jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Kwa nini umeamua kubadilika?Serikali hii haina umakini ni kama vile inaendeshwa na mataahira. Mikataba ya uchimbaji wa madini iliposainiwa kama sikosei mwaka 2000 bei ya ounce moja ya dhahabu ilikuwa ni $220.
Bei ya dhahabu ikaanza kupanda kuanzia mwaka huo na hadi kugusa $1,900 kwa ounce moja, lakini bado tulikuwa tunapata mrahaba ule ule wa 3% pamoja na kuwa mapato ya hao wawekezaji kutokana na dhahabu yetu yaliongezeka karibu mara 20.
Pamoja na ahadi za Kikwete 2005 kwamba angehakikisha mikataba ile inafanyiwa modification ili Tanzania ifaidike na dhahabu yake lakini ni mwaka wa sita sasa hajafanya lolote.
Mapendekezo ya kamati ya Bomani kwamba makampuni ya uchimbaji wa dhahabu yatozwe kodi kubwa ambayo iwe inapanda na kushuka kama bei ya dhahabu katika soko la dunia hayakufanyiwa kazi.
Sioni kama hii Serikali taahira itafanya lolote la maana kati ya sasa na 2015 ili kuhakikisha mrahaba unaongezwa toka 3% labda hata kufikia 20% na pia kuanza kuyatoza makampuni hayo kodi kubwa sana ili nchi ifaidike, kama hawatakubali basi waruhusiwe kuondoka tena wafanye hivyo haraka sana.