Hii ndizo siri kubwa kwa nini unalipa bili kubwa ya umeme,kuliko matarajio yako.

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Habari wanajamvi,


Hakuna asiye yajua maumivu ya bili kubwa ya umeme iwe masikini ama tajiri.Katika makala hii nitazungumzia namna ambavyo unaweza kupunguza bill kubwa ya umeme katika makazi yako.


Uchambuzi nitakao ufanya hapa unarejea tafiti nyingi za matumizi ya nishati ya umeme ambazo zimefenywa na taasisi binafsi za umeme zikizingatia sheria ambazo ziko chini ya ya IEE regulation ambayo inasimamia kanuni za uunganishaji na matumizi ya umeme yalio salama.


Pia maelezo haya yatahusisha pia utafiti mwingine ulio fanywa na kampuni ya umeme ya Edison Electric Institute (EEI) ambao ni watafiti na wagunduzi wa maswala ya umeme ikiwa na makampuni wanachama yanayo sambaza umeme karibia kaya milioni 220 duniani.


Uchambuzi huu utasaidia kupunguza hasara ambayo si ya razima kwa mtumiaji wa umeme,pia ifahamike kuwa uchambuzi huu utaepuka aina yoyote ya michanganuo ya kitaalamu na kiufundi,ili kumwezesha kila mmoja hata asiye mtaalamu wa umeme aweze kunufaika na uchaambuzi huu.


Hapa Tanzania watu wengi wamekuwa wakiteseka na bili kubwa ya umeme;wengine wakijaribu kuita mafundi kutazama tatizo lakini mara nyingine hata baada ya fundi kufanya marekebisho bado bili inakua palepale.


Tafadhari fatilia mchanganuo huu vizuri hatua kwa hatua naamini kwa asilimia flani utasaidia kupunguza​
Gharama za maisha katika kaya yako

WATUMIAJAI WA AIR CONDITION


1.Epuka kufunga air condition compressor maeneo yenye nafasi ndogo mfano uchochoro,maeneo yenye msongamano wa miti n.k.Funga compressor ya air condition eneo ambalo itakuwa free in air,kuifunga compressor katika eneo lililo bana inasababisha compressor kutumia nguvu nyingi zaidi hivyo kuongeza matumizi yake ya umeme.
6691030_f520.jpg 9a367fc293f308145e54ac720f3f4e3d.jpg


2.Epuka kufunga compressor ya air condition katika mwelekeo unao pigwa na jua muda mrefu katika siku,kabla ya kufunga compressor ya air condition hakikisha unafanya utafiti kujua ni upande upi ambao jua halipigi kwa muda mrefu katika siku,Upande ambao una kimvuli kwa muda mwingi katika siku ndio unafaa kufunga mtungi wako wa air condition.Sababu hii ya 2 pia izingatia sababu namba 1 hapo juu.


3.Tambua sehemu zenye upenyo ambao unaweza ukawa unaingiza hewa wakati air condition ipo ON,hakikisha madirisha na milango vinafungwa vizuri ili kuipunguzia mzigo air condition kutumia nguvu nyingi katika kukipooza chumba husika,kwani kama itatumia nguvu nyingi basi itaongeza pia bili ya umeme.


Pia kama air condition ipo katika sebule ambayo ina milango ya vyumba vingine hakikisha milango ya vyumba hivyo pia inafungwa ili kupunguza space ya hewa ya baridi ku-cover eneo husika tu.


4.Hakikisha kipimo cha baridi unacho kiweka kiwe kile cha juu ambacho unawezakuhimili,kwani unavyoweka kiwango cha juu cha baridi ndivyo unavyo tunza nguvu kuliko unavyo set baridi kidogo.


5.Epuka kuweka vifaa vinavyo zalisha joto kama vile TV za ukutani ama Fridge jirani na Air condition thermostart,kwani joto linalotoka katika vifaa hivyo linaweza kuidanganya thermostart ya air condition ikahisi joto limeongezeka katika chumba kumbe ni joto liliozalishwa na TV ambayo iko jirani yake.Hali hii itasababisha thermostart iendelee kuiwasha compressor hata wakati baridi usika imesha fikiwa katika chumba,hivyo hali hii itapelekea matumizi ya umeme kuongezeka.
llllllllll.jpg black-friday-home-depot-fridge.jpg


5.Jaza gesi katika mitungi ya air condition ambayo imepungua ama kuisha,kama gesi itakua imeisha ama kupungua kwa kiasi kikubwa compressor itafanya kazi kwa muda mrefu zaidi katika kufikia kiwango flani cha baridi,mfano kama ilibidi compressor ifanye kazi kwa dakika 10 kupooza chumba kimoja,compressor itafanya kazi zaidi ya dakika hizo hivyo kupelekea kuongezeka kwa matumizi ya bili kubwa ya umeme,Jitahidi kufanya repair ya air condition zako mara kwa mara ili kuepuka tatizo hili.


WATUMIAJI WA MAFRIJI NA FREEZER


1.Epuka kuweka maji ambayo hayajafunikwa katika friji lako,sababu za kitaalamu zinaonyesha kuwa kama utaweka maji katika friji lako na maji hayo yakawa katika chombo cha wazi basi maji hayo hutengeneza mvuke kabla ya kupoa mvuke huo husababisha friji kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo ungefunika maji hayo wakati wa kuyaweka katika friji ili kuzuia mvuke wake kusambaa ndani ya friji.


Hapa haijarishi kama maji ni ya moto,vugu vugu au baridi yakupasa kufunika maji yako wakati wote unavyo yaweka katika friji.Hivyo jitahidi kuweka maji kwa kutumia chombo ambacho ni rahisi kukifunika mfano gallon n.k.


2.Epuka kuweka vyakula vya moto ambavyo bado havijapoa katika friji lako.Subiri hadi pale chakula chako kitakapo poa ndipo uweke katika friji lako.


Uwekaji wa vyakula vya moto katika friji husababisha compressor kufanya kazi kwa muda mrefu ili kufidia kiwango cha joto kilicho ongezwa kwa makusudi katika friji hali hii hupelekea ongezekokubwa la bili ya umeme.


3.Kila baada ya miezi mitatu safisha condenser coil ambayo iko ndani ya friji lako,mtafute mtaalamu wa kusafisha condenser coil.Kwani kama condenser coil isiposafishwa itasababisha compressor kufanya kazi muda mrefu ili kufikia kiwango flani cha ubaridi.
coils.jpg

Hivyo hali hii itapelekea kuongezeka kwa bili kubwa ya umeme.


4.Hakikisha mipira ya mlango wa friji iko imara,mipira hii husaidia mlango wa friji kufunga vizuri ili kuzuia hewa ya joto kujipenyeza ndani ya friji.Ili kuthibitisha kama mipira ya friji ipo sawa weka fedha ya noti katika mrango wa friji kasha funga mlango wa friji;kama utaweza kuivuta noti hiyo iliyobanwa na mlango wa friji kirahisi basi ujue mipira ya mlango wa friji imesha dhoofu na inahitaji kubadilishwa.

august-home-maintenance-to-do-list-7-refrigerator.jpg


5.Hakikisha friji lako lina kifaa cha kutambua kiwango cha joto ambacho kitakuwa kikiwasha au kikizima friji kutokana na kiwango flani cha joto ulicho chagua,ukiona compressor ya friji lako inawaka mfurulizo bila kujizima tambua kuwa friji lako lina tatizo na ili kuepuka bili kubwa ya umeme hakikisha unamuita fundi aje alikaugue ubovu wake kitaalamu.


6.Epuka kujaza vitu vingi kuliko ujazo ulioshauliwa katika kitabu cha matumizi cha friji husika,Kila friji lina kiwango chake cha ujazo wa vitu ndani yake katika upande wa freezer na ule wa refrigerator.


Kujaza vitu vingi katika friji au freezer linasababisha compressor kufanya kazi muda mrefu bila kujizima kwa sababu friji au freezer inakua ikishindwa kutengeneza joto linalo takiwa,hivyo thermostart yake huendelea kuiwasha compressor kwa muda mrefu hadi pale ubaridi husika utakapo fikiwa.


Hivyo kama utakuwa umejaza vitu vingi kuliko ujazo harisi wa friji utasababisha compressor kuwaka kwa muda mrefu bila kujizima kwasababu ubaridi husika unakua mgumu kupatikana kutokana na friji kujazwa vitu vingi zaidi ya vile inavyo shauliwa.
Winter 2011 033.JPG


7.Jaza gesi ya friji mara tu unapo hisi au kutambua kuwa imeisha,jitahidi kulifanyia service friji lako angalau mara moja kwa miezi mitatu hasa kwa mafriji yale yenye umri zaidi ya miaka miwili.Kama gesi itakua imepungua au kweisha compressor hufanya kazi muda mrefu zaidi ya kawaida kufikia kiwango flani cha joto,kutokana na kiwango cha gesi kuwa kidogo.


Kama compressor itafanya kazi muda mrefu itapelekea bili ya umeme kuwa kubwa zaidi.


WATUMIAJI WA MAJIKO YA UMEME NA OVENA


1.Hakikisha sufuria inayotumia kupikia au kuchemshia kitu chochote katika jiko lako la umeme kitako chake kipo tambalalek isiwe kimebonyea au kimebinuka kwa sababu kama kitakua kibebinuka au kubonyea kitasababisha sufuria hiyo kuto kukalia kitako cha jiko vizuri hivyo kuna kiwango cha joto kitakua kikipotea bila kutumika.


Hali hii susababisha kitu kinacho pikwa kuchelewa kufikia hatma yake kutokana na kiwango cha joto kupotea,japo kuwa joto hilo linapotea bila kutumika lakini mita yako ya umeme itakuwa inahesabia kiwango chote cha umeme unacho tumia hata ule umeme uliotumika kutengeneza joto lililo potea utaulipia.


2.Safisha plates za jiko lako mara kwa mara.Vitako vya jiko mara nyingine hujawa na utando wa uchafu au kutu zilizo ganda juu yake,Jitahidi kuondoa uchafu huo uliogandia katika plates hizo,kwani uchafu huo hupunguza kiwango cha joto kinachosafiri kutoka katika kitako cha jiko kwenda katika kitako cha sufuria hali hii husababisha kiwango flani cha joto kupotea bila kutumika jambo ambalo linaongeza matumizi ya umeme yasiyo ya lazima.


3.Anza kupikia kwa joto la juu hadi pale kile ulicho kitenga kitakapo anza kuchemka unaweza kupunguza joto na kuendelea na mapishi yako.Epuka kuanza kupika kwa joto la kawaida kwani husababisha umeme mwingi kutumika kwani kile ulicho kitenga kitakawia kupata joto.


4.Kwa matumizi ya kupasha chakula n.k,inashauliwa kutumia OVENA zaidi kuliko jiko la umeme,ovena inatumia umeme kidogo zaidi sababu inapasha chakula kwa haraka zaidi.Pia kwa matumizi ya ovena utakuwa umepunguza kwa asilimia 50 ya bili ya umeme,dhidi ya matumizi ya jiko la umeme.


WATUMIAJI WA HEATER ZA MAJI


1.Epuka kuacha maji katika container ya heater,hakikisha maji yaliomo katika container la heater yanaisha yote baada ya kumaliza kutumia.Kama utaacha maji katika container la heater mara nyingi husababisha kutengenezwa kwa kutu katiaka heater coil hali ambayo baadae husababisha kiwango cha joto kupotea kutokana na kutu kuizunguka coil inayozalisha joto.


Joto hili linalo potea bila kutumika linaongeza bili kubwa ya umeme kwa sababu umeme umezalisha nguvu ambayo imepotea bure bila kutumika.


2.Inashauliwa watumiaji wa heater kukinga maji ya kuoga ya moto katika mabeseni,ndoo au masinki Haishauliwi kuoga maji ya moto ambayo moja kwa moja yanatoka katika bomba la heater kwani kitendo hicho kitasababisha heater kufanya kazi muda wote ambao unakuwa unaoga,wakati kama ungeamua kujaza maji ya moto katika beseni heater ungeiwasha wakati wa kukinga maji hayo mfano dakika mbili tu na ndoo ikisha jaa maji moto unaizima heater na kuoga maji amabayo umekinga ambayo tayari ni ya moto.


Lakini kama utaoga moja kwa moja maji ya,moto yatokayo katika heater basi heater yako itabakia kuwa ON hadi pale utakapo maliza kuoga,mfano kama utaoga dakika 30 basi heater nayo itakuwa ON dakika 30.Na kama ungekinga maji katika ndoo yako au beseni lako au sinki lako heater ingewaka kwa dakika moja au mbili tu.Hivyo ni gharama kubwa sana ya bili ya umeme utakua umesave.(SAVE YOUR BILL
BY TAKING BATH AND NOT SHOWER).
WATUMIAJI WA TAA


1.Matumizi ya taa ambazo zinajulikana kama Energy saver ndiyo yanashauliwa kutumika katika makazi yetu kwani zimeonekana kukabiliana na tatizo la bili kubwa ya umeme vizuri zaidi.


2.Taa ambazo zinasauliwa kuzimwa hasa taa za nje ni vizuri ukafunga mfumo wa taa kujiwasha na kujizima zenyewe,hii itasaidia kuzuia taa kuwaka mchana,hivyo kupunguza matumizi ya umeme yasiyo ya lazima.


Pia katika hili wengine hufunga mfumo wa taa kuwaka kila baada ya muda flani na kujizima ,kwa kujirudia rudia,utaratibu unakua huo huo hadi asubuhi.


Pia kuna taa ambazo hujiwasha pale tu kitu chochote kinaposogele eneo la nyumba,na kama hauna kitu chochote kitasogelea taa hazita waka usiku mzima,hivyo zitakua zimesave energy kwa kiwango kikubwa.


3.Taa katika vyumba vya watoto.Kama watoto wanasomea katika vyumba vyao hakikisha unawawekea taa mbili,moja ya kumulika chumba kizima ambayo mara nyingi hua na mwanga mkubwa,pia taa ya kusomea ambayo huwa ya mezani mara nyingi huwa na mwanga mdogo.


Taa ya kumulika chumba kizima mara nyingi huwa mwanga zaidi hivyo hutumia energy nyingi zaidi hivyo kama taa hiyo itatumika kusomea itabidi iwake kwa muda mrefu zaidi hivyo kutumia energy nyingi zaidi.


Inashauliwa kama chumba cha kulala pia kinatumika kusomea taa ya mezani ya kusomea ni muhimu zaidi kwani huwa na mwanga mdogo pia hutumia energy kidogo hivyo kama mtumiaji wa chumba atahitaji kujisomea atazima taa ya mwanga mkali na kuwasha taa yake ya mezani kwa ajili ya kusomea.


WATUMIAJI WA VIFAA VYA ELECTRONICS


1.TELEVISION



-Matumizi ya LCD TV ni bora zaidi katika matumizi ya umeme zaidi ya PLASMA TV.Nikimaanisha LCD
TV zinatumia umeme mdogo zaidi kuliko PLASMA TV ambazo zinakula umeme zaidi.
-Epuka kuzima TV kwa kutumia Remote control,TV inapozima kwa kutumia remote control hua haizimi kabisa bali huingia katika standby mode,TV ikiwa katika standby mode huendelea kutumia kiasi flani cha umeme,Hivyo TV itakua inatumia umeme na kuongeza bill yako pasipo ulazima.Ni vizuri kuzima TV yako au kitu chochote kinachotumia umeme katika switch yake au katika switch ya ukutani (Socket).


2.COMPUTER



Computer kama haitumiki ni vizuri ikazimwa,hata kama computer hujiweka katika sleep mode isipo tumika kwa muda flani,lakini haimaanishi haitumii umeme,hivyo kama huna matumizi na computer husika hasa DESKTOP computer,ni vizuri kuizima kabisa ili kuzuia computer isiendelee kula umeme.


3.CHARGER
Epuka kuacha chaji za simu,laptop au TV katika socket bila kuzima,Vifaa hivi huendelea kutumia umeme hata kama havitumiki.

MWISHO

Taarifa hii imeandaliwa na Transistor,Na inatolewa bure kwa Watanzania wote.

Tafadhari makala hii isihaririwe kwa machapisho mengine.



Pia waweza kusoma makala zangu nyingine hixi hapa


SABABU TANO KWAMBA NYUMBA YAKO IPO KATIKA HATARI YA KUUNGUA MOTO WA UMEME.


VOLTAGE SURGE NI HATARI AMBAYO WENGI WANAISHI NDANI YAKE.
 
Hapo kwenye automatic lights system mtaalamu nipo pia relays kwa wenye three phase nawawekea kupunguza Copper loss kwani umeme unapo flow tu kunakuwa na power wastage ivo kama ukifunga relay ita minimize
 
Back
Top Bottom