Umakini katika madini unaweza kunusuru uchumi na kuimarisha shilingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umakini katika madini unaweza kunusuru uchumi na kuimarisha shilingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Oct 31, 2011.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  NB: WAKATI NAANDIKA TAARIFA HII KWA UMMA TAREHE 28 OKTOBA 2011 DOLA MOJA ILIKUWA 1800, PAMOJA NA HATUA ZA KIFEDHA ZA BENKI KUFANIKIWA KIDOGO KUSHUSA MPAKA 1700 KWA KIWANGO CHA LEO BADO HATUJAWEZA KUREJEA KWENYE KIWANGO CHA KARIBUNI CHA CHINI YA 1600.

  PIA, HATUA TATU ZILIZOCHUKULIWA NA BENKI KUU ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA MZUNGUKO WA FEDHA NCHINI IKIWEMO KUPUNGUA KWA UPATIKANAJI WA MIKOPO KATIKA BENKI ZA KIBIASHARA HALI AMBAYO ITAKUWA NA MADHARA KWENYE UZALISHAJI SIKU ZA USONI. HIVYO, NI MAONI YANGU KWAMBA SUALA LA KUHUSISHA KWA KARIBU SEKTA YA MADINI KWENYE JUHUDI ZA KUKABILIANA NA MFUMUKO WA BEI NA KUIMARISHA SARAFU YETU BADO LINAHITAJI MJADALA ENDELEVU WENYE KUWEZESHA HATUA ZA HARAKA KUCHUKULIWA.

  TAARIFA KWA UMMMA-28/10/2011: Pamoja na kuchukua hatua za dharura za kuchochea ongezeko la uzalishaji katika kilimo na viwanda na kuwezesha udhibiti wa bei ya bidhaa muhimu kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha kunakosababishwa na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania pamoja na; serikali inapaswa kuitumia sekta ya madini katika kunusuru uchumi wa taifa na maisha ya wananchi.

  Izingatiwe kwamba mfumuko wa bei nchini pamoja na kusababishwa na kupungua kwa uzalishaji unachangiwa pia na nakisi ya bajeti pamoja na udhaifu katika matumizi ya serikali wakati kuporomoka kwa sarafu kunatokana pia na ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya ongezeko la uagizaji wa mafuta na malighafi nyingine toka nje.

  Hatua tatu za kifedha ambazo zimechukuliwa na benki kuu katika kipindi cha takribani wiki moja hazijaweza kuimarisha sarafu yetu badala yake imeendelea kuporomoka kutoka dola moja kubadilishwa kwa 1600 mpaka 1800; hali ambayo inahitaji hatua za ziada na za haraka kuchukuliwa na mamlaka zingine za kiserikali kwa kushirikiana na sekta binafsi.

  Kati ya hatua hizo ni Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na benki kuu kuitumia sekta ya madini katika kunusuru uchumi wa nchi kwa kurejea mapendekezo ya bajeti mbadala za kambi ya upinzani kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

  Kati ya hatua hizo ni pamoja na Wizara ya Fedha na Benki Kuu kutumia sera, sheria na kanuni husika kufanya majadiliano ya haraka na makampuni ya madini yaweze kuzingatia taratibu za kutunza sehemu kubwa ya fedha za nje (walau 60%) kwenye benki za ndani ili kusaidia kwa dharura kudhibiti kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania.

  Hatua nyingine ni Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana kwa haraka na Wizara ya Fedha na Benki Kuu kutunza sehemu hifadhi yetu ya fedha za kigeni katika mfumo wa madini hususani dhahabu kutokana na thamani ya mauzo ya madini kuongezeka wakati sarafu ya Tanzania ikizidi kuporomoka.
  Hatua ya ziada ni kutoza sehemu kubwa ya mrabaha kwa dhahabu badala ya kutoza kwa fedha pekee; na kutoza mapema mrabaha huo kwa asilimia nne kabla ya kukokotoa baadhi ya gharama kama Sheria ya Madini inavyohitaji badala ya asilimia tatu baada ya kuondoa baadhi ya gharama kama ilivyo sasa hatua ambayo itachangia katika kuongeza pato la taifa na kuimarisha sarafu yetu.

  Hatua ya nyongeza ni kwa serikali kuelekeza mapato mengine yaliyopatikana katika sekta ya madini katika kutekeleza mpango maalumu wa dharura wa kuongeza uzalishaji na kupunguza madeni yenye kuongeza mfumuko wa bei na kuporomosha shilingi ya Tanzania. Mathalani vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa tarehe 27 Oktoba 2011 vimeeleza kwamba kampuni ya Anglo-Gold Ashanti italipa kodi ya mapato ya kampuni kiasi cha dola milioni 50 (ambayo ni takribani bilioni 90) kwa kiwango cha sasa cha kubadilisha fedha na kwamba tayari imeshalipa bilioni 8.6 katika katika kiasi hicho ikiwa ni mara ya kwanza toka kampuni hiyo ianze uchimbaji wenye tija zaidi ya miaka kumi iliyopita.

  Haya ni mapato hayako kwenye bajeti ya serikali 2011/2012 hivyo serikali inapaswa kutumia mapato hayo kama bajeti ya nyongeza ya kutekeleza mpango wa dharura na kupanua wigo wa kuyataka makampuni mengine ikiwemo African Barrick Gold (ABG) yenye migodi mikubwa minne ambayo yote hailipi kodi ya mapato ya kampuni. Hatua hii iende sambamba na kupunguza matumizi ya anasa pamoja na kuvitumia vyanzo mbadala vya mapato vilivyoelezwa na kambi ya upinzani ili kupata fedha za nyongeza za kuingiza katika mpango wa dharura wa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi. Hata hivyo, udhibiti wa ziada unahitajika katika kutekeleza mipango yote ya dharura ili kuepusha mianya ya ufisadi kama ilivyokuwa katika miradi ya kufua umeme IPTL, Alstorm Power Rentals, Richmond na fedha za kuchochea uchumi (Stimulus Package).

  Itakumbukwa kwamba tarehe 23 Oktoba 2011 nilifanya mkutano na waandishi wa habari kutaka hatua za dharura kuchukuliwa na Rais Kikwete na bunge kuhusu kupanda zaidi kwa gharama za maisha kunakochangiwa na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa kasi kwa shilingi ya Tanzania.

  Katika mkutano huo nilitahadharisha kwamba hali ngumu ya maisha kutokana mfumuko wa bei ambao umefikia asilimia 16.8 na kuporomoka kwa sarafu yetu ambapo sasa imefikia dola moja ya Marekani inabadilishwa kwa zaidi ya 1800 ni tishio kwa uchumi na usalama wa nchi na maisha ya wananchi.
  Katika mkutano huo nilieleza kwamba bidhaa zinazochangia kwa kiwango kikubwa mfumuko wa bei ni vyakula na nishati hususani matatizo ya umeme na gharama kubwa za mafuta na gesi asilia. Aidha, kuporomoka kwa thamani ya shilingi kunachangiwa na mahitaji makubwa ya dola miongoni mwa waagizaji wa bidhaa toka nje na urari hasi wa biashara kutokana na upungufu wa mauzo ya bidhaa zetu katika masoko ya kimataifa.

  Kwa hali hiyo nilishauri hatua za dharura za Rais na Bunge katika kuongeza uzalishaji na usambazaji hususani wa vyakula katika soko la ndani, kuwezesha wazalishaji wadogo na wa kati katika kilimo na viwanda kuongeza mauzo ya nje na kuharakisha matumizi ya gesi asilia na utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.Juhudi hizo ziende sambamba na kampeni maalumu ya kuhamasisha watanzania kununua bidhaa za ndani na serikali kutekeleza mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini. Kadhalika, kwa upande wangu nilieleza kusudio la kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya udhibiti wa bei ya bidhaa muhimu hususani za chakula ili kukabiliana na ukiritimba katika soko na kuweka mfumo wa kupunguza gharama za maisha kwa watanzania wa kipato cha chini.

  Kwa upande mwingine, nilieleza kwamba kwa kuwa mfumuko wa bei unachangiwa pia na matatizo katika mfumo wa bajeti na matumizi ya serikali kutokana na ufisadi, ubadhirifu, matumizi ya anasa, mikopo isiyokuwa na udhibiti, kushuka kwa mapato ya serikali ikiwemo kupungua kwa fedha toka washirika wa kimaendeleo kutokana na matatizo ya kifedha katika ukanda wa ulaya; hivyo hatua za dharura za kibajeti na kimfumo zinahitajika kwa kuhusisha serikali na bunge badala ya kuachia hatua za kisera za fedha za benki kuu pekee.

  Wenu katika utumishi wa umma,

  John Mnyika
  Mbunge wa Ubungo na
  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

  28/10/2011
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,177
  Likes Received: 1,178
  Trophy Points: 280
  Selikali hii haikanyiki!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Siri ya kuimarisha shilingi yetu huenda ikaharakishwa zaidi na umakini kweli katika umakini wetu jinsi tunavyongoza uchimbaji madini na kuzingatia sera ya uongezaji thamani kabla ya kusafirishwa kwenda nje.

  Vile vile tunahitaji kuweka mfumo shirikishi kwa wadau kwa wigo mpana zaidi katika sekta hii na sekta ya umeme na hasa ule unaotokana na gesi ili tusijeingia mkenge tena kwenye suala zima ya mikataba.

  Umakini katika eneo hili la pili litatusaidia kufanya gharama ya uzalishaji kushuka na idadi ya wawekezaji kuongezeka, mapato ya serikali kupanda, ajira kushamiri, demokrasia kuimarika na amani na utengamano kupatikana kiuhakika zaidi.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,572
  Trophy Points: 280
  Serikali hii haina umakini ni kama vile inaendeshwa na mataahira. Mikataba ya uchimbaji wa madini iliposainiwa kama sikosei mwaka 2000 bei ya ounce moja ya dhahabu ilikuwa ni $220.

  Bei ya dhahabu ikaanza kupanda kuanzia mwaka huo na hadi kugusa $1,900 kwa ounce moja, lakini bado tulikuwa tunapata mrahaba ule ule wa 3% pamoja na kuwa mapato ya hao wawekezaji kutokana na dhahabu yetu yaliongezeka karibu mara 20.

  Pamoja na ahadi za Kikwete 2005 kwamba angehakikisha mikataba ile inafanyiwa modification ili Tanzania ifaidike na dhahabu yake lakini ni mwaka wa sita sasa hajafanya lolote.

  Mapendekezo ya kamati ya Bomani kwamba makampuni ya uchimbaji wa dhahabu yatozwe kodi kubwa ambayo iwe inapanda na kushuka kama bei ya dhahabu katika soko la dunia hayakufanyiwa kazi.

  Sioni kama hii Serikali taahira itafanya lolote la maana kati ya sasa na 2015 ili kuhakikisha mrahaba unaongezwa toka 3% labda hata kufikia 20% na pia kuanza kuyatoza makampuni hayo kodi kubwa sana ili nchi ifaidike, kama hawatakubali basi waruhusiwe kuondoka tena wafanye hivyo haraka sana.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mnyika tunahukuru kwa mapendekezo yako lakini ni lazima uelewe yafuatayo

  1. Tanzania imefanya makosa makubwa kutokununua hisa kwenye haya mashirika hata kama ingekuwa 20% ya uzalishaji ingetosha. Hii ni kwasababu ingewezekana kabisa kwa serikali badaya ya kuuza kuchukua fungu lao na kuhifadhi kama Gold.

  Vilevile ingesaidia kwenye mapata ya serikali kwani Gold siyo madini ya bahati nasibu. Serikali haijachelewa inaweza kufanya hivyo kwa miradi mipya inayopatikana.

  2. Hakuna sera nzuri Tanzania za ubalishaji wa pesa. Mimi nilikuja Tanzania na kama $1500 na cha kushangaza dola imekuwa kama bidhaa badala ya pesa.$100 ina bei tofauti, $50 ina bei tofauti na $20 ina bei tofauti. Dollar nyingine $100 zilikataliwa kwasababu ni zimetengenezwa 1996.

  Hii mimi nilikuwa sijawahi kuiona na kukaa kwangu hapa USA kwa miaka 14 sasa sijawahi kusikia dola ina thamani tofauti!. Hivyo dola kama wamesema inakubalika ikubalike kama nchi nyingine yeyote bila masharti ambayo hayana msingi. Ili bidi nirudi na dola zangu huku.

  3. Utalii: Dola zote za utalii zinaenda wapi? kuna watalii million moja kila mwaka hizo pesa za kigeni zinaenda wapi? Mnatakiwa kufuatilia hili vizuri kule Arusha labda huyo mbunge mwezenu wa Arusha anaweza kutupa majibu.

  4. Ukweli ni kwamba vitu vingi vya Tanzania vinatoka nje na kama uchumi unakuwa na hakuna uzalishaji wa vifaa Tanzania ni vigumu sana kutatua tatizo hili.

  Siku hizi hata vitasa na cable zinatoka nje sasa ni vigumu sana kwa nchi inayoendelea kupata dola nyingi hivyo za kila mara.Vilevile cha kushangaza ni kwamba kama watu wanaenda kununua vitu China ni kwanini wasinunue pesa ya China bank badala ya kununua dola?. Hawa wa China wanawachezea na ni lazima muangalie hilo.

  5. Bank: dolar nyingi zinatumwa Tanzania lakini hazifiki mfano Money gram na western union hawapeleki dolar Tanzania bali wanawapa shilingi. CRDB na bank nyingine za Tanzania zingeweza kutatua hili Tatizo mafano kama watu wote tungekuwa tunatuna pesa kwa bank badala ya Money gram au western union basi bank zetu zingekuwa na reserve kubwa na wangeweza ku import hizo dollar.

  Cha kushangaza mfano CRDB wana account kwenye Citi Bank ya NY na ile pesa hawaipeleki Tanzania wanaiweka huku kama savings yao badala ya kwenda bongo kusaidia kupunguza thamani ya dola.

  6. Mfumuko wa bei wa Tanzania hautokani na bei ya mafuta huo sio ukweli Tanzania inatumia mafuta kidogo sana na kuna magari chini ya million moja Tanzania nzima!. Mfumuko wa bei unatokana na umeme!. Umeme unaongeza gharama sana za uzalishaji, unapunguza upatikanaji wa gas hivyo vitu kama vyakula haviwezi kuhifathiwa.

  Hii ni sababu kubwa kwani Watanzania wengi wafanya bishara ndogo wa mazao ya mboga, nyama, samaki hawawezi kufanya bishara wakati huohuo bei ya vyakula muhimu inakuwa juu. Kiuchumi wanasema kwa kiingereza " demand for food is inelastic" maana yake watu watanunua tu hata kama bei iko juu lakini vilevile wanasema "price of food is elastic" hivyo bei inaweza kuongzeka hivyo ni kwamba hata kama bei itakuwa juu watu watanunua vyakula.

  7. Mwisho kuna watu wengi sana wanajaribu kutulinganisha na Kenya lakini Kenya sera yao ni ku control exchange rate kama China wakati Uganda na Tanzania Exchange rate zetu zinaenda na market kama western countries. Exchange rate za Tanzania na Uganda ziko realistic kuliko za Kenya.

  Siwezi kuelezea zaidi hili lakini google.
   
 6. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  heshma kwako jm.
  Kwanza nasema tumechelewa,na kama ukitaka kujua tunaliwa kiasi gani kwenye madini mtafute kamishina wa madini wa zamani ambaye yupo dodoma.
  Mr.kenyunko.unaweza kujua jinsi nchi inavotafunwa.

  Mgodi kama buliyankulu wameshachimba kwenda chini kama 2000m deep=2km deep na wanapata 60g of gold kwa 1tonne of rock inayochimbwa. Mwanzoni walikuwa wanapata 2g of gold kwa 1tonne of rock inayochimbwa. Means as they go down concentration ya gold inaongezeka.je wat we get as a nation???
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mimi naona swala la ufisadi ndilo linachangia haya yote. Chukulia mfano mikataba ya madini ambayo mwekezaji halipi kodi ni swala ambalo halishughulikiwi just because kuna vigogo wananufaika.

  Sekta ya umeme ndio inategemewa kuwanufaisha wajanja wachache. Kwa kuwa wahusika tuliowapa mamlaka hawezi kuchukua hatua yeyote kwa sababu wao binafsi wana maslahi yao kutoka kwenye huu mfumuko na ugumu wa maisha tunaou'face leo hii, dawa ni kuwawajibisha kwa kuwaondoa madarakani. Basi.
   
 8. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  We umegusa part tu, na whole
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi kuna uhakiki wa hii migodi kweli?
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hongera mnyika kwa kufikiria kuendelea kusafisha hilo donda.
  ila kaka tuwe wakweli hapo ni kukata mguu tu,kidonda hakitibiki tena,mguu unaoza unaingia kwenye nyonga sasa.

  ni wakati wa mabadiliko ya kweli tubadilike.nakuunga mkono kwenye signature ila kwenye maoni tuchukue nchi tuyafanyie kazi hawa watu ni viziwi.
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Umeongea vizuri Mh. Mnyika maana Watanzania wengi siku hizi tunalalamika tu bila kutoa suluhisho la matatizo.
  Umetimiza wajibu wako lakini tatizo hawa wenzetu walioko upande wa pili wa utekelezaji (watawala) daima hawapendi kusikiliza ukweli na katika hili la devaluation ya shilling limekaa vibaya kutokana na usimamizi wa uchumi usiokuwa na mwelekeo!
   
 12. M

  Mangolo Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mh umesema na umeandika na tumekusoma ni mambo ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu
  tatizo ni nani wa kuyafanyia kazi?angalau hata kufanyia majaribio,wako na mambo mengine tofauti na unayofikiri.
  Usikate tamaa endelea kusema iko siku.
   
 13. P

  POLITE MAN Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kanali muamar al gadaffi aliweza kutumia rasilimali moja tu ya mafuta ambayo wamepewa wananchi wa libya kuweza kupandisha uchumi wa libya maradufu, ela ya libya ilikuwa inatofautiana sikuzote kwa kiasi kidogo sana na dola ya marekani, yeye sera yake alikuwa sikuzote anataka mafuta yabadilishane na dhahabu na ilo sikuzote ndiolo alililokuwa akihimiza. Leo hii sisi tuna rasilimali lukuki lakini bado masikini wa kutupwa haya yote ni kukosa uwajibikaji kwa waliopewa dhamana, b.o.t na wao wanafanya kazi kisiasasiku izi, kila mtu anaona kuwa shilingi inapolomoka tena kwa kasi wao wana tutangazia kuwa shilingi ina imarika . How!!!!!!!!!!!!!??????????????
   
 14. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Uhakiki utoke wapi?
  Mikataba mibovu ndo inayotutafuna
  Toka enzi zile ounce moja dola 200 mpaka sasa 1900dola we unategemea nin?
  Tumuachie mungu!
   
 15. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Kamundu,

  Nakubaliana na wewe katika sehemu kubwa ya uchambuzi wako. Suala la kuwa na hisa katika uwekezaji mkubwa ni la muhimu sana; na hii ndio linapaswa kuwa jukumu kubwa la STAMICO. Hata hivyo, matatizo yetu ni zaidi ya kuwa na hisa; kwa muda mrefu tumekuwa na hisa katika mgodi wa Mwadui kwa mfano, lakini ufisadi na udhaifu wa kiuongozi ukafanya taratibu tuuze hisa zetu kutoka 100%, ikawa 50% na sasa 25%; lakini pamoja na kubaki na hisa hizo bado utakubaliana nami hatujaweza kuitumia vizuri fursa hiyo kwa manufaa ya taifa. Hali imekuwa hivyo katika migodi mingine pia. Lakini kwa ujumla, hata migodi ambayo hatuna hisa, MDA zinavifungu vyenye kutoa fursa kwa serikali kutekeleza hayo mapendekezo niliyotoa. Hivyo, hata sasa tunaweza kabisa kuyatekeleza kama kukiwepo na umakini na uadilifu.

  Kuhusu utalii, sehemu kubwa ya mapato yanabaki nje kutokana na package tourism; ndio maana nimesisitiza kwamba masuala ya kukabiliana na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shililngi yasiachwe kwa Kamati ya Fedha na Uchumi pekee pamoja na Wizara mama bali kila sekta iangalie kwa upande wake. Kama ilivyo kwa madini sekta ya utalii inayofursa ya kuchangia katika kuimarisha uchumi wetu, ndio maana rai yangu imekuwa kutaka kamati zote za kisekta za bunge kuchukua hatua za haraka kuisimamia serikali katika sekta zao ili kunusuru taifa. Hivyo hivyo, kwa mfumo wetu wa kuhifadhi fedha za nje kama ulivyodokeza katika mabenki.

  Nakubaliana nawe pia kwamba mfumuko wa bei umechangiwa pia na matatizo ya umeme kuanzia kupanda kwa bei 18.5% mwezi Januari 2011 na hatimaye madhara ya mgawo wa umeme katika uzalishaji kwa kipindi chote cha uhaba wa umeme kutokana na kupungua kwa uzalishaji na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji. Hata hivyo, suala la mafuta nalo ni la msingi wake kwa kuwa katika siku za karibuni kumeongezeka mahitaji ya mafuta zaidi ya matumizi ya kawaida kwa ajili ya majenereta ya viwandani na pia kwa ajili ya mitambo mbalimbali ya umeme wa dharura ambayo kwa sehemu kubwa inatumia mafuta. Hali hii imeongeza mahitaji ya dola kwa ajili ya kuagiza nje. Hata hivyo, chanzo cha hali hii bado kinarudi pale pale kuwa ni umeme.

  JJ
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mh. Mnyika,

  Baada ya crisis meeting nilianzisha thread hebu kaipitie:-

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/183840-after-mkulos-crisis-meeting-bot-3-key-policies-to-rescue-shillings-3.html

  Narudia economist wengi wanasema hivi there is a little to what the Central Bank will be able to achieve to stimulate economic growth and saving currency volatility. Central Bank will either pumping more money into the economy or lower interest rate to encourage growth or reduce the amount of money in the economy. Currency yetu inasumbuliwa fiscal factors which needs the central government to get hold of it. Tightening of the fiscal policy will help to stabilise the currency.

  Leo hii 1$ ni sawa na 1600-1690 nchini utaona kuwa shillingi imepanda thamani. Sasa sijui ni zile hela za benki kuu au relaxation of the foreign currency deposits it is unknown kwanini shillingi imepanda thamani kutoka 1$ - Tshs 1850-1890 hadi kurudi Tshs 1600-1690. Kuna mambo yanahitajika kuwa tackled kwa kutumia fiscal policies.
   
 17. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nashukuru na tunawaomba mtembelee hapa tuongelee mambo mengi kama ya elimu, afya na fetha. Nitakuwa natoa topic za kuangalia mbali na naomba support kutoka kwenu. Kila wiki nitatoa topic moja ya msingi naomba tuisome
   
 18. M

  Mpambanaji K Member

  #18
  Nov 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwanakili, how can one possibly link with Mr. Kenyuko, the former mining commissioner as you directed us?
   
 19. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Mh.Mnyika, labda nikufahamishe kuwa Watanzania wengi wanakukubali kwa hoja zako hilo halina ubishi na mungu akulinde ili baadae hiyo hazina ya sera nzuri uliyo nayo watanzania tuje tufaidi hasa mtakapo chukua dola kwa njia ya sanduku.Ninakushauri ufanye yafuatayo;
  1. CDM mtumie mbinu mbalimbali za halali za kuelimisha umma wa watanzania ili mswaada wa katiba unaotarajiwa kujadiliwa uwe owned na tatanzania na si rais
  2. Kama hautabadilishwa basi muandae plan B maana bila kufanya hivyo watanzania twafaaaaaaaaaaa
  3. Katiba mpya iandikwe na watanzania wenyewe na si serikali, haiwezekani mkaba utengenezwa na service provider badala ya mwenye mali
  Ukifanikiwa haya wewe na CDM nina hakika hayo mazuri unayotuandikia leo utayatekeleza kwa nafasi na uhuru.Unachokifanya mkuu leo ni kumpigia mbuzi gitaaa.
  Mwisho fikisha salamu kwa Mh.Lema mwambie tuko nyuma yake watanzania pamoja na uoga wetu lakini karibu tutakomaaa kupitia nyinyi wabunge wa CDM
   
 20. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  shilingi ya Tanzania yaweza kuimarishwa kama ifuatavyo according to several readings:

  1. Kuuza Reserve ya Madini kama vile Gold, Diamond, Tanzanite, Ruby kwa pesa ya kigeni na kununua shilingi inayoporomoka kwenye soko la Kubadilisha fedha. Hii Benki Kuu wanaielewa. Ni Kama vile Mh. Mnyika ulivyosema tutumie MADINI yetu kuokoa kuporomoka kwa Shilingi VS Pesa ya Kigeni.

  2. Kubana matumizi ya Serikali kama vile a)kupunguza Posho na Safari zenye msururu wa Wapambe wasiotakiwa. Yaani hao Wapambe hata kama hawapo safari inakamilika. Sio Kiongozi kuhahakikisha kuwa Marafiki na ndugu zao wako kwenye Misafara yao ya Safari za Kigeni na hata ndani ya nchi. b) kutumia magari ya kifahari na kadhalika.

  3. Kuongeza Interest za Benki kwa wale walioweka akiba. Yaani ile akiba iliyowekwa Benki izae kiasi kwamba mtanzania ataona hana haja ya kukaa na pesa nyingi nyumbani bora ziwekwe Benki ili zizae tofauti na sasa hivi kwamba hakuna Benki inayotoa faida kwa wale tuliweka savings za kawaida. Badala yake tunakatwa Riba ya kuweka pesa Benki.

  Tunaweza pia kukopa fedha ya kigeni kwenye taasisi za Kimataifa
   
Loading...