Umbea. . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,695
58,770
Ushawahi kuwa mmbea? Ulishasutwa?

Mi niliwahi zamani kidogo wakati nikiwa darasa la nne nadhani, na nilivunja urafiki na my 'then' best friend kwa huo umbea na hapo hapo nikakoma.

Kulikua na msichana mmoja darasani kwetu, mkubwa kuliko wasichana wote. Hata kukua(vunja ungo) alikua wa kwanza, yani darasa la nne tayari alikua ameshalipuka kila kona ya mwili, alafu alikua anapenda kweli kukunja sketi yake ya shule iwe fupi na kufunguo vifungo vya shati wakati wengine tulikua tunafunga mpaka karibu na shingoni. Zaidi ya hapo alikua hamaind kabisa kushikwa shikwa na wavulana na wenyewe wakawa wanajua na walikua wanamshika haswa.

Sasa bwana huyo msichana alikua na mdogo wake mdogo sana, maneno yakazuka kwamba yule sio mdogo wake ni mtoto wake kutokana na story zilizokua zinasikika kuhusu yeye na wanaume. Mimi baada ya kuambiwa na msichana mmoja jirani yangu kesho yake wakati wa kwenda shule nikamnong'oneza rafiki yangu. Siku moja hata sikumbuki kilitokea nini si akaenda kumwambia mhusika na wasichana wengine bana. Loh likanijia jopo bana. Basi kunipiga hawawezi, kwenda kushtaki kwa walimu hawawezi wakaishia kuongea tu. Baadae nikawaelezea kwamba mi niliambiwa na sikuongeza chochote, ila nikamwambia huyo msichana mwenyewe samahani kwa kumwambia mtu mwingine basi yakaisha.

Ila kwanzia siku hiyo yule rafiki yangu ubesti uliisha tukawa tunaongea kawaida tu. Since then maneno ya "nimesikia, akasema" hua nayaogopa kweli. Kusutwa noma!!!
 
ha ha ha ha
uzuri utotoni nilikuwa mwoga sana

nimevunja ungo wa kuongea baada ya kuanza kazi
ilibidi niwehuke kudeal na clients.
 
Ha ha haaa...Lizzy...nakusoma nakusoma...kumbe umeanza mdomo zamanieeeee

HA nilijifunza aiseee. Matokeo yake niliambiwa kitu kikubwa sana tena kuhusu watu wazima ndugu zangu nikapiga kimya mpaka walipojuana wenyewe na bado mpaka leo hawajui nilijua kabla yao. Bora kuficha siri kuliko kishushuliwa. . . ni AIBU!!
 
Loh,kweli mlikua watoto maana...!
Mi nilisutwa sekondari tena huo umbea uliniangukia tu jamani.
Kuna dada alikua anahisiwa mjamzito mi sikujua. Watu wakateta wakakatisha ghafla mi sikumjua anayesemwa kumbe anakuja na kaskia.
Badae tupo wawili akaniuliza mi nikasimulia kilichosemwa bila kujua namsema yeye.
Loh,kutoka pale akaenda kusema niliyomwambia,wakaja nikawekwa kati,najitetea watu wanazidisha kelele tu. Nikalia....lol
na nikaonekana mbea hasa
 
Heheh pole lizzy! Mie nilishawa wahi kusutwa na mama yangu tu ktk maisha kwa kumuongopea kwa baba! Ila tangu hapo alinifunda kutokutumia maneno alisema, anasema, atasema! Ila nimesuta wengi!
 
Da Prety ivi umbea umeshaacha au bado unaendelea nao maana mkao wako huo...umbea! umbea tu!
 
ha ha ha, pole
i can imagine...
Sijui nilie sasa hivi for u

ila kwa sasa hata nikisutwa siogopi
Loh,kweli mlikua watoto maana...!
Mi nilisutwa sekondari tena huo umbea uliniangukia tu jamani.
Kuna dada alikua anahisiwa mjamzito mi sikujua. Watu wakateta wakakatisha ghafla mi sikumjua anayesemwa kumbe anakuja na kaskia.
Badae tupo wawili akaniuliza mi nikasimulia kilichosemwa bila kujua namsema yeye.
Loh,kutoka pale akaenda kusema niliyomwambia,wakaja nikawekwa kati,najitetea watu wanazidisha kelele tu. Nikalia....lol
na nikaonekana mbea hasa
 
Loh,kweli mlikua watoto maana...!
Mi nilisutwa sekondari tena huo umbea uliniangukia tu jamani.
Kuna dada alikua anahisiwa mjamzito mi sikujua. Watu wakateta wakakatisha ghafla mi sikumjua anayesemwa kumbe anakuja na kaskia.
Badae tupo wawili akaniuliza mi nikasimulia kilichosemwa bila kujua namsema yeye.
Loh,kutoka pale akaenda kusema niliyomwambia,wakaja nikawekwa kati,najitetea watu wanazidisha kelele tu. Nikalia....lol
na nikaonekana mbea hasa

Hahahahahahaha. . . .
Da Pretty nimecheka karibu chozi. Huyo msichana alikupata vizuri kweli japo sio wewe uliyeanzisha maneno. Mara nyingi umbea hua anaekamatwa nao mwisho ndio mtuhumiwa, hamna cha nimesikia wala nimeambiwa.
 
Heheh pole lizzy! Mie nilishawa wahi kusutwa na mama yangu tu ktk maisha kwa kumuongopea kwa baba! Ila tangu hapo alinifunda kutokutumia maneno alisema, anasema, atasema! Ila nimesuta wengi!
Yeahh hayo maneno ni ya kuyaogopa sana kwakweli.

Hhhm ulowasuta walikua wanakuzushia wewe?
 
mtanivunja mbavu
unasutwa na mama mzazi???
how??

Heheh pole lizzy! Mie nilishawa wahi kusutwa na mama yangu tu ktk maisha kwa kumuongopea kwa baba! Ila tangu hapo alinifunda kutokutumia maneno alisema, anasema, atasema! Ila nimesuta wengi!
 
Ushawahi kuwa mmbea? Ulishasutwa?

Mi niliwahi zamani kidogo wakati nikiwa darasa la nne nadhani, na nilivunja urafiki na my 'then' best friend kwa huo umbea na hapo hapo nikakoma.

Kulikua na msichana mmoja darasani kwetu, mkubwa kuliko wasichana wote. Hata kukua(vunja ungo) alikua wa kwanza, yani darasa la nne tayari alikua ameshalipuka kila kona ya mwili, alafu alikua anapenda kweli kukunja sketi yake ya shule iwe fupi na kufunguo vifungo vya shati wakati wengine tulikua tunafunga mpaka karibu na shingoni. Zaidi ya hapo alikua hamaind kabisa kushikwa shikwa na wavulana na wenyewe wakawa wanajua na walikua wanamshika haswa.

Sasa bwana huyo msichana alikua na mdogo wake mdogo sana, maneno yakazuka kwamba yule sio mdogo wake ni mtoto wake kutokana na story zilizokua zinasikika kuhusu yeye na wanaume. Mimi baada ya kuambiwa na msichana mmoja jirani yangu kesho yake wakati wa kwenda shule nikamnong'oneza rafiki yangu. Siku moja hata sikumbuki kilitokea nini si akaenda kumwambia mhusika na wasichana wengine bana. Loh likanijia jopo bana. Basi kunipiga hawawezi, kwenda kushtaki kwa walimu hawawezi wakaishia kuongea tu. Baadae nikawaelezea kwamba mi niliambiwa na sikuongeza chochote, ila nikamwambia huyo msichana mwenyewe samahani kwa kumwambia mtu mwingine basi yakaisha.

Ila kwanzia siku hiyo yule rafiki yangu ubesti uliisha tukawa tunaongea kawaida tu. Since then maneno ya "nimesikia, akasema" hua nayaogopa kweli. Kusutwa noma!!!

proved mwanamke umbea kusutwa suna...sosi mitikisiko ya pwani na dida
 
Niliwahi kusutwa pia humu jf na jamaa mmoja alikuwa anajiita wa kusoma! Baada ya kupigwa ban akaja na jina la complicator nikamgundua! Heheh nilivyomuweka hewani alinisuta nikashindwa kuthibitisha kuwa ni yeye!
 
ha ha ha, pole
i can imagine...
Sijui nilie sasa hivi for u

ila kwa sasa hata nikisutwa siogopi

Nilikua mzembe tu hadi najiuliza ilikuaje maana ningewacharukia...
Tangu pale sijasutwa tena maana nina hasira za mwaka ule,atakaetaka kunisuta akianza kuuliza nikimjibu moja tu anageuza njia
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom