Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 6,441
- 13,550
Sote tunafahamu ukali wa maumivu ya moyo na mwili pale unapo mpenda na kumuamini mtu halafu analeta ufala na kuishia kukuumiza.
Hii hali linapotokea huwa inakuacha na maumivu makali sana ambayo huchukua muda kupoa na kuisha. Kuna ambao tiba ni kusamehe na kusahau na kuanza upya, kuna wale ambao hawakubali hadi walipizie.
Leo nawalenga hawa ambao hawakubali hadi walipizie ndio roho zinakubali utulivu na kuachia maumivu. Mimi nipo kundi hili pia.
Sifa moja ya watu wanaolipiza kisasi hadi kinatimia ni kuwa wao binafsi hawapendi kuumiza wengine hivyo wakikosewa huwa hawakubali hadi wahakikishe yule aliyewakosea kwa makusudi ameondoka na somo au funzo la kuja wahadithia wajukuu zake na asije mkosea tena mtu mwingine maishani mwake na ajue alikosea mtu wa kuchezea.
Kwa experience yako unakumbuka ulitoa somo gani na kwa nani (mwanaume au mwanamke) na ilimgharimu vipi hadi ukajua?