Umasikini ni chanzo Cha Mabaya (Umasikini ni ulozi)

Umasikini ni chanzo Cha Mabaya (Umasikini ni ulozi)

fact only

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
975
Reaction score
1,356
Habari wana JF.

Umasiki ni chanzo Cha Mabaya kero, Uchawi, ulozi, kunuka jasho, wivu, ukatili n.k.

Masikini ndiyo mtu wa kwanza kuingia Motoni hata kama ulikuwa unasali sana kama umekufa masikini ni Motoni moja Kwa moja.

Kwasababu.

Umasikini unakufanya muda wote unawaza mabaya Mabaya, unawaza kushidwa, Unaona kila kitu kizuri ni cha shetani ukiona mtu/watu wamefanikiwa unaamini wameloga au Freemason.

Hauwezi kukuta mtoto (Binti) wa Bakhresa anataka/waza kumloga jirani/ndugu yake kisa kamzidi kimaisha(Uchumi, watoto, elimu n.k). Masikini fasta anakupoteza.

Umasikini ni chanzo Cha uchafu unafanya watu wananukanuka hovyo (midomo, jasho, shida, nyuchi n.k). Mtu anaenda chooni na kopo, ndoo ya maji nusu matokeo yake hajisafishi vizuri wisho ni kunuka tu.

Umasikini unakondesha, unatia unyonge, una fedhehesha, una hangaisha, umasiki unakupa wivu usio na faida, umasikini unatesa unatesa unatesa, umasikini unakujengea chuki with no reason umasikini una kupeleka mbiombio ili uteseke zaidi na zaidi.

Wakuu tupambane na umasikini vizazi vyetu visiendelee nao otherwise umasikini utaendelea kukupeleka mbiombio with no reason.
 
Back
Top Bottom