sakapal
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,804
- 1,425
Habari zenu wana mmu,
poleni na majukumu ya maisha yanayowakabili, baada ya kimya kifupi cha kukabiliana na shuhuli za kuingiza shekeli kule bandarini weekend hii nilikutana na kioja hiki nikaona ngoja nije nishirikishe wana jamvi walidadavue kila mtu kwa mtizamo wake.
Jumamosi nimejikwatua kwatu na kuridhika barabara kiasi kwamba ntapata salamu hadi kwa mtoto kwa jinsi nilivotokelezea (nilivopendeza) msishangae najisifia kupendeza raha jipe mwenyewe ukingoja kupewa....................
Basi bana (mnisamehe kwa kuwa na maneno mengi katikati ya habari yenyewe) ndivyo nilivo huwa nashindwa kufupisha stori. Sasa nilikuwa naenda kwenye hafla ya kampuni fulani (naomba kuihifadhi kwa sababu za kiintelejinsia) namie nilialikwa kama mdau wa kampuni hiyo, nilikuwa mwenyewe baba Rainer alikuwa safarini kikazi hivyo saa kumi na mbili jioni nilikuwa nshafika eneo la tukio (nikiwa naenda kwenye hafla mwenyewe bila baba Rainer huwa napenda kuwahi kufika ili niwahi kurudi, hii ji sehemu ya wivu tu wa baba Rainer maana huwa mawasiliano yanakuwepo kila saa utaskia party haijaisha? si urudi tuu nyumbani). Sasa bana nikaingia ukumbini na nikatafuta meza iliyo katikati ya ukumbi na kukaa (huwa sipendi kukaa mbele sana wala mwisho kwasababu za kiintelejinsia) sherehe ilianza kama saa moja kamili mziki kwa sana vinywaji vya kila aina na muda masosi ulipofika ndo picha ilianza. Kwenye meza niliyokaa walikuwa watu wengine 9 (zilikuwa meza za round za kukaa watu 10) kati ya hao 9 kapos 2 na wengine 5 wako single yaani kila mtu kivyake. kufika kwenye bifee kila mtu kujisevia kwa minajiri ya tumbo lake na ukubwa wa kifuko chake cha kuhifadhia chakula kilichomeng'enywa. Ile kurudi mezani kila mtu ashambulie sahani yake na mie mpango wangu nikimaliza kula na nikicheza miziki 2 tu nasepa zangu home. Kwa vile nilikuwa alone nilikuwa nakunywa sweet wine nachanganya na juice hivyo sikuwa alcoholic. Sasa wakati tunakula moja ya kapo mkewe inaonesha ndo alikuwa anajifunza kula kwa uma na kisu na ikaonekana hakutaka kuonekana wa bush maana mumewe alimnong'oneza ale kwa mkono tuu kama mumewe alivokuwa anakula kuku kwa mkono ila mkewe hakukubali. Heee huku na kule kwenye kukata kuku fyuuuu ikamuangukia dada mmoja jirani yake kwakuwa ilikuwa na michuzi ikamchafua gauni ya yule dada. akaomba msamaha yakaisha tukaendelea kula mumewe akasikika kwa minong'ono ya chini pale mezani akimsisitiza mkewe amalizie kula chakula kwa mkono au kijiko maana ule uma na kisu vilikuwa vinampa shida kwani alikuwa akichota umaukifika mdomoni unapunje 3 za wali na salad vingine vimedondokea kwenyesahamni. Kwa kifupi yule mkewe hakuweza kutumia uma na kisu hasa ukiangalia mkonoaliokuwa anatumia kula ni wa kushoto huku wa kulia ndo umeshika kisu. Naomba nihifadhi yaliyotokea baada ya hapo na nije kwenye dhumuni la kuleta mada hii hapa.
Swali nililojiuliza kwanini wazungu wanakula kwa mkono wa kushoto ilhali ni mkono unaotumika kunawia chooni?
wakati mimi nakua nimefundishwa kula ka mkono wa kulia na marufuku kula na mkono wa kushoto ukionekana hata mkong'oto unatembezewa ila huku ukubwani vyuoni na makazini ndo tumejifunza kula kwa umana kisu na umma unaushika mkono wa kushoto na watu wanakula hivyo na unaonekana wa kisasa. Je nisawa? na ukienda sehemu hizo za hoteli na ukala kwa mikono au kutumia kijiko tuu kama nyumbani kwako kuna shida?
Au wazungu kwakuwa wananawa kwa kutumia tissue na hawali kwa mkono ndo maana wanakula kwa mkono wa kushoto kwa kutumia umma? kwa nini umma huo usishikwe mkono wa kulia na kisu kushoto? Au wazungu wananawa na mkono wa kulia na kulia kwa mkono wa kushoto na sie tunawaiga tuu bila kujua siri yao?
Jamani naombeni msaada wa hayo maswali, karibu kila mmoja kuchangia kwa ufahamu ulionao kuhumu table manners ukizingatia kula kwa mkono, wa kulia au wa kushoto, kwa kutumia umma au kijiko.
Mwisho wewe mwenye mtoto unayesoma hapa, mtoto wako umemfundisha kula kwa mkono gani? kwa nini?
Na je, umemfundisha mtoto wako kula kwa umma na kisu? kwa nini?
KARIBUNI WOTE .............
its me Sakapal