Umaarufu wa Bush washuka Marekani................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Umaarufu wa Bush washuka Marekani

Wednesday, 08 December 2010 19:40 administrator



WASHINGTON, Marekani

RAIS mstaafu George W. Bush wa Marekani ndiye kiongozi wa nchi aliyepoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa kulinganisha na wengine, imeelezwa. Kwa mujibu wa utafiti, Bush ndiye kiongozi asiye na umaarufu miongoni mwa viongozi wa Marekani ambao bado wapo hai. Bush ambaye ana umari wa miaka 64, kutoka chama cha Republican amepewa jina la utani la Dubya. Utafiti huo unahusisha marais walioongoza katika kipindi cha miaka 50. Katika uongozi wake aliingiza Marekani kwenye vita dhidi ya ugaidi na nchi ilishuhudia ikiingia kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi.

Rais mstaafu Bush ambaye ni mtoto wa Rais mwingine mstaafu wa Marekani, George H. W. Bush, alikuwa kiongozi wa 43. Aliongoza kuanzia mwaka 2001 hadi 2009. Kuingia kwake madarakani mwaka 2000 kulitawaliwa na utata katika kura baada ya kumshinda kwa kura chache mgombea kupitia chama cha Democratic, Al Gore. Akiwa madarakani na baada ya Marekani kushambuliwa katika tukio la Septemba 11, Bush aliamuru kuanzishwa kwa vita dhidi ya ugaidi na kuishambulia Afghanistan na baadaye mwaka 2003 kuishambulia Irak. Katika awamu yake ya pili mwaka 2004, Bush alifanikiwa kushinda, lakini kwa kura chache dhidi ya mgombea mwingine wa Democratic, John Kerry. Utafiti huo ulisema kuwa John F. Kennedy, ndiye kiongozi maarufu kuliko wote katika historia ya Marekani. Kiongozi huyo aliuawa mwaka 1963. Marais wengine waliofuata kwa umaarufu ni Ronald Reagan, Bill Clinton, George H. W. Bush, Gerald Ford, Jimmy Carter, Lyndon Johnson.
 
Wache aaibike kama kushuka huo kunamwaibisha kwa kiasi fulani kwenye jamiaa
 
Bush ametoka madarakani miaka miwili iliyopita kuporomoka kwa umaarufu wake kutamuathiri vipi?
 
Back
Top Bottom