujua? Ngoja nifanye uchunguzi nikiupata kama ulinifukuzia kandege jiandae kufanyiwa sherehe. . . lolz!!Kuna namna ya kum-alert mtu kama siri yenyewe yaweza kumuondolea mtu matatizo bila hata ya yeye mwenyewe kujua. Mbona hata wewe nilishawahi kukuambia 'umbea' na haukustukia na sikusutwa hehehe (usije ukaniletea tarumbeta, ntakuruka futi 100!!)
But ukimuambia mtu kwa njia ya ushabiki na kutaja majina ya watu nadhani inakuwa tatizo. Na especially kama mtu anafanya backbiting... Yaami wakati anasikia anashadadaia afu anaenda kwa muhusika anashadadaia! If need be, ukisikia kuhusu mtu na unadhani itamsaidia ku-discuss nae hiyo issue unam-probe akifunguka unatoa opinion yako. Akigoma unamuacha, kwani wewe mama yake?
Lol! Ushakuwa sugu wa kusutwa eeh!
Hujasutwa na matarumbeta na maandazi ya iliki wewe, utacheza mirindimo yoote uimalize.
Mie I can keep a secret like a witch! Kuna siri ya rafiki yangu aliniambia like 15 yrs ago, anashangaa hadi leo hajawahi isikia kwa mtu manake it was dirty like dirtttyyy!
Ila a few times nilizofanya umbea ambao haukuwa serious sijawahi kusutwa. Na hii binduki, ntaua mtu!
POPOBAWA anapita anaelekea jukwaa la dini.
Hahahaha ulikua mkorofi/mtundu/unajiamini wewe. . .Nliwahi kusutwa na mwalimu wa kiume nikiwa form 3,kisa kuna dada mmoja alikuwa anasemwa eti anatembea na huyu mwalimu wa geography. huyu mwalimu alikuwa anampendelea dada kwa kumpatia marks nzuri. sasa darasani kwetu kila mtu alikuwa anaongea ila kwa kujificha ficha. mimi nilijifanya mbabe nikawa naongea kwa sauti tena kwa mafumbo mle darasani , si yule dada akaniskia bwana na akaniquote maneno yangu.....akaenda kushitaki kwa yule mwalimu wa geography, mwalimu akaniita kuniuliza na kunitaka niseme yale yooote niliyoyasema class na niliyatoa wapi, mie nilikataa kata kata nikamwambia amuite aliyemwambia alate ushahidi....ticha alishindwa akaniacha ila ndo akawa ananikomoa kwenye geography....from there mie na geography ikawa kama mafuta na maziwa.....