Ingawa naelewa umuhimu wa mtoa picha na habari wa Ikulu kuedit kinachotoka mfano hata kama ni kwa bahati mbaya mkuu kanyanyua kidole cha Kati juu, picha hiyo haiwezi kutolewa, ukosefu wa ueledi katika kufanya kazi ni tatizo linaloigusa pia tasnia ya habari kwa kiasi kikubwa.
Wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika pale uwanja wa taifa, sauti za wapiga soga na matusi zilirushwa ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Nilishangazwa pia na namna Bw Michuzi alivyojiegesha katika jukwaa kuu Kama Mgeni mwalikwa (ikumbukwe hii ilikuwa ni siku chache tu baada ya taarifa kwamba anakaimu upigaji picha wa Raisi,Ikulu.) Nilijiuliza hivi Yuko pale kupiga au kupigwa picha?hii ni mifano michache Kati ya mingi ya matukio yanayoonyesha ukosefu wa UELEDI.
Picha ya Raisi kufananishwa na salute ya Hitler kwa mtazamo wangu Haina tatizo kwani jamii YETU haina mtazamo huo na wala hatuijui hiyo saluti