Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,103
Wakati wazungu wakiwaza waisaidiaje Africa kupiga hatua kiuchumi, Africa inawaza iombeje misaada kwa kuhonga Raslimali zake kwenye mataifa hayo makubwa ulimwenguni .
Umasikini wa Fikra ni vita kubwa sana ulimwenguni kuliko vita yeyote iliyowahi kutokea.
Unadhani kama siyo umasikini wa fikra tungeweza kutengeneza zile Machine pale Muhimbili kwa kiasi cha bilioni 3 kisha ikaharibika na tukatengeneza tena na Sasa tumenunua machine hiyo kwa kiasi cha dola za kimarekani kiasi cha milioni 1.7?
Nawaza tu, hivi tunaweza kuwa Taifa la Tano kwakuuza Tanzanite Duniani ile hali Madini hayo Ulimwenguni yanapatikana Tanzania Pekee??
Tunasema Tunapunguza ukubwa baraza la Mawaziri ile hali tunaweka watendaji wake (Makatibu wakuu na manaibu makatibu zaidi ya hamsini) ukijumlisha na Mawaziri wake ni zaidi ya 80... Umasikini wa Fikra upigwe vita sana kuisadia Tanzania (Africa) Magogo yanauzwa nje na bado Watoto wetu hawana madawati wanakaa chini...Misitu imegeuka kuwa sehemu ya mateka..
Dhahabu zinawafanya watu kuumwa ugonjwa wa trakoma kwakuwa wanaachiwa vumbi na mashimo ambayo eti wanatumia kwaajili ya kukinga maji ya mifungo, madini yanatengeneza barabara, majengo makubwa ambayo viongozi wetu wakienda nje huenda kulala huko na kulipia fedha za kutosha wakisubiri mirahaba baada ya mchanga kusafishwa.... Africa inahitaji kupambana na umasikini wa Fikra.. Elimu,Elimu,Elimu ndiyo suluhu ya umasikini was vita hii ya Fikra.