- Thread starter
- #81
nimesoma post zote na mleta maada nikagundua jambo la ajab sana, awali mkao wa maada na jukwaa alilotumia mleta maada haviendani na mlolongo wa majibu..
Nimeyapenda majibu yake kwamba ni kweli au si kweli inabakia kwa masomaji mwenyewe lakini mleta maada anajitahidi kujibu kwa weledi na si kipuuzi au utani kama jukwaa alilotumia, na kwa maana hiyo basi hata wauliza maswali wengi maswali yao ni ya jokes na katuni lakini mleta maada aliulizwa swali kwanini umepost post ya kipuuzi, mleta maada akadefend kwamba post yake si ya kipuuzi kwa sababu asilimia 98 ya matatizo ambayo ama mwanadam anakutana nayo au anajidumbukiza matatizoni ni kutokana na kukosa majibu ya maswali kadhaa kwenye njia ya maisha yake ambayo to me ni ukweli usiopingika..
Najaribika kuwaza mleta maada anaweza kuwa na 'kitu' .. Siulizi swali bali nashauri maada yake ama mods waibadilishe jukwaa au ailete kwenye majukwaa fikirishi .. Huku huwa tunakuja kufanya brainwash and nothing very serious you gona expect to meet kwenye jokes,gossips forum..
kutokana na hoja ulioitoa nakubaliana na wewe kuwa hii mada sikupaswa kuitoa kwenye jukwaa hili. Na nimeufunga rasmi mjadala huu na kuwaomba memba wote wasiendelee kuuliza maswali tena kwani sita-respond