Uma na kisu kwenye meza za hoteli

Uma na kisu kwenye meza za hoteli

Swali nililojiuliza kwanini wazungu wanakula kwa mkono wa kushoto ilhali ni mkono unaotumika kunawia chooni?

hivi personal hygiene si inakuhitaji uoshe mikono yote miwili tena ishikane ule unaojivunia msafi na ule mchafu ulioshika ambavyo waona havifai tena vimetoka mwilini mwako? Sasa mikono ikishikana katika kunawa yote hadhi yao si inakuwa ni sawa? Hakuna cha huu ni wa kushoto au huu ni wa kulia maana yote imesafishwa tena na sabuni tena kwa kupakazanapakazana ili itakate.

mengineyo ni mila na desturi tu ambayo zafaa sasa tuzitupe kapuni na kujinoma bila ya bughudha ambazo hazizingatii hali halisi.
 
huyo jamaa mwenye mke hakutembea ma talaka za akiba amuangushie palepale?? aibu gani hii

Jamani yaani ampe talaka mkewe kwa ajili ya aibu na kushindwa kula na umma na kisu? Je ingekuwa ndo mwanamme ndo hawezi na mwanamke ndo anaweza kutumia umma na kisu? ..............
 
We nawe, maelezo mareefu swali lenyewe mistari miwili...
Wazungu wanatumia mkono wa kushoto kulia chakula kwa sababu wanatumia toilet paper katia kujisafisha wakishajisaidia wakati sisi tunashika kinyesi kwa mkono wakati wa kujisafisha na maji baada ya kujisaidia, uwezekano wa kutoka na uchafu ni mkubwa kwa sababu ya kucha..... LOL

BTW
Swala la mkono gani utumike kwa kulia chakula ni la kijamii zaidi lakini sidhani kama kuna sheria iliyowekwa mahali kuwa ni lazima mkono wa fulani utumike wakati wa kula chakula.

Jamani kaka Mtambuzi mwenzio nilishajistukia ninamaelezo marefu na kufupisha siwezi, usilogwe kunialika kwako na ukanipa nafasi ya kuombea chakula, ntajikuta nawasalia hadi kizazi chako cha nne ambacho hata hakijazaliwa na naombea hadi mtaa wako wote. Haya back to the topic nashukuru kwa ufafanuzi wako ila hujaniambia watoto wako umefandisha kula kwa umma na kisu au kwa mkono tuu? kwa nini? kimtazamo wako tuu sorry kama ntakuwa nimeintafia intelejinsia yako.
 
Last edited by a moderator:
Si kosa lake bali mume alichangia, kimsingi mume alitakiwa ampe mkewe semina tangu nyumbani na ndio maana inashauriwa kuwa na vifaa vya kulia chakula kama vile uma na visu majumbani mwetu kwa ajili ya ku-practice.
Haya mambo ya kutumia zana za kulia chakula kwa mfano uma na kisu hakuna aliyezaliwa akiwa anajua, wote tumejifunza tena wengine wamejifunza ukubwani. kwa mfano chuo cha diplomasia pale Kurasini mojawapo ya kozi zinazofundishwa pale ni pamoja na table manner na matumizi ya glass mbalimbali na matumizi ya uma na kisu. hata hao wazungu wapo wanaojifunzia hayo mambo ukubwani. tusidanganyane hapa.....

ni kweli usemacho kaka kuelimishana na kufanya mazoezi nyumbani ni muhimu ili hata siku unapata wadhifa unaitwa ikulu uko high table na wakubwa hupati shida. Ila nimejaribu kuchunguza pia nimegundua kuwa wengi wa watumiaji wa umma na kisu huwa sahani inabaki na chakula kingi namaanisha huwa makombo kwenye sahani yanabaki mengi. Hii ni kwasababu ya ugumu wa kula kwa umma na kisu hivyo moja ya madoido ni kutokula sana hasa kula kuku au samaki, unakulaje kichwa cha kuku hadi ubongo wake na macho ya samaki kwa kutumia umma na kisu? Tofauti na mtu anayekula kwa mkono au kutumia kijiko sahani inabaki nyeupee labda msosi uwe mbaya. We jaribu kuchunguza kwenye hafla za umma na kisu watu wanokula kwa umma na kisu na wale wanaokula kwa kijiko na mkono mabaki ya sahani zao huwa tofauti. Na je mona ya sheria ya kula kwa umma na kisu hutakiwi kumaliza sahani yote? au wanakuwa washakula home pale wanarembaremba tuu?
 
Dada sakapal. haya mambo uloeleza yanahusu sana tamaduni za watu weupe. Kulingana na 'English table manners'
mkono wa kushoto ndo unakamata uma na wa kulia kisu. Kisu kinapakulia chakula (nyama, vipande vya mboga nk)kwenye umana mkono wa kushoto kupeleka chakula kinywani. Huku kwetu uswahilini, mkono wa kushoto una hadithi zake za maliwatoni. Uswahilini, ndani ya vyoo vyetu utakuta ndoo ya maji na kopo, na kama mhusika anajiweza ataweka bomba la maji. Ukimaliza shida zako mkono wa kushoto unashughulikia usafi kwa kugusa kabisa uchafu unaotakiwa kuondolewa! Na ndio maana mkono huu uswahilini hauheshimiki sana hata mtu akikunyooshea mkono shoto kukusalimu, unasita na kumshangaa! Kwa wenzetu wa magharibi Mkono wa shoto hauna kazi chooni sanasana ni wa kulia ndo ufanyao kazi ya usafi bila kugusa uchafu wenyewe maana wao wanatumia karatasi laini. Kwa hiyo kwao mkono shoto hauna kinyaa hata kidogo kiasi kwamba wanautumia kupeleka chakula kinywani kwa njia ya uma.

Kwa kuwa ulimwengu huu umejaa utamaduni wao ni vizuri kuwafundisha watoto wetu jinsi ya kula kwa kutumia uma na kisu. Mimi binafsi sijaanza hili somo maana bado sijanunua uma wala visu vya mezani. Nataka nianze masomo haya mwezi Julai mwaka huu.Kufahamu kula kwa kutumia uma na kisu mezani ni stadi muhimu sana kwa watoto wetu.

hygeia

asante kwa maelezo yako nimekuelewa vizuri wacha nami nianze darasa kwa watoto wangu wasije aibika mbele za watu
 
Kushika kisu kwa mkono wa kulia (wenye nguvu) husaidia ukataji wa chakula.
Ndio maana hata wanaotumia mkono wa kulia kushikia umma, ikifika muda wa kukata chakula hubadilisha. So kuepusha kubadilisha badilisha mikono bora umma uzoee kwenye Mkono wa kushoto.

Ngoja nimuite muingereza wetu wa ukoo aje atumbie zaidi. KIKUNGUuuuuuuu!!!!!!!
Kaunga asante kwa maelezo je ni vyema kuwaelimisha watoto wetu utumiaji wa umma na kisu au tuwaachie wazungu utamaduni wao?
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
kujifunza ni muhimu ili usijeaibika kunako. namshukuru bi mkubwa aaah sijapata shida.
ila kupata utamu wa chakula shurti ule kwa mkono. so mara nyingi i do not care nipo kwenye sherehe ip au wapi na nani sijui, ninapohitaji kujifaidia najifaidia kwa kula kwa mkono so long as ni msafi!
shida ya nini mie!
 
Mmmh ilumbuye Kaunga kusema kweli hata sijui kwa nini wazungu walileta hii,Uma kushoto,kisu kulia lakini kwangu mie it is just natural kushika uma na mkono wa kushoto wakati nakata na kisu na mkono wa kulia,it is more comfortable kuliko kushika uma na kula kwa mkono wa kulia wakati unakata kwa kisu na mkono wa kushoto.
Tatizo sisi waafrika tuna penda pia kutukuza tamaduni za kimagharibi bila sababu kwani kwenye function kama hiyo kutumia kisu na uma sio lazima afterall hujazoea.Wakati nasoma nilikuwa nakaa kwenye student's apartment moja na couple wa kifaransa sasa siku moja moja nilikuwa najipikia ugali wangu na kwa sababu tulikwa tunashare jiko na dining,siku ya kwanza walishangaa kuniona nakula ugali kwa mkono,mke wa yule mfaransa sijui alileta lile swali kwa nia ya ubaguzi au vipi sijui,alishanga kwa nini nakula na mikono na akaniuliza nam-quote "..........can you eat by feet as well....".Sikukasirika ila nilimuelewsha asili na tamaduni zetu zikoje.Siku moja nikapika pilau na nikawakaribisha na kuwaambia kuwa pilau huliwa kwa mikono na nikawafundisha,it was a struggle maana punje hata ishirini zilikuwa hazifiki mdomoni.Sasa itafuja wewe hujazoea uma halafu ule wali kwa uma.
Kitu cha msingi kuwa free kutumia utamaduni/mazoea uliyokuwa nayo as long as huvuji taratibu/sheria ya hapo ulipo

nimekubamba na nimependa hiyo scene yako na huyo mke wa kifaransa, nimekufananisha na mtu fulani hivi kwa faida ya wengi namreserve. ila hata uandishi wako mnafanana mno. Back to the topic asante kwa maelezo na ushauri, ila wewe binafsi unafikiri kuwafundisha watoto wetu kutumia umma na kisu ni sawa?
 
Aiseee kaka yangu mstaarabu, maana mimi ningemtukana huyo mfaransa mpaka angekuwa mwekundu.

Umesema kweli, hii Eurocentric mind inatusumbua sana, nimemfikiria huyo dada alodondokewa na kuku mwenye michuzi sijui ilibidi aondoke baada ya kula, au hakunyenyuka tena alipokaa.

yaani huyo mke wa yule jamaa alivoomba msamaha kwa huyo dada aliyedondokewa na kuku kwenye gauni yake ikabidi tu yule mdada amsamehe na shukuru mungu gauni yake ilikuwa nyeusi, hakuondoka mezani alinywea tuu na kumalizia msosi wake ila baada ya mlo alienda jirekebisha kidogo maliwatoni.
 
Kama Kaunga alivyosema, mkono wa kulia unafaa kwa kushika kisu wakati wa kukata.

Ila bora kula kwa mkono kama hujui kutumia uma na kisu kuliko kujiaibisha.

Niliwahi kwenda hotel moja mji fulani, kuagizza msosi nikaletewa vile vijiti vya kichina, nilichokaje?

Nimejifunza hadi leo, siagizi aina hiyo ya msosi tena, labda niwe home. Yaani nguvu inayotumika kushika vijiti ni bora kulala bila kula angalau utakuwa na vinguvu vimebaki.

hapo kwenye red umenichekesha mnooooo hahahahahahahaaaaaaaaa!!
 
Kaunga asante kwa maelezo je ni vyema kuwaelimisha watoto wetu utumiaji wa umma na kisu au tuwaachie wazungu utamaduni wao?

Nafikiri ni vyema kuwafundisha, huwezi jua hili gurudumu la maisha litawapeleka wapi.
 
kujifunza ni muhimu ili usijeaibika kunako. namshukuru bi mkubwa aaah sijapata shida.
ila kupata utamu wa chakula shurti ule kwa mkono. so mara nyingi i do not care nipo kwenye sherehe ip au wapi na nani sijui, ninapohitaji kujifaidia najifaidia kwa kula kwa mkono so long as ni msafi!
shida ya nini mie!
mimi napenda sana kujua matumizi ya vitu vingi ingawa sipendi kuvitumia....
kwangu nina hadi chop sticks kwa ajili ya kuwafundishia wanangu kutumia.....
mwenyewe nikijimwaga kwa hotel za kichina/kijapan aku... kwa raha zangu.... hadi wali nakula kwa chop sticks........
ila sasa utamu wa msosi hasa pilau/ugali bila mkono aisee naona kama sitashiba, lol!
 
nimekubamba na nimependa hiyo scene yako na huyo mke wa kifaransa, nimekufananisha na mtu fulani hivi kwa faida ya wengi namreserve. ila hata uandishi wako mnafanana mno. Back to the topic asante kwa maelezo na ushauri, ila wewe binafsi unafikiri kuwafundisha watoto wetu kutumia umma na kisu ni sawa?

Nitakutafuta sakapal.Back to topic nafikiri ni muhimu sana kama unapata muda wa kuwafundisha watoto table manner kwa desturi zote mbili,yaani ya kiafrica na kimagharibi kwa sababu dunia imebadilika sana,mnaweza karibishwa sehemu ambayo kutokana na mazingira ya pale ni ya kimagharibi(kutumia uma na Kisu) zaidi au ya kiafrika zaidi(kukaa kwenye jamvi/mkeka na kula kwa mkono)kwa hiyo watoto waweze kuji-tune kutokana na mazingira.Nina mfano hai,watoto wangu hawakuwahi kufika nyumbani,bongo,mpaka walivyokuwa na umri wa miaka saba na mitano,sasa kutokana na matumizi ya vyoo vya kukaa,(Europe ni very rare kukuta Indian WC),mtoto wangu mdogo siku ya kwanza kwenda chooni kwenye choo cha kuchuchumaa alishindwa kujisaidia kwa sababu alikuwa hajawahi kuona/tumia hicho kitu.Maana yangu ni kwamba ni bora kuwa-expose watoto na mazingira tofauti tofauti mapema otherwise wanaweza kuwa vituko
 
acha nipite..... Maana mie situmii uma na kisu hata niwe wapi.....ni mkono au kijiko atakayenuna ahame meza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom