Umasikini wetu ni akili sio mali wala fedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umasikini wetu ni akili sio mali wala fedha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by meningitis, Dec 20, 2011.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kuchunguza mambo hasa katika field ya afya na nimeona tatizo linalotusumbua sio fedha bali ni akili au utashi wa kufanya mambo muhimu.

  Nikichukulia mfano wa mama mjamzito anapokwenda kujifungua bila kubeba pamba, mipira(gloves) au cord clamp kisa kaambiwa huduma ya kujifungua ni bure! Ukipiga mahesabu vifaa hivi vinaweza kugharimu sh.10000 tu lakini mama huyo huyo ataletwa hospitali na tax(10000) huku akiwa amebeba kanga na vitenge vipya vinavyogharimu sh 35000+,halafu akijifungua atafanyiwa party inayogharimu zaidi ya sh 60000. Sasa hapa utajiuliza kipaumbele ni nini!

  Wamarekani(USAID) wanajichukulia umaarufu katika kuchangia huduma hizi za afya na hela hizi huchangwa na watu(wananchi) wa marekani.

  Je, kwanini wananchi wa Tanzania wasitoe michango yao(fund rising) na kusaidia watanzania wengine? Tunasaidiwa fedha ambazo tunaweza kuzikusanya wenyewe kama tukiamua.

  Hivi tuna shida gani upstairs?
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  huduma za afya sio bure bali zimelipiwa,kwa bahati mbaya waliolipia sio watanzania na wakiamua kujitoa tutaumia sana!
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sure aminia
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu huu ni ukweli ambao hatutaki kuujadili lakini tumezoweshwa vibaya ndio maana cameroon anatudhihaki.
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe 100%.
   
 6. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nashukuru ff,tuweke ushabiki wa siasa pembeni na tubadilike.
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  tukubali au tukatae tumekuwa watu wa porojo bila vitendo.
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hivi hiyo akili tumeipata lini? Wakati miaka zaidi ya 20 ya mwanzo tuligubikwa kwa kuaminishwa kuwa mwenye akili ni mmoja tu. Tuliwekwa ndondocha.
   
 9. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  WaTZ wote ni vilaza, kwa hiyo usishangae sana.
   
 10. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  tusirudi kuangalia nyuma,tunapoelekea ni pagumu hawa wazungu watasitisha misaada.tunahitaji kubadilisha fikra,tunahitaji kujitegemea tukatae misaada ya fedha badala yake tupewe vifaa na utaalamu.
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  naomba kwa heshima na taadhima uniondoe kwenye kundi hilo la vilaza.
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Tanzania si akili bali ni utamaduni!. Watanzania inabidi tuwe makini sana kila siku tunapolalamika eti hatuna akini hakuna hata kitu kimoja kinachoonyesha kuwa sisi hatuna akini za kuzaliwa kutokana na kuwa Watanzania.

  Mfano mzuri ni Watanzania walioenda nje!. Wengi walifikiria wenyewe kwenda nje, wakatafuta vyuo wenyewe, wakaomba visa wenyewe, wakasafiri, wakajifunza maisha na utamaduni wa nchi walizokwenda, wamejifunza lugha, wengine wamejisomesha kwa kazi zao, wapepata kazi za degree baada ya kusoma, wameanza familia na kusaidia nyumbani. Haya yote yamefanyika bila msaada wowote wa kulipiwa chochote na serikali yeyote. Sasa hawa vijana walioenda nje sio kwamba wana akili zaidi kuliko wenzao waliobaki Tanzania na kuingia vyuoni na mara nyingi kielimu hawa waliobaki Tanzania walifanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya Form 6. Tofauti ni utamaduni walioenda nje ilibidi wabadilike ili waweza kwendana na maisha mapya kwenye nchi za watu!. Tatizo ni kwamba sisi tulio nje tukizungumzia swala la utamaduni tumekuwa tukipigwa madongo kwamba tunajifanya tumebadilika lakini ukweli ni kwamba kuna matatizo mengi ya Tanzania ni utamaduni mbaya. Hata vitu kama rushwa ni utamaduni kwani nchi nyingine hakuna utamaduni wa kumpa mfanyakazi wa serikali pesa na unaweza kufungwa miaka mingi kwa hilo
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni ulimbukeni mama wakati wa Nyerere hatukuwa na Kitchen party, Valentine wala sikukuu ya wachawi.. harusi tulizifunga kiislaam kwa misahafu tu na hakuna gari chukua mkeo hata kwa baiskeli, leo hii usipoambiwa millioni 10 labda umeona mmasai..
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Sikiliza kwa makini;

  Wazungu na sisis hakuna tofauti ila rangi ya ngozi.

  Sisi tumejaaliwa kila kiyu kuliko "wazungu". Kama unabisha uliza wasio wazungu na walio wazungu ni nani anae faulu zaidi katika mitihani?

  Hapo ndio tunapokosea. Kufaulu mitihani haina maana sisi ni bora zaidi. Boara zaidi ni yule anae jislalimisha kwa mola wake.
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo pakufanye uelewe kuwa Nyerere alitufungia hata kujuwa Kitchen party ni nini.

  Kitchen party ipo zama na zama. Ni majina tuu, wenzetu waliiita "kitchen Party" kwa kuwa wanaume walikuwa hawaruhusiwi wasikie yanayoongelewa jikoni. Na ndio mpaka leo hapa kwetu hatualiki mwanamme kwenye "kitchen Party", wanaume tunawaalika "chicken party" tu.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mfano mwingine, watanzania wengi tu mtu hana kazi maana lakini ana simu mbili..matumizi mabaya ya pesa
   
 17. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Faiza umenifanya nicheke,eti wanaume wanaalikwa kwy chicken party,napita tu
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa nini waseme huduma ya afya ni bure nami niende bure kisha niikose hiyo huduma ya bure? Wao ndio wana akili afkani. Waseme kuwa uje na hiki na hiki, na asipokuja navyo ndio tumzodoe huyu mama. Kwa hilo hauko sahihi. Uko sahihi kuwa hayupendi kujifikirisha na kusema 'what if'. Hii what if ndio msingi wa planning.
  What if wazazi wanaongezeka kwenye zahanati yetu.
  What if wahisani wakiahirisha misaada yao
  what if mafuriko yakija
  what if magari yemeongezeka kwenye barabara zetu hadi capacity imekuwa chini ya demand
  what if, what if, what if kwenye kila sekta. Mwisho wa siku mnnajikuta mnakuja na plan against the pruduct of what if. Hapo ndio hatujui
   
 19. t

  teamoo Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza ukawa na fedha lakin kam akil ya kupambanua mambo huna, bas bdo tutakuita maskini. Ni kwel umaskin ni pamoja na maradhi, ujinga, rushwa, na mengne meng. Hivyo tunahtaji kuelmika pia ndipo tutaanza kutoka katika umaskini wetu
   
 20. t

  teamoo Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mmasai anahtaj ng'ombe za kutosha ndo umpate bint yake. Bdo ni gharama tena kubwa 2.
   
Loading...