Umakini unahitajika kwenye hii Mitandao

Umakini unahitajika kwenye hii Mitandao

Kwangu nakukatalia kama ifuatavyo...

6. Mimi ndiyo mwana ambaye sijasoma kama walivyosoma wana JamiiForums wote hapa

7. Mimi ndiyo mwana JamiiForums nisiye na Baiskeli, Guta, Pikipiki, Gari na Nyumba kuliko wana JamiiForums wote.

Nasubiri Maua yangu kwa huu Uwazi.

Kusoma umesoma sema umesoma chuo uchwara, chuo cha hovyo kuliko wote humu JF.
 
Kuna jamaa anauza duka la nguo la shemeji yake Tabata.

Yule mshkaji ninajua kwa hakika kabisa kuwa analala store nyumbani kwa dada yake. kila mtu anajua nguo zake kwa maana ni chache mno.

Ingia instagram yake sasa, kwanza kama sikosei anajiita either 'don' ama 'rich boy'. ZIle nguo anazouza ana kazi ya kuzivaa na kupiga picha na kupost instagram. Karibu ya duka la shemeji kuna pub moja kubwa sana, hapo ndipo anapofanyia photoshoot zake.

Ukipitia picha zake unaweza hata mlaumu Mungu juu ya umaskini wako, ila fuatilia ukweli sasa ni lazima utamuonea huruma.

Hana off, anapiga kazi j3 mpaka j3 saa mbili asubuhi mpaka 3 usiku.
 
Nimecheka kwa sauti jamani 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wanasema kujiita masikini, ni kujilaani mwenyewe; unatakiwa ujimwambafai ili kuongeza roho ya upambanaji
Umenikumbusha mkuu.

Niliwahi kusimuliwa kwamba kuna jamaa alikuwa kapuku wa kutupwa, siku isiyo na jina akaingia show room ya magari akaanza kukagua magari kama anataka kununua vile!

Baadaye akatoka. Rafiki yake akamuuliza kwanini amefanya vile, jamaa akajibu aliingia mule show room ili aushtue umaskini, imani yake kubwa ni kwamba umaskini wake siyo hali ya kudumu, hataki umaskini umzoee. Kwasababu bado anapambana basi kuna siku atatusua.

Niliona logic kwenye hoja zake kwasababu kwa sisi Wakristo hata Biblia inamesema, "ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo".
 
Back
Top Bottom