Walimtafuta ex wangu wakamwambia nadaiwa 🤣🤣
Ila wale wanadai bana.
Ila nilipojua kuwafungia call, walikoma
Pole sana Kaka. Mimi nakumbuka yalinipata nilipokopa kwenye app za Zima Cash, Cash X na Pesa X. Walituma SMS hadi kwa ndugu wa damu na marafiki zangu kwamba ninadaiwa kisa tu, nimechelewesha marejesho!
Nilipata auheni kipindi cha app ya Branch International. Nilikuwa nikikopa na kufanya marejesho bila stress tena walikuwa wazungu kwelikweli. Hawakusumbui ovyoovyo, hawatumii SMS zenye kauli za ajabu wala hawawatafuti mtu yeyote yule zaidi ya wewe.
Walinifurahisha sana hasa kwa upande wa viwango vyao vya malipo na hata muda wa kufanya marejesho. Ilipofika siku ambapo niliona hawatoi huduma tena nililia sana. Mpaka leo hii bado nawakumbuka.
Hawa wengine ni Waswahili tu! Hawajui kudai, hawajui kufuata taratibu za kwenda na kipindi ambacho unapaswa kufanya marejesho, mtu umebakiza siku mbili kufanya marejesho, unapigiwa simu ukiambiwa; "Fanya marejesho leo hii ili upate kukopa zaidi!" Au "Fanya marejesho leo ili wengine waweze kukopa!" Sasa, mimi ninategemea kukopa tena kwenu? Au, hao wengine wananihusu nini? Nikipata mapema nitalipa mapema, nikipata ndani ya siku hiyo ya marejesho, nitarejesha siku hiyo!
Ushauri wangu, kopeni benki kupitia app za benki(Sim Banking, NMB Mkononi, n.k.) au za kwenye mitandao ya simu kama Vodacom na Yas(Mgodi, Nivushe Plus, Songesha, n.k.) achana kabisa na hizo za mitandaoni!