Ulitumia muda gani kumpata uliyenaye?

Ulitumia muda gani kumpata uliyenaye?

Aisee kweli kazi ipo!
Kwani shida iko wapi ...Siku hizi mpesa na tigo pesa zimebaki za kuwatumia wazee vijijinii lakini nyie panda mwendo kasi...na kwa kuwasaidiaa unachukua bodaboda ukifika analipwa anasepa
 
Pamoja na yote hayo hadi kubadili njia lakini akakunasa! Chezeya kidume kikipenda hakichoki kufukuzia mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima lol!

Aisee, ilinichukua mwaka na..., kumkubalia huyu bae wangu!!! Jamaa alikuwa msumbufu balaa, kuna wakati ilikuwa inanilazimu kubadili njia ili tu nisikutane nae..... Hahahah daah, basi tuu
 
Kwani shida iko wapi ...Siku hizi mpesa na tigo pesa zimebaki za kuwatumia wazee vijijinii lakini nyie panda mwendo kasi...na kwa kuwasaidiaa unachukua bodaboda ukifika analipwa anasepa
Ukinambia hivyo hunipati hata kwa mzizi! Yaani ukishasema oooh kopa ukija nitalipa na blah blah za hivo nakutia kapuni nasonga mbele. Bora unambie huna hela ili kama vp nitumie pesa zangu nijue mara moja!
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Pamoja na yote hayo hadi kubadili njia lakini akakunasa! Chezeya kidume kikipenda hakichoki kufukuzia mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima lol!
We acha tuu, ilibidi niwe mpole!!
 
nimeanza mwezi wa 10 mwaka jana mpaka sasa hakieleweki na bado sijakoma
ngoja nisubscribe huu uzi akikubali nakuja kukupa data
mpaka sasa nina miezi 7 score board inasoma 0-0
 
Ukinambia hivyo hunipati hata kwa mzizi! Yaani ukishasema oooh kopa ukija nitalipa na blah blah za hivo nakutia kapuni nasonga mbele. Bora unambie huna hela ili kama vp nitumie pesa zangu nijue mara moja!
Utawaweka kapuni wangapi ??

Tatizo na nyie ukishampata mtu unamtwisha mizigo yote mpaka majukumu ya mzazi unataka afanye
 
Akikaaa mwka ndo akujibu kwan anafanya uchunguzi ili agundue nn
Enzi hizo ukitupia nyavu anakuchunguza wewe na ukoo unao toka maana walikuwa na masharti mengi sana siku hizi ukirusha nyavu unatoka nae hapohapo maana anajua asipo kukubali wengne watachukua nafasi
 
Ni enzi hizo mkuu

Wakati huu nitawezaje kukuchunguza ili hali kwenu ni Lindi na mie kwamatindi ndani ndani huko,

Km sina kizuizi na nakuona unafaaa kwann tusimalizane hapo hapo kuliko kufanya mambo kuwa magumu?
 
Back
Top Bottom